Afrika Kusini sio salama, kuna Watanzania wameuawa siku za karibuni

Hatusemi vibaya marehemu lakini sura tu zinawasaliti kwakweli.

Vijana tufanye kazi halali tuishi maisha yaliyo ndani ya uwezo wetu tuwe smart kimuonekano na zaidi kama hakuna ulazima tubaki tupambane tukiwa nyumbani

Ni hayo tu.
Hatuwezi wote tikafanya kazi halali

Mkuu,dunia uwanja wa fujo

Ndomana kuna magereza,polisi nk

Ova
 

Nakuunga mkono kwa 100% , na ulibadilika baada ya kupata muongozo sasa wenzako hawana hiyo bahati kwanza tunadanganyana kwa madiba mserereko hakuna kitu kama hiyo na wabongo wenye vyeti wachache wengi wanaishi kimagumashi sana, hata awe na pass unakuta muhuni kapitisha miaka kibao, acha wale wanaodandia maroli kutoka malawi au wanapita maumbiji kwa kuchana senyenge, zote hustle lakini kwa dunia ya sasa tuelezane ukweli bila hivo tutapoteza wengi
 
Niliwahi kufika mayotte katika harakati za kuruka ufaransa nikajifanya mkimbizi wa burundi, nikaumbuliwa na jamaa mburundi nikabaki pale town nikaona warundi wanavyouza matunda na kuendesha pikipiki kubeba abiria pesa wanayotengeneza ilikua ndefu sana toka hapo nilivogeuka nikasema sitoforce tena kujilipua nikaanza kutumia akili zangu na tafiti japo game zito lakini tutafika tu,
 
Hahaha,aise kweli god is good

Ova
 
Kuwa salama au kutokua salama kunategemea na mazingira ya shughuli zako. Hao wote ni kazi chafu.

Mimi nina mbwa nilimpeleka huko namuita mbwa kwa sababu kafanikiwa na amepata uraia, na maisha yamenyooka, lakini mbwa yule kasahau fadhila.
Tenda wema, kisha nenda zako. Uwe na uhakika kwenye hili, kila wema, au ubaya atendao mtu hulipwa na Mungu sometimes inaweza isiwe kwako bali kwa uzao wako. Be grateful.
 
Zipo sura hata mtu ukiambiwa huyu anaishi nchi ya nje ya Tanzania ni vigumu kuamini huyu ilitegemewa umkute jela tena jela za bongo za wale walioshindikana


Kama huyu hapa hata mtaani kwangu ninakoishi huku Mbezi Makabe shamba sijawahi kukutana na sura kama hii for years labda sogea sogea Manzense au Kigogo ile ya Mburahati ya wakorofi ila nashangaa nasoma kaenda fia South Africa,how!?

Huko watu kama hawa zaidi ya kwenda kufanya uhalifu hakuna lingine.
 
Unaweza kulaumu lakini kihistoria Watu wengi wa mwanzo walioenda Nje hasa Afrika Kusini ni wale walikuwa na ujasiri na ambao wengi wao walikuwa hawana elimu. Wasomi (angalau kidato cha sita na kuendelea) walikuwa na uhakika wa kazi, uoga wa kusafiri kimagumashi na Nchi ilikuwa na utulivu wa kisiasa. Matokeo yake ni kuwa wengi wakaishia kufanya shughuli ndogondogo na hatimaye kuingia kwenye uhalifu.

Kwa wenzetu, kidogo hali ilikuwa tofauti. Kwa mfano Wakenya na Wanaijeria, wengi waliokuwa na shule ndiyo walienda South au ughaibuni. Matokeo yake elimu ikawasaidia kujiendeleza na kuingia kwenye shughuli nyingine rasmi, na hata kama ni wahalifu lakini walitumia akili nyingi na elimu iliwasaidia. Just imagine miaka ya mwanzo tisini Nigeria tayari kila jimbo kuna Chuo kikuu, Kenya tayari walikuwa na vyuo zaidi ya saba na likazaliwa tatizo la ajira kwa wasomi mapema zaidi wakati huku kwetu miaka hiyo elimu tu ya kidato cha sita unaringa hata kwenda jeshini na vyuo vikuu ni Sokoine na UD.
 
Acha kuogopesha wanaume.kufa kupo pale pale hata kama utajifungia ndani.Ata bongo hapa watu wanafanyiziana vile vile.Kikubwa naisha yaende haya mengine ni mapito tu.
 
Shukraani mkuu kwa kumsaidia mtanzania mwenzako, welldone ipo siku nawe utasaidiwa na ninaamini baharia huyu alikuombea sana mkuu, yes maisha hapa ni tough na hakuna opportunities za kugeuza maisha kama huna connections zozote, SA unaweza geuza maisha hata kama hujawa connected, we don't need kufagia watanzania wote kwa ufagio mmoja, wapo hapa nchini wapopo kibao wanauza drugs na wanaishi better life kuliko wazawa ila hatuwahukumu wapopo wote kuwa wanafanya drugs peddling, baharia kama unataka kwenda kiwanja nenda, maisha popote pale
 
Ulitaka fadhila gani? Ulishakamilisha part yako, tulia.
Tulia wewe msukuma kuna kukwama nani kakuambia mimi sikuwahi kukwama nikamuomba msaada. Sijamaanisha anilipe, kuna kukwama unamuomba mtu msaada ukitegemea anaweza kukusaidia maadam ni jamaa yako na umewahi kumsaidia.
Give without remembering and receive without forgetting.
 
Uthubutu...sasa watoto wa siku hizi wanaweza nini zaidi ya kulialia
Na mwishow kujingiza kwenye mambo ya ajabu kama ushoga nk

Ova
 
hata hapa tanzania wapo watanzia wanauwawa. Kufa ni mambo ya kawaida. Hawa wengi wanaenda huko sauzi kujihusisha na uhalifu, wanatuletea aibu kama taifa acha wote wauwawe ili aibu ya nchi iondoke. Pumbafu sana
 

Kiwanja nishatimba sana root za kiwanja lusaka kupeleka magodoro, kiwanja malawi nilifanya sana. Nimegonga sana kwa kaburu sema mkaratasi full nilikua naingia na kutoka kihalali, maisha popote najua na baharia hakati tamaa laini akili kichwani
 
Uthubutu...sasa watoto wa siku hizi wanaweza nini zaidi ya kulialia
Na mwishow kujingiza kwenye mambo ya ajabu kama ushoga nk

Ova

Watoto walaini sana siku hizi wanagawa ubingwa kiboya wakati zamani mtu anasuffer south akidadindia ikikubalika baharia taarifa mtasikia barcelona, antwep, roterdam, hamburg, au port of valencia, wahuni waliweza kuvizia mingo hadi suez canal na walikua na akili sio maboya, respect kwa mabaharia wa kale,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…