Afrika Kusini sio salama, kuna Watanzania wameuawa siku za karibuni

Luck dube alikuwa mtanzania? Kifupi hiyo nchi imesha fall,hakuna mtu duniani asiyeijua south africa kwa roho mbaya zao,wana roho mbaya kwanza wao kwa wao,polisi na wao,harafu wao na wenyeji wao
 
Huyu nae kapigwa risasi wizini 70% ya watanzani waishi Durban ni wezi wa kuvunja majumba.
 
Yaani kuuliwa hao watatu ndio useme SA sio salama?mbona bongo watu wanauliwa Kila leo,na nchi ipo salama,
 
Hili nakupinga!!!Watu wengi tu wameondoka miaka ya 90 na degree zao kukimbilia mamtoni na wapo wamesettle wanamiliki mijengo na familia zao na maisha mazuri tu. Usichukulie hao wachache unaowafahamu wewe ukawajumlisha na wengine. Kuanzia 1995 wabongo wengi sana walitimkia ughaibuni na South Afrika walikua wasomi walioona nchi inakokwenda sio na wapo wengine ndio hao unaowasema. wakenya na wanigeria ni wengi kwa vile walianza kusafiri kitambo sana na wala sio kwamba wapo smart kuzidi wabongo.Kwavile walisafiri kitambo waliingia kwenye system kwahio huo ujanja ni vile wanafinywa masikio na waliotangulia lakini wabongo wachache kwenye system kutokana na kuanza kuingia huko juzi juzi tu 1990s..
 
Mbona ni kama wote walienda kufanya kazi nyeusi?
 
Binafsi siwezi kuwanyoshea kidole moja kwa moja wasouth.

Sijajua vijana walikuwa wakijihusisha na kipi kule.
Sidhani kama kunawasouth walikuwa wanatembea na bunduki wanauliza wewe ni mtanzania?, then wanapiga shaba. Kule mbona kunawatz wengi tu?

Kama wameuawa kwa ukatili wa wasouth, baasi Mungu awalaze mahali pema..

kama wameuawa kwa kujihusisha na mambo mabaya, Mungu awasamehe makosa yao pia na awahurumie na azitie nguvu familia zao.
 
Mkuu huyu jamaa naweza kuwa namfaham au lah, maybe nijue ulimtoa eneo gani coz kuna kiumbe mmoja alitokea ktk kijiwe changu cha kazi hapo Dar miaka ya 97 but alichukuliwa kuelekea huko until now nasikia familia yake inakula matunda fresh!.
Hapana huyu sie. Huyu kaondoka 2007.
 
Sawa na wasomi madaktari na walimu miaka ile waganda na wakenya wanachangamka na Botswana wanalipwa mapesa mengi sisi tumelala, tunakuja kustuka michongo ilishaisha tu wachache ndio walifaidika wengi walikalia uoga uoga wa bila sababu
Wabongo wengi ni wazito waoga kutoka nje
Ila kwa walimu,madokta waliyoenda Botswana mpk sahv hawajutii kuondoka

Ova
 
Yote maisha tu

Wabongo wamezagaa duniani kote

Ova
 
hajari kazini kwani tz hawafi?
 
Niko group moja la mabaharia South Africa, kila baada ya siku mbili Kuna post ya rambirambi, mara mwamba kauawawa na Wazulu, mara polisi mara wenyewe kwa wenyewe, sio poa aisee.

Noma Sana, pande hizo sio kwa wake wenye mioyo mwepesi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…