Afukuzwa kazi ya Umeneja TRC kwa kumkosoa Rais Samia kuhusu tozo kwenye miamala ya simu na kukusanya mapato

Ukiona wanajilinda sana..ujue wanawaibia.

Hatuna viongozi tuna majambazi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Jamani naomba muwe wavumilivu wakati natafuta mawasiliano na PUTIN aje kuifanyia jambo maalum hii serikali.....
 
Naona hamna tofauti kati ya awamu ya 5/6 Wembe unakata lakini kimyakimya.
 
Baraka Shamte ametumia zaidi ya nusu ya maisha yake kutukana wapinzani.
Alipojisahau akakosoa watawala kachukuliwa nyumbani kwake na aliporudi akasimilia kipigo alichopewa. Sasa hivi hata kutoka nyumbani ni kwa safari za lazima tu kama za hospitali.
 
Huyo mtumishi akate rufaa haraka sana kisha atafute wakili kinara kama kibatala, hiyo kesi itwadhalilisha sana washitaki.
Hakuna tusi lolote lililotajwa kwenye mashitaka na pia chanjo ni hiari ambapo anayehamasisha na anayepinga wote wako sawa hovyo hakuna kosa lolote lililotendwa.

La mwisho kama mtumishi kafukuzwa kutokana na makosa dhaifu kama haya basi serikali tayri imeshafeli pakubwa kwa mambo yake muda utaongea
 
Kuna maamuzi ya kisasa na kisheria sana sana atamchelewesha ila atapata haki yake
Haki inapatikana japo kwa umbali, mahakamani. Sasa serikali ishapiga marufuku watumishi wa umma kwenda mahakamani, akienda ni kwa review kupinga maamuzi ya rais na sio maamuzi ya mamlaka ya nidhamu, sasa hapo kuna kutoboa kweli?
 
Tanzania hatuna tofauti na nchi kama North Korea, Russia, Cuba na China. Bado tuko kule kule kwenye zama. Naona itakuwa ngumu sana kutoka huko mpaka pale CCM itakapotoka madarakani!
Ukosefu wa heshima kwa mkuu wako wa kazi (insubordination) lazima uliwe kichwa.
 
Hii itakuwa kesi ya kihistoria kuondokana na huo ukale.
Asante sana wakili PETER KIBATALA kujitolea msaada wa kisheria bure.View attachment 2331593
Anaweza kuwa anapoteza muda huyo aliyefukuzwa kazi. Huwezi kuidharau ofisi za rais kwa maana ya cheo chake halafu uendelee kuwa mtumishi wa serikali unaopokea mshahara wa serikali.

Uhuru wa kidemokrasia una mipaka yake.
 
Asikosolewe yeye ni Mungu, uhuru wa fikra ulindwe. Hao mabosi ni kujipendekeza tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…