Afukuzwa kazi ya Umeneja TRC kwa kumkosoa Rais Samia kuhusu tozo kwenye miamala ya simu na kukusanya mapato

Afukuzwa kazi ya Umeneja TRC kwa kumkosoa Rais Samia kuhusu tozo kwenye miamala ya simu na kukusanya mapato

Anashinda mapema kivipi wakati ameelekezwa kukata rufaa tume ya utumishi wa umma ambako nako licha ya rufaa kusikilizwa baada ya miaka 3 toka kuwasilishwa, watasema rufaa yake haina mashiko na kisha watamwelekeza akate rufaa kwa Rais wa JMT, huko maamuzi yake ushajua yatakuaje. Usisahau kuwa Rais anaweza kutoa maamuzi ya rufaa hiyo hata baada ya miaka 4...umapema unatoka wapi happ mkuu?
Kuna maamuzi ya kisasa na kisheria sana sana atamchelewesha ila atapata haki yake
 
Wewe unaishia Dunia gani? Unakumbuka kilichomfukuzisha Mafuru pale hazina? Alialikwa clouds 360, akahojiwa kuhusu malalamiko ya wananchi kwamba vyuma vimekaza! Akatoa sababu za kiuchumi ikiwa ni pamoja na serikali kubana matumizi, serikali kufanya miradi mikubwa inayochukua pesa nyingi Kwa pamoja hivyo pesa nyingi kwenda huko na hivyo kupunguza mzunguko wa ndani!

Baada ya hapo, alikutana na barua ya kutumbuliwa ofisini!
Ni Mafuru pekeake ndio alitumbuliwa wakati huo?

Tuoneshe barua ya kutumbuliwa kwake na sababu za kutumbuliwa kwake.
 
Kihallisia Hilo suala sidhani hata kama Rais analijua. Kuna michawa fulani katika harakati za kujipendekeza ndio Huwa inachonga mashtaka kama hayo ila nakuhakikishia hakuna mkono wa Rais hapo.
Ni maagizo toka juu. Hawa watendaji wa chini huwa wanacheza ngoma ya mkubwa
 
Mambo ya kustaajabisha sana haya, bora siko huko serikalini maana wangenifukuza mapema sana sababu huwa siwezi unafiki.
Sasa mkiona watu wamenyamaza au kusapoti kila kitu muwaelewe. Huyu ana bahati kufukuzwa kazi. Yaani kufukuzwa kazi ashukuru Mungu.
 
Kihallisia Hilo suala sidhani hata kama Rais analijua. Kuna michawa fulani katika harakati za kujipendekeza ndio Huwa inachonga mashtaka kama hayo ila nakuhakikishia hakuna mkono wa Rais hapo.
Mjulisheni atengue hio hukumu.
 
Trailer la JOB NDUGAI halikueleweka,mapicha yenyewe yanakuja

jitieni mnajua sana toa mawazo yenu wakati mnaemwita mpole anawaskia

vikauli vyake vyepesi sana ila (vina command ndani yake) "na hili nalo mkalishughulikie"

kwa sauti nyororoooo,sasa wewe fkiria ile sauti ndio na moyo uko hivyo hivyo,ki ufupi

nasema tutakaa miaka 100 kuja mpata JPM mwingine,muogope sana mtu mnafki

anaekuchekea usoni ila moyoni ana yake,JPM alikua hana unafki anakupa hapo kwa hapo

akifurahi unajua akikasirika wote tunajua,OGOPA sana hawa viumbe wanaojitia wao HASIRA kwao ni JINAI hawakasiriki hadharani,wanakasirikia mafichoni effect wanazipata wahusika.

Hii nchi kama unajua kula yako inaitegemea serikali,Unga zako tu juhudi maisha yako na wanao na familia yakuendeee,acha mawazo ya kitundu lissu,mawazo ya ki pinzani pinzani.

Baki na mawazo yako moyoni kwa usalama wa familia na maisha yako kwa ujumla,tupo ktk uongozi ambao bila kuwa Mnafki hutoboi, Viongozi wa juu wote ni wanafki.

na huu unafki wao mtaujua MAMA akitoka madarakani,namna watavyoungana na wanaomponda bi tukinao.

Unafki sinaga na hivi sitegemei mafao yao wala v8 zao hazinihusu ntasema wazi siku zote Nchi hiii Rais alikua JPM tu wengine wote walikua Full Unaaaa + Aliepo wote ni wanaaa...
 
Mambo ya kustaajabisha sana haya, bora siko huko serikalini maana wangenifukuza mapema sana sababu huwa siwezi unafiki.
Wanasema hata jamaa wa bandari, kamwagwa kwasababu ya kutokukubaliana na mauza uza ya mkataba wa wavaa kobasi na jamhuri, kaona liwalo na liwe, bora kutemeshwa mzigo kuliko kushiriki ulambaji asali ule!
 
Inakiwa ieleweke kwamba tuna UHURU wa kusifia na sio UHURU wa kukosoa, hili suala lipo wazi.
 
Uonevu tu, kasema ukweli kwamba TOZO ni kero tena kero kubwa mno. Yaani mshahara wangu mnakata PAYEE afu bado tu mnaufuatilia hadi BENKI nako mnataka TOZO kila napotoa...

Haya isitoshe nakwenda kununua vitu madukani bado nako mnataka tena VAT 18% ; Jamani mbona mnatuonea sana sisi wafanyakazi?

Yaani kazi nifanye mie afu tugawane pasu kwa pasu - hii si HAKI.

CCM mbona mnatufanya hivi lakini ?
 
Back
Top Bottom