Afukuzwa kazi ya Umeneja TRC kwa kumkosoa Rais Samia kuhusu tozo kwenye miamala ya simu na kukusanya mapato

Afukuzwa kazi ya Umeneja TRC kwa kumkosoa Rais Samia kuhusu tozo kwenye miamala ya simu na kukusanya mapato

Upo serikalini Tena kwenye nafasi ya uteuzi,unapopinga Yale yanayosimamiwa kupitia sera na miongozo ya serikali,huo ni utovu wa nidhamu,kama hukubaliani nao,Kaa kimya,toa maoni jinsi ya kuboresha lakini sio kukosoa kwa kuonyesha jinsi viongozi wako wa juu wanavyokosea,uwezi kumkosoa boss wako harafu akuache tu,hii ni logic simple kabisa.

Viongozi wa kisiasa wanapo amua mwelekeo wa jambo fulani kupitia sera,sheria miongozo au maagizo,mtumishi wa umma ni kutekeleza tu,huwezi kutumia nafasi hiyo kupinga,na kuleta upinzani,hii sio Sawa,lazima utekeleze Yale wakubwa wa kisiasa wanataka serikali ifanye kwa niaba ya wananchi,sio jukumu lako kusema hiki hakifai!wewe hujachaguliwa na wananchi,waliochaguliwa ndio Wana haki na uwezo wa kutenda kwa niaba ya wananchi.

Sasa fikiria Dakitari wa hospitari ya umma,wakati waziri na nchi wanahamasisha chanjo ya COVID,yeye apite kimya kimya chini chini anawashawishi watu wasipime kwa vile ina madhara!!sasa serikali haiwezi kufanya kazi na mtu asiyekwenda na miongozo inayoitoa,lazima upigwe chini.
Well said!
 
Hata kama kulikuwa na kumdhalilisha Rais, mwajiri hana mamlaka ya kumfukuza mfanyakazi kwa kosa hilo kwa kuwa halihusiani na kazi ya mwajiriwa. Sana sana Serikali inaweza kumshitaki mtuhumiwa chini ya vipengee vingine vya sheria na akaadhibiwa kwa kutozwa faini au kufungwa lakini si kwa kufukuzwa kazi kwa kuwa kosa halihusiani na utendaji wa kazi.
Amefukuzwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma. Barua imequote na vifungu vya Sheria na Kanuni. Nawe lete vifungu, otherwise utakuwa huna jipya.
 
Kumkosoa muheshimiwa raisi kistaha siyo kosa!Ila nadhani meneja alitukana viongozi matusi mazito ya nguoni tena bila staha,Mama ameamua kumparura[emoji51]

Kwa jicho la mbali naona hata akikata rufaa hashindi.
Hawezi kushinda huyo, kakashifu maelekezo ya viongozi wakati anatakiwa kuwa mtekelezaji wa maelekezo hayo ni insurbodination. Tozo zishapitishwa na bunge na sheria imesainiwa, wewe mtumishi wa umma unapinga tena kwenye public.... Kufukuzwa ni obvious. Isitoshe kafukuzwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi wa umma ambazo kila mtumishi lazima aziishi na kuzitii
 
Kumkosoa muheshimiwa raisi kistaha siyo kosa!Ila nadhani meneja alitukana viongozi matusi mazito ya nguoni tena bila staha,Mama ameamua kumparura😬

Kwa jicho la mbali naona hata akikata rufaa hashindi.
Una uhakika na unayosema?
 
Hawezi kushinda huyo, kakashifu maelekezo ya viongozi wakati anatakiwa kuwa mtekelezaji wa maelekezo hayo ni insurbodination. Tozo zishapitishwa na bunge na sheria imesainiwa, wewe mtumishi wa umma unapinga tena kwenye public.... Kufukuzwa ni obvious
Sheria sio porojo za Yanga na Simba.
 
Upo serikalini Tena kwenye nafasi ya uteuzi,unapopinga Yale yanayosimamiwa kupitia sera na miongozo ya serikali,huo ni utovu wa nidhamu,kama hukubaliani nao,Kaa kimya,toa maoni jinsi ya kuboresha lakini sio kukosoa kwa kuonyesha jinsi viongozi wako wa juu wanavyokosea,uwezi kumkosoa boss wako harafu akuache tu,hii ni logic simple kabisa.

Viongozi wa kisiasa wanapo amua mwelekeo wa jambo fulani kupitia sera,sheria miongozo au maagizo,mtumishi wa umma ni kutekeleza tu,huwezi kutumia nafasi hiyo kupinga,na kuleta upinzani,hii sio Sawa,lazima utekeleze Yale wakubwa wa kisiasa wanataka serikali ifanye kwa niaba ya wananchi,sio jukumu lako kusema hiki hakifai!wewe hujachaguliwa na wananchi,waliochaguliwa ndio Wana haki na uwezo wa kutenda kwa niaba ya wananchi.

Sasa fikiria Dakitari wa hospitari ya umma,wakati waziri na nchi wanahamasisha chanjo ya COVID,yeye apite kimya kimya chini chini anawashawishi watu wasipime kwa vile ina madhara!!sasa serikali haiwezi kufanya kazi na mtu asiyekwenda na miongozo inayoitoa,lazima upigwe chini.
Fact
 
Hii ni hatari sana. Ina maana kutoa maoni ni kosa? Inara ya 18 ya katiba JMT inasema vipi?

TAMKO LA TRC
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk alipoulizwa kuhusu suala hilo amesema: “Kwa sasa sijapata taarifa rasmi ya suala hilo, nalifanyia kazi kisha nitatoa taarifa rasmi,” - Jamila
Mtumishi wa umma jifunze kuishi kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi. Ni ajabu mtu ushafikia umeneja halafu unafanya mambo ya namna hii. Pia hata ku upload hiyo barua hapa itakubania riziki zako siku za usoni ndugu yangu
 
Watumishi wa Umma wengine ni kichefu chefu sana, unakuta mtu yuko ofisini kazi kukaa mitandao ya jamii kutwa hafanyi kazi, na huko mitandoni kutukana na kukashifu serikali ya CCM kwa kila namna, Mtumishi wa hivyo ni hasara sana kwani productivity ni zero, in a week unakuta kafanya kazi say 10% tu, kazi mitandao tu, acha ajifunze hana adabu kama Manara.
Na sisi tunaotumia 70% ya muda wetu makazini kuisifia CCM tunawekwa kundi gani?
 
Hii ni hatari sana. Ina maana kutoa maoni ni kosa? Inara ya 18 ya katiba JMT inasema vipi?

TAMKO LA TRC
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk alipoulizwa kuhusu suala hilo amesema: “Kwa sasa sijapata taarifa rasmi ya suala hilo, nalifanyia kazi kisha nitatoa taarifa rasmi,” - Jamila
Mtakapo ingiza siasa ktk kazi nakufikiri watu watatishika nikweli watatishika ila je kesho ya hili Taifa itakuwaje kumbukeni yalio tokea Libya nchi iliyokuwa imepandikiza makachero kila kona ila nyuma ya pazia walikuwa wakitemgeneza. Uwasi mbaya ulio pelekea taifa kuanguka. Kweli amekosea ila je alisema kwa nia gani nje ya kazi ni Raia nje ya kazi ni mpiga kura nje ya kazi ni mtanzania wakawaida kama wengine kosa lake ni kutokubaliana na kile serikali wanakifanya well ni haki yake ya msingi kwani hili ni taifa la kindemokrasia na kama hakuna hiyo democrasia ondoeni vyama vingi ondoen mambo yakupiga kura maana tuta umizana bure pasipo sababu.
 
hatari sana hii tunaelekea wapi wapi Tanzania, akikomaa na kupata mwanasheria mzuri anaweza kuchomoka
Sio kuchomoka tuu bali kufanya mfumo wetu wa utawala udhalilike kabisa.
Niwaombe taasisi za kiharakati za kupigania demokrasia kulivalia njuga suala hili ambalo limejulikana wazi.
Ni dalili kuwa wengi wanakumbana na Masahibu ya aina hii na tunaporeza wataalamu wetu kwa kuwalinda wanasiasa majambazi wasikosolewe.
 
Huu upumbavu wa kadogosa unaukuta tanzania, nchi kama Kenya zenye independent judicial system huwezi kuta mtu anaandikiwa barua za kipumbavu kama hii
 
Mambo mengine usije kuta Ni walamba viatu wa mama.
Mama mwenyewe hata habari hana
 
Kwa ufupi ni kwamba ukiajiriwa na serikali hutakiwi kupinga anachosema Boss wako
 
Back
Top Bottom