Afungwa jela kwa kosa la kumlawiti mkewe kama adhabu anapokosea

Afungwa jela kwa kosa la kumlawiti mkewe kama adhabu anapokosea

Pamoja na adhabu iliyotolewa, nadhani kulikuwa na haja Mahakama ikajiridhisha zaidi Kwa kupata ripoti ya Daktari.

Lakini pia, isije kuwa hii ni mbinu inayotumika kutuumiza Wanaume.

Unaweza ukawa unapewa hayo mambo kama sehemu ya Starehe na mapenzi yenu na Mkeo alafu baadaye akaja kuitumia kukufunga jela.

Mtafanya Wanaume tuombe talaka Kwa Wake zetu sasa kuogopa hayo yasije kutokea.

Mungu atunusuru Wanandoa, naona Taasisi ya Ndoa inaendelea kupigwa Vita Kila Leo 😭
Ndoa siku hizi ni msala ujao
 
Nikikuta umechelewa kupika kifiro
Nikikuta unachat na wanaume wengine kifiro
Nikiacha hela ya nyama nikakuta maharagwe kifiro.
Ukichelewa kujib txt kifiro
Daaaaah!!! Kwa hawa dada zetu wa mjini, atajitahidi kila siku akoseee
Dah
 
Kwa matukio kama haya watu wa 'Kataa Ndoa' wanaeleweka vuzuri sana akilini mwa watu.
Ni mambo ya ajabu kabisa

Wanataka kuidhohofisha Taasisi ya Ndoa kabisa

We unadhani hayo mambo hayafanyiki kwenye Ndoa, vipi Kila Mwanamke akienda kuripoti Polisi, si almost Wanaume wengi watafungwa

Hawa watu ni hovyo kabisa
 
Mahakama ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa imemtia hatiani Dickson Mbwilo (42), mkazi wa Kitelewasi na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumlawiti mke wake.

Kulingana na maelezo ya mwanamke huyo mwenye umri wa miaka (32), mumewe alikuwa akimfanyia kitendo hicho pale anapokuwa amekosea ili iwe ndiyo adhabu yake hali ambayo ilimsababishia sehemu zake za siri kuharibika vibaya.

Hata hivyo, mpaka kufikia hatua ya Mbwilo kutiwa hatiani na kufungwa, mlalamikaji hakuwahi kufika kortini kutoa ushahidi wake, isipokuwa Mahakama iliamua kuegemea maelezo yake aliyokuwa ameyaandika Polisi.

Hukumu hiyo ilitolewa Machi 6, 2024 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, Benedict Nkomola na nakala yake kupatikana Machi 12, ikisema ushahidi uliotolewa umethibitisha mashtaka dhidi ya Mbwilo.

Hakimu amesema katika kesi ya jinai, maelezo ya malalamikaji yanaweza yakatumika kama sehemu ya ushahidi kwa kuwa sheria ya ushahidi inatoa utaratibu wa kushughulika na kesi ambazo mlalamikaji atakuwa hapatikani kutoa ushahidi.
Sio zanzibar hii, lkn basi
 
Kuna njemba ya Lugarawa huko Njombe Ludewa, yeye alimfumua rinda mke wake kwa kosa la kuchelewa kurudi kutoka kwenye harusi kama sikorei.
Uzi uko hapahapa JF.
Hao sio wakinga ni wahamiaji
 
Back
Top Bottom