Agenda ya Mohamed Said ina ukakasi

Nakubaliana nawe. Huyu mzee huwa ananuka udini. Ni mtumwa wa kiarabu wa kujitakia. Kila akiongea au kuandika, unaona sumu na udini visivyo mithalika
Father...
Ukinitambulisha kwa maneno ya, "Huyu mzee..."

Tayari najua kuwa umeghadhibika.

Hakika mimi ni mtumwa lakini si wa Kiarabu ukisema hivyo ni kunipa mimi kabila isiyo yangu.

Najua ulikusudia kuniita mimi mtumwa wa Waarabu.
Mimi ni mtumwa na najifaharisha kwa kuwa mtumwa.

Mimi ni mtumwa wa Yule Aliyeumba Mbingu na Ardhi.
Allah.

Siwezi kujinasibisha na Mwenyezi Mungu kisha kauli yangu ikawa sumu.

Ningekuwa natema sumu nisingekuwa ndani ya kitabu cha maisha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kilichoandikwa na Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Othman na Dr. Ngwazi Kamatha.

Wala nisingekuwa ndani ya Dictionary of African Biography.
Wala Cambridge Journal of African History.

Wala sijaandika udini wowote mahali popote.

Nilichoueleza ulimwengu wa wasomi ni kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika imefuta sehemu kubwa sana ya ukweli kwa kukwepa wazalendo walioupigania uhuru wa Tanganyika.

Wengi wa wazalendo hawa ni Waislam.
Nimeandika historia zao kwa kirefu.

Julius Nyerere hakuwa peke yake.
Kwa nini walifanya khiyana hii ni hofu tu ambayo haikuwa na sababu.

Nimeiandika historia ya kweli kitabu kina uhai wa robo karne kimepigwa chapa mara nne na nchi ni shwari.

Kitabu changu hakijasababisha machafuko yoyote.
 
hoja yako haina ithibati yoyote zaidi ya wivu,kwakuwa anachofanya mohamed said ni kuweka historia vizuri au sawasawa
 
Mwanangu Mohamed, hujambo? Samahani sana kwa kukutoa usingizini. Nilikusudia japo nikuchokoze ujieleze zaidi kama siyo kujitetea. Kwanini unapenda kuwaita watanzania waislam kwanza badala ya watanzania? Hebu fanya utafiti kidogo. Najua unajua kufanya utafiti. Angalia waarabu wanavyojiita. Huanza na uarabu ndiposa huja huo uislam wako. Huwa sina ugomvi na mawazo wal mlengo wako. Badala yake huwa nahangaishwa na namna unavyowaweka waswahili kwenye uislam kabla ya utanzania wao. Hebu angalia jamahiriya za wale wanaojiita waarabu ingawa wako Afrika. Ni Arab Republic of Egyt, United Arab Emirates, et cetera ingawa wako Afrika. Kwanini hawasemi Islamic republic yada yada? Utumwa ni jambo baya japo linapokuja kwenye kile unachokiamini hata kama ni cha hovyo kama wahindu waaminivyo vinyago nawe Allah, inatia shaka. Allah si Mungu wa wamanyema. Ni Mungu wa kuletwa tu. Nakubaliana nawe unavyopigana kuibua yale yaliyofichwa. Hata hivyo, kwa msomi aliyeiva huwa anajitahidi kuepuka kuelemea upande fulani. Na kama ikitokea akataka kufanya hivyo, huwaelezea wasomaji wake udhaifu au bias yake au zake. Wewe hufanyi hivyo na bado unataka uonekana uko impartial.
Huo ndiyo ugomvi wangu nawe mwanangu wa mitaa ya kwetu ya Kipata na Mchafukoge kwa akina Litela, Nyangwele na wengine toka Rufiji na umanyemani.
 
Ni babu tapeli wa kihistoria anachanganya uongo na ukweli ili kupotosha kwa msingi wa udini, mi huwa namwona mhalifu siku nyingi!
Ni moja ya watu wanaogawa Watanzania wasiishi kwa kujiona wamoja!
 
Father...
Kwa nini hujajiuliza ni nini kilisababisha kuandikwa kwa historia ya uongo?
 
Ni babu tapeli wa kihistoria anachanganya uongo na ukweli ili kupotosha kwa msingi wa udini, mi huwa namwona mhalifu siku nyingi!
Ni moja ya watu wanaogawa Watanzania wasiishi kwa kujiona wamoja!
Mzizi...
Nitashukuru ikiwa utaweka hapa uongo wangu.

Unadhani kwa kuifuta historia ya kweli na kupachika kitu kingine ndiyo kutajenga umoja?

Umoja unaletwa na haki na usawa kwa raia wote.
Umepata kujiuliza hili?
 
Huyu mzee mimi nilisha m flash. Ni mzee mmoja hivi mpuuzi sana. Ana chuki na wakristo na anaumia zaid pale ambapo ile chuki kwa wakristo haibadilishi chochote kwa hyo moyoni mwake kunawaka moto. Anatamani ajilipue 🤣
Tash...
Ukianza na huyu mzee najua umeghadhibika.
Hii ndiyo sababu unatukana.

Mimi si ''mpuuzi.''
Mimi sina chuki na yeyote.

Wala moyo wangu hauwaki moto.
Moto unawaka ndani ya nafsi yako wewe.

Ushahidi ndiyo huu: ''Huyu mzee,'' na kutukana, ''Mpuuzi,'' ''Flash.''
Haya si maneno ya adabu kumwambia mtu ambae unajua ni mzee.

Ningekuwa mpuuzi watu wasingejaa kwenye nyuzi zangu kunisoma na kujadiliana na mimi.

Tukiwaita watu watuhukumu si mimi nitakaevishwa kofia ya mpuuzi.
 
Umelalamika sana lakini hujaeleza kwanini afungiwe au afungwe.
 
Massa,
Huo si uwanja wangu mimi nimesahihisha historia iliyokuwa imeandikwa sivyo.
Nilulize kuhusu hilo.

Sawa mzee mohamed acha tuendelee kusubilishia hadi miujiza itakapotokea. Uje ata viongozi wa juu mnawapa wakati mgumu sana maana hawajui wafanye nini kuondoa hilo tatizo. Mwisho wa siku wajukuu wa waislam watafundishwa kuhusu matatizo ya waislam tanganyika alafu watawachukia wajukuu wa wagalatia. Muna muda wa kutoa ushauri kufanyike marekebisho lakini hamtaki. Mtu Kama unaona kuna shida unasema na unashauri nini cha kufanya huo ndo uungwana. Au waandishi wa history hamuluhusiwi kushauri?
 
Massa,
Msome John Sivalon (1992), Bergen (1981) na Njozi (2002).
 
Duh,
Yaani unaamini kila mtu anakujua?!!

Inawezekana una mashabiki na wafuasi wengi, lakini wanaweza kuwa wa mrengo fulani tu hasa wa kidini, siyo watu wate.
Tupo tusiokujua kabisa
Anti...
Lakini mimi si mtu wa dini ingawa ni Muislam.

Eneo langu ni katika ''Scholarship,'' yaani elimu.

Kusoma, kusomesha na kuandika.

Haya si maeneo ya ''washabiki,'' na ''wafuasi.''

Hao utawapata kwengine.

Haya yangu ni maeneo ya elimu na utafiti.

Nitafute katika Cambridge Journal of African History (1998).

Nitafute katika Dictionary of African Biography (2011)
Nitafute katika Nyerere Biography (2020)

Je umeona dini hapo?

Kulikuwa na mjadala hapa JF uliodumu kwa miezi 6 nikisomesha historia hii.

Mjadala ulipitiwa na watu karibu milioni moja.

Haijapata kutokea.
Wewe ulikuwa wapi?

Anti...
Hakika wako wengi wasionijua ikiwa si wanachama wa ''clubs'' mfano wa hizo hapo juu na hapo chini lakini nafahamika hapa Dar es Salaam kwa kuwa ndiyo kwetu na kwa mengine mengi.

Ningependa kukufahamu.
Nani mwenzangu?

Mitaa niliyopata kuishi mimi inajieleza yenyewe:

The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.

The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006

Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.

Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.

Uamuzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.

Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam.

Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam

Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigani Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam

Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam

Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam

The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam

Rajabu Ibrahim Kirama, Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam, Readit, 2020, Dar es Salaam

Sal Davis An Autobiography, Readit 2023

In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).

Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).

Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)

The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).

Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).

The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).

Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).

Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).

Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).

Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).

Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.

Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.

Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.

Awards: Several Awards

Visiting Scholar: (2011)

University of Iowa, Iowa City, USA

Northwestern University, Chicago, Illinois, USA

Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.

OTHER COUNTRIES VISITED

Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.


 
Pole sana mzee wangu .
Allah aendelee kukupa wepesi , nilijitaahid sana kukufuatilia sana kwenye kipindi pendwa pale UTV ila sikupata kuyasikia haya ndiyo maana nimehamaki kuyasikia .

Ila pole sana Allah aendelee kukuruzuku.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Kupenda kutiliana fitna ndio maana waafrika hatuendelei.Mpaka mtu akiwa na wazo anaogopa kuliweka hadharani kuogopa fitna.Halafu tunalalamika eti waafrika hatuna akili kumbe fitna na uchoyo ndivyo vinaturudisha nyuma.Hatufaidiki na wasomi wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…