Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Friends, ladies and gentlemen.
Je ni kweli kwamba umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu?
Inaonekana kwenye siasa za Tanzania hasa upinzani, chuki binafsi, migawanyiko, uhasama na utengano miongoni mwa vyama vya siasa eti ndiyo huleta nguvu na ndiyo kipaumbele chao kwa sasa.
Kitendo cha Mwenyekiti wa wa chadema taifa, Freeman Aikaeli Mbowe kuonyesha chuki dhidi ya alivyoviita vyama 14 vya siasa vya upinzani, na kujaribu kuvikaripia kwa ukali na pengine kuvielekeza kufikiri kama inavyofikiri chadema, kinaashiria udikteta wa wazi kabisaa.
Je,
huku sio kuingilia uhuru, haki, uelekeo na mipango mikakakati ya vyama vingine vya siasa kadiri wanavyoona inafaa?
huu ni wivu tu au ndiyo udikteta unajipambanua mapeeeemaaaa ili iwe rahisi kwa uma kuudhibiti vizuri kwenye sanduku la kura?
Ni dhahiri chadema haina ushawishi ndani ya chadema yenyewe, haina ushawishi katika upinzani kwa ujumla, na zaidi sana haiaminiki wala haina ushawishi kwa raia na wapiga kura tena. Imebaki na press conference, matamko na kushinikiza tu vyama vingine vya siasa vifanye nini.
Yaani vyama vya upinzani badala ya kushawishiana kwa hoja, kushauriana kama ndungu na kuhubiri umoja miongoni mwa upinzani, eti Freeman Aikaeli Mbowe anahubiri, anachochea na kuhamasisha chuki na utengano miongoni mwa vyama vya siasa. Kweli upinzani, hasa chadema una nia njema na taifa hili ndrugo zangu?
Ni wazi chadema katika ujumla wake, haina dhamira ya kufanya siasa safi, wala haina mipango ya kushinda uchaguzi, ima kushika dola, kuunda serikali, kuongoza nchi wala kuwatumikia wananchi,
Bali chadema ina lenga kuchochea chuki, uhasama na kuligawa taifa katika misingi ya vyama miongoni mwa wananchi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini na kuingilia uhuru na haki za vyama vingine vya siasa hasa upinzani, visifanye kazi na majukumu yao kwa uhuru kadiri ya malengo na mitazamo yao, bali vifanye siasa kadiri chadema inavyotaka.
Migawanyiko, chuki na uhasama ndani ya chadema, sasa inachochewa na chadema yenyewe hadi katika vyama vingine vya siasa vya upinzani nje ya chadema. Ni dhahiri kuna tatizo chadema.
Unadhani Chadema ina feli wapi hata kufikia hatua ya kuingilia uhuru na haki za vyama vingine vya upinzani nchini, na asasi za kiraia zenye mipango, malengo na maono yao?🐒
Mungu Ibariki Tanzania