Air Tanzania, Soko la Afrika Kusini, Abiria ni wengi ajabu!

Acha kuogopa ushindani,boresha huduma zako,huwezi fanya biashara peke yako
Unahisi hiyo biashara ni kama kuuza nyanya sokoni kwa kuwa Mudi anauza na wewe unaweka meza ili kuuza.

Hujiulizi kwa nini sio kila nchi ina shirika imara la ndege?

Umewahi hata kujiuliza Modal wanayotumia mashirika kama Emirates na Qatar Airways....

Why Africa ni Ethiopian Airlines, Kenya Airways na Egypt Air....?
 
ATCL ikiamua kwenda hizo routes hawezi kosa wateja.

Kwanini uzunguke mpaka Bole wakati unapata direct flight toka Dar kwenda Cape Town/J'burg/Dubai?

Binafsi sioni mantiki upoteze muda utoke S.A uende Bole ndo uje TZ wakati unaweza chukua direct flight mpaka Dar.

Soko lipo ila akiamua kuwa serious.
 
Mwamba hapa umejua kudadavua.

Tatizo vijana hata wasio na ujuzi wa hii Sekta kwa kuwa wana akaunti Jf wanahisi wanaweza kuchangia chochote.

Wanahisi unaamua tu asubuhi upige route ya Johannesburg au Cairo [emoji2][emoji2][emoji2].

Mtu anajenga hoja kwa mahojiano ya Youtube[emoji54][emoji54].

Ushawahi ona Ethiopian Airlines mkurugenzi wake anaeleza mpango kazi YouTube [emoji38][emoji38]
 
Haya mambo makubwa huwa hayajadiliwi kwa video za YouTube.

ATCL haikuwa active kwa miaka mingi, huwezi kuingia na kushindana na hao, unatakiwa ianze taratibu kwa soko la ndani kwanza.

Biashara ya usafirishaji wa anga sio kama biashara ya Daladala Mbagala kwenda Kawe [emoji23][emoji23]
 
Jamaa anadhani abiria wa ndege wanapimwa kama wa dala dala la Mbagala mpaka Kawe!
 
Nunua hiace kashindanie soko na SHABIBY, Dar- Dodoma.

Unahisi hiyo biashara ni kama kuuza matikiti pale Stereo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hiace (Dar-DOM?)
 
Haya mashirika yote yalianzishwa pamoja!?..Kama laa..mbona waliofuatia hawakuogopa kuanzisha kwa kuwa Kuna mashirika yapo sokoni na biashara ni tricky!?
 
Hayo yamezungumzwa jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Dkt. Ally Possi, wakati akizungumza na menejimenti ya ATCL, na kusisisitiza kwamba pamoja na maboresho yanayofanyika kwa sasa Shirika linakamilisha mpango biashara wa muda mrefu ili kuhakikisha ATCL inajiendesha kwa faida pamoja na kulipa madeni yaliyopo.



“Serikali imeendelea kuwekeza kwenye Shirika hili na niwahakikishie maboresho ya viwanja vya ndege nchini yatachochea kwa kiasi kikubwa ongezeko la mapato na hatimaye madeni yanayoripotiwa yatalipwa", amesisitiza Dkt. Possi.



Aidha, Dkt Possi ameipongeza Menejimenti ya ATCL kwa kazi kubwa wanayoifanya na kuwataka kuhakikisha changamoto mbalimbali zinazokabili Shirika hilo ikiwemo mabadiliko ya ratiba yanaripotiwa mapema kwa abiria ili kuwafanya abiria kuendelea kuliamini na kutumia Shirika hiyo.



Naye Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Eng. Ladislaus Matindi, amemuhakikishia Naibu Katibu Mkuu huyo kuwa Shirika linaendelea kuboresha utendaji na huduma ili likue na kuendelea kuaminika kwa utoaji huduma bora kwa zaidi ya vituo 15 vya ndani ya nchi na zaidi ya vituo sita vya nje ya nchi inavyovihudumia.



Eng. Matindi ameongeza kuwa kwa mwaka huu Shirika linakamilisha mazungumzo na mashirika makubwa ya ndege kama KLM na Emirates ili kuboresha huduma pale itakapoanza safari zake kwa vituo vya Uingereza na maeneo mengine kimataifa.



“Tayari tunashirikiano na mashirika makubwa ya ndege kama Air India ambao wanachukua abiria wetu tunaowapeleka Mumbai kuwapeleka kwenye maeneo mengine, lakini kwa sasa tunakamilisha mazungumzo na KLM na Emirate ili kuboresha huduma pale tutakapoanza safari za Uingereza na maeneo mengine", amefafanua Eng. Matindi.



Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kwa sasa ina ndege 11 ambazo ni Boeing 787 ndege mbili, A220-330 ndege nne, Dash 8-Q400 ndege tano na tayari Serikali inaendelea na manunuzi ya ndege nyingine tano ambazo zinatajiwa kuanza kuwasili nchini mwaka 2023
 
nazan hatuna haja ya kuihoji serikali yetu maana hatuta pata tunacho takiwa kukipata...

hoja hazina mantiki...
 
ni kwa sababu hujui kinacho fanyika ndio tatizo... na una andika kama unajua ambacho atcl wana fanya...

kama kisinge kuwa na tija basi haya madege yasingekuwa yana nunuliwa kila uchwao...

wewe mwenye bisinezi modo sijui plani endelea kujenga hoja jf, nazani ndipo sehemu sahihi kujadili au kujenga hoja za atcl au mashirika ya ndege yajiendeshe vipi...

kila la kheri ktk safari yako mkuu
 
Kuna ndege nzuri tu atc wamenunua
Ndege nzuri sawa ila nyingi hazifit soko letu ndo maana nauli zi akuwa kubwa na ku discourage watu kupanda ndege zetu, Dar mbeya the cheapest ni 200,000plus one way, fast jet alikuwa hadi 90,000 one way
Dreamliner 787 ndege kubwa , inahitaji feeder planes na inahitaji pia kukaa kweye hub airport, Ethiopian haleti 787 , 777 au A350 hapa dar , hizi utazikuta Bole airport tu , hapa analeta 737, bombadier q400 ambazo technicaly zinatumika kama shuttle planes kuelekea kwenye ndege kubwa,
Ukishakuwa na ndege kubwa halafu likawa linajitafutia abiria kama hizi zetu , huwezi pata faida.
 
Hebu tuthibitishie kuwa ethiopian airlines inatoka capetown kupitia dar kwenda addis., tuwekee hata dumb itinerary.
Kuna wakati wanafanya hivyo hasa kama wakiwa na route za bombadier zao , kunaroute ethiopian huwa anafanya hata itinarary huwezi kupata ,
Kuna siku nilikuwa nasafiri kwenda sehemu kupitia bole , tulipaa dar na kushuka zanzibar abiria walitoka uk, then ndo safari ya bole ikaendelea , route hii nimewahi shuhudia mara kadhaa na huwa haipo kwenye ticketing options
 
Hao KLM twende nao taratibu wasije wakatupa kesi ya kulipa mabilioni. Sie size yetu INDIA na China
 
Kijiografia ukitoka SA unapita anga la BOTSWANA, MALAWI, TANZANIA kisha KENYA na hatimae ETHIOPIA (Bole). Hao wahudumu wa ET wana roho mbaya kishenzi. Safari ya masaa 6 msosi kiduchu.
 
Mode ya biashara ya ndege ambayo Atcl angepata faida mapema sana ni ile ya budget airline, sio hii ya bussiness class ambayo haswa ni kwa watu wa corporates, tulikuwa tuna mengi sana ya kujifunza kwa fast jet kabla ya kumfurusha
Ndege kama magari huwezi nunua vogue ili ufanye ubber , fast jet hakuwahi kuwa na turbo props ambazo ni slow na huruka umbali mdogo kutoka sea level
 
Madeni ya ATCL yanalipwaje? sina uhakika kama shirika ndio mmiliki wa ndege tajwa. Huenda ndo kikwazo cha kufanya partnership na ndege zinazojielewa eg. Swiss, Emirates, KLM, Oman Air, United Airlines etc
 
Kijiografia ukitoka SA unapita anga la TANZANIA kisha KENYA na hatimae ETHIOPIA (Bole).
Sahihi kabisa , lengo lao wanataka ku utilize zile ndege zao kubwa kwenye safari ndefu, safari ya south inaanza dar na ndege zao ndogo ,mkifika bole mnapanda kubwa halafu utaona kwenye map mnapita hapa hapa bongo tena kuelekea south
 
Madeni ya ATCL yanalipwaje? sina uhakika kama shirika ndio mmiliki wa ndege tajwa. Huenda ndo kikwazo cha kufanya partnership na ndege zinazojielewa eg. Swiss, Emirates, KLM, Oman Air, United Airlines etc
Ndo bussness plan ilipofeli hapo, Atcl ilitakiwa iwe declered bankrupt ,ili izaliwe new Atcl ambayo ingekuwa detached na madeni
 
Sahihi kabisa , lengo lao wanataka ku utilize zile ndege zao kubwa kwenye safari ndefu, safari ya south inaanza dar na ndege zao ndogo ,mkifika bole mnapanda kubwa halafu utaona kwenye map mnapita hapa hapa bongo tena kuelekea south
ET wanarusha ndege kubwa Boeing 787 mara 2/3 to Johannesburg (kwa siku)na Boeing 787 mara 1 to Cape Town (kwa siku). KQ anabwana pumzi huko ila bado kakomaa.
NB: Nauli zao bwerere, December 2022 naenda na familia Cape Town kiroho safi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…