Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

mleta mada unaleta hii habari kimzaha kwanini? Umenisikitisha sana. Tunapenda mzaha ndio Kwa mambo menginine lakini siyo kama haya. Kaamon ONDOA HARAKA SANA HIYO EMOJI YA ULIMI.

Poleni wahanga na wafiwa Mungu awape wepesi
 
Pole sana mkuu....ni wajibu wetu wazazi kuwalinda watoto wetu...japo ajali ni popote
 
Reactions: SDG
mleta mada unaleta hii habari kimzaha kwanini? Umenisikitisha sana. Tunapenda mzaha ndio Kwa mambo menginine lakini siyo kama haya. Kaamon ONDOA HARAKA SANA HIYO EMOJI YA ULIMI.

Poleni wahanga na wafiwa Mungu awape wepesi
Sishani kama ni mzaha, hicho ki-icon atakuwa amekiclick bahati mbaya. Hawezi kuwa na mzaha kwa habari kama hii.
 
Ajali ya kuua watu 50+ mbona itakuwa ya kutisha sana. Coaster inabebaje watu 50+? Nna mashaka na idadi inayoripotiwa... Ila all in all hata kama amekufa mmoja ni jambo la kusikitisha sana...

Mungu awarehemu watoto wetu na awape faraja wazazi wenzetu.

Wapumzike kwa amani. Amen.
 
Poleni wazazi wote na wanafunzi wenzao.ikiwa ni pamoja na uongozi was while. Mungu awatie nguvu ya kukabili majonzi mliyonayo.
 
mkuu ucsahau kama wanafunzi wanabebeshana, wanabana matumizi
 
We acha tu nipo na jamaa mmoja alikua eneo la tukio na kasaidia kuokoa anasema wamefariki wengi...
Yaani nawaza mpaka nasisimuka najikuta nawaona wanangu wakiwa wanaenda zile trips zao za study tour.. Mungu huyuu...
 
Aisee! Ajali zote ni mbaya,. Hii imezidi kuwa mbaya zaidi... Ee pokea roho za marehemu hawa, na kuzipumzisha kwenye makazi yako ya raha na amani huko mbinguni, Amen!
 

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…