Alichokifanya Israel ni dharau dhidi ya Iran. Kuna haja ya kurudia tena mashambulizi kule Israeli

Ni huzuni kwa kweli.
 
Ona ulivyo umedata.
Nani kasema kuwa Hizbollah ana makombora bora kuliko Iran!?
Nimekwambia miongoni mwa makombora bora ya Iran ni yale aliyoyatumia Hizbollah dhidi ya Israel kulipua Galilee.
Soma kwa umakini.
Una uhakika kuwa Iran hatoweza ku intercept hayo makombora ya Israel!?
Khordak-3 na khordak-15 zinafanya kazi gani Iran kama sio airdefence!?
Usisahau kuwa hayo makombora ya ujazo wa kati na pia US navy na RAF ya UK ilisaidia kuya intercept,au hilo umesahau mkuu!?
Je yangeenda mazima pasi na baadhi kudunguliwa na US navy na RAF na Jordan army Israel je ingekua na uwezo wa kuyadungua yote!?

Kama unadhani hizo ndio missile kubwa Iran alizo nazo basi pole sana.
Iran ana shehena ya makombora makubwa kuliko hayo alorusha.

Pia usijisahaulishe Iran alilenga Negev kambi ya jeshi hakulenga eneo la raia.
Tofautisha na Israel ambae yeye akirusha kombora hupiga shuleni,sokoni,majumbani hata mahospitalini,yani akiamua anapiga popote.
Iran alilenga sehem ya kambi ya jeshi.
Usijisahaulishe hilo.
 
Unamaanisha Iran hana makombora yenye ufanisi!?
Je yale makombora anayotumia Hizbollah yaliyoteketeza kambi ya Galilee Kaskazini mwa Israel kayaunda nani kama sio Iran!?
Kwahiyo unaamini makombora ya jana ndio ya kiwango cha juu ya Iran!?
Ushasahau kama JORDAN,USA,UK wame play part kubwa kudungua hayo makombora na drones!?
Au hilo unajisahaulisha!?
 
Order zimeanza huko

BREAKING: Lockheed Martin wins $17 billion US missile defense contract
 
Mlisema wako peke yao leo hii eti karuhusiwa na Urusi na Uchina? Hamkawii kuomba msaada mtakapoanza kutwangwa kama njugu
 
Asikupotezee muda huyo kipindi urusi inaanza kuishambulia Ukraine alimwaga mashudu mpaka baadae akaona aibu akakimbilia kijijini kwao kulima mpunga huyo ndie alie sema urusi wanatumia washing mashine kama silaha baada ya Ukraine hali kuzidi kua mbaya kakimbia uzi wenyewe
 
Hivi unajitambua wewe??
Tusishabikie vita ndugu zangu Watanzania.

Supply ikikata huko duniani shida ni kwetu, maana Kwa utegemezi HATUJAMBO!
Mwambie huyo pimbi hapo juu.
 
Mlisema wako peke yao leo hii eti karuhusiwa na Urusi na Uchina? Hamkawii kuomba msaada mtakapoanza kutwangwa kama njugu
Iran ni one man army.
Ila kama escalation itakua kubwa proxy wa Iran watakinukisha wa hapo hapo middle east,na Russia huwenda akatumia hiyo fursa pia kwa kumsapoti Iran.
 
Du leo umeongea point umetumia vizuri akiliyako kushinda ushabiki wa hao wanaoishi bongo known as wavaa miwani ya mbao ..Denmark imekufumbua macho.
 
Khordak-3 na khordak-15 zinafanya kazi gani Iran kama sio airdefence!?
Ni lini air defense system yoyote ya Iran iliwahi dungua kombora la Israel popote pale?
Tunao ushahidi wa mamia ya makombora ya Iran yakidunguliwa na Israel.
Khordak 15 inaishia kwenye kuzuia cruise missiles na sio ballistic missiles, hiyo system inazidiwa ubora hata na S-300. Lini S-300 iliwahi zuia aerial targets za Israel, hata ndege tu achana na makombora.

Hiyo Khordak 3 ungekuwa karibu yangu ningekuzaba kofi. System inayoiga BUK, yenye kubebwa na 6×6 truck na haizidi range ya 200km na altitude ya 30km izuie ballistic missiles za Israel?

Usisahau kuwa hayo makombora ya ujazo wa kati na pia US navy na RAF ya UK ilisaidia kuya intercept,au hilo umesahau mkuu!?
US Navy na RAF wamezuia makombora mangapi? Makombora mengi yametokea Iran yakapita nchi kavu kuja Israel, yaliyozuiliwa na US Navy ni yaliyopita mwambao wa bahari ni machache mno nadhani yametokea Yemen. RAF nayo imezuia machache sana. Labda useme US na UK wamezuia mangapi tuone.
Je yangeenda mazima pasi na baadhi kudunguliwa na US navy na RAF na Jordan army Israel je ingekua na uwezo wa kuyadungua yote!?
Hayo yaliyoenda Israel hayajaua hata mbwa koko. Kwamba Jordan iweze kuyadungua alafu Israel ishindwe? Direction ni hii, mengi Iran imeyapitisha route fupi ambayo haina air defense mpaka ukifika Israel
Kama unadhani hizo ndio missile kubwa Iran alizo nazo basi pole sana.
Iran ana shehena ya makombora makubwa kuliko hayo alorusha.
Makombora 300 ya uwezo wa kati hayajaambulia kitu, mlisema mnalipiza kisasi. Mara leo mnadai mna makombora makubwa kuliko, si mgetumia hayo sasa. Hamna kitu makelele tu
 
Kwanza ni kukosoe aliye italifu Israel kuwa Iran inajiandaa kuishambulia ni Marekani na si Israel yenyewe kugundua, nadhani viongozi wa Israel walivichukulia vitisho vya Iran kama vya siku zote tu mpaka walipo kuja kushutuliwa na Marekani kuwa Iran yuko siliasi.

Pia Iran iliitarifu Marekani na nchi za Kiarabu kuwa itatekeleza shambulizi dhidi ya Israel masaa 72 kabla ya kushambulia na mpaka saa Iran anaanza mashambulizi Marekani na Iran walikuwa na mazungumzo Marekani akijaribu kiushawishi Iran isifanye mashambulizi.
Kwa aina ya hili shambulizi baadhi ya wachambuzi wanasema wenda hili shambulizi Iran alitaka kuonesha ya kuwa ana uwezo wa kufanya kitu chenye madhara dhidi ya Israel na sio kuiumiza Israel.

Hao walio kaa hapo ni kama wanawake ambao wao wanaanzisha ugomvi alafu wanakimbilia kujificha nyuma ya Waume zao ili wawalinde, na hicho chumba walicho kaa kiko kwenye handaki walikuwa wamejificha kuogopa makombora ambayo ww upo hapa unayadharau.
 
Ona unavyoongea utumbo.
Ksifuatilie BAVAR 373 NI LONG RANGE ANTI BALLISTIC MISSILE.
Bado haujasema wewe.
Kwani kuna siku Israel amewahi kurusha makombora Iran!?
Embu nitajie hiyo siku.
Iran ina mifumo mingi tu ya air defence system sio Khordak peke yake kuna Bavar pia ambayo hutumika kudungua ballistic missiles.
Naona Israel iliweza kudungua makombora ya Hizbollah yalilolipua kambi za kaskazini mwa Israel.
Na usisahau nakusisitiza yale guided missiles zimeundwa na Iran.

RAF ilidungua zaidi ya drones na makombora ya cruise 70.
USA ilidungua idadi zaidi ama inayofanana na hiyo.
Jordan naye alidungua baadhi ya missiles na drones za Iran.
Israel ali intercept 120 drones + ballistic missiles na 7 zikapenya.

Nimekuuliza swali,je kama hayo mataifa yasingesaidia kudungua je Israel angeweza kudungua drones+missiles zote 300?
Kama tu 120+ zilizofika zimepenya saba je kama mzigo ungefika wote 300+ Israel angedungua zote!?
Sijui unasoma kwa uelewa we jamaa!?

Kama unataka tukuletee makombora yenye nguvu ya Iran tutakuletea.
Pia usisahau Iran alilenga kambi hakulenga eneo la raia.
 
Ww jamaa bwana unatapatapa sana ww siulikuwa unasema kuwa hakuna kombora lililo vuka mipaka na kuingia Israel sasa hiyo mifumo ya Israel iliyadungua saa ngapi hali ya kuwa hayakuingia kwenye anga yake?
 
Hizo drone za Iran na nyinginezo mbn speed zake zinajulikana hayo masaa 8 hata wasingesema hata wewe kama ni mwelewa ungejua.
Wangetaka kufanya shambulizi la kushutukiza wala wasinge tumia hizo drone bali wangetumia makombora moja kwa moja.
 
Iran amerusha makombora kwenda Israel huku akitoa taarifa. Ushawahi kuona vita inatolewa taarifa siku kadhaa kabla.

Hao walikua wanatuliza hasira tu za wananchi.
Endelea na uhandisi, hii kada iko juu yako saaaana ya issue za diplomacy. Alafu inaoneka history uliisoma ujaze mitihani tu. Mbona vitu vinajieleza tu hvo
 
Basi tunasubiri hiyo Israel yako ijibu ili tuone kama hayo unayo sema ni Kweli au utaumbuka kama ulivyo umbuliwa na akina Chui 2 na Abraham kwenye offense huko Ukraine mpaka ukaukimbia uzi, hapa upo una atupigia kelele tu.
Ww unadhani Marekani na washirika wake ni wajinga na wana mawazo ya kinyeto kama ww kuionya Israel isithubutu kuishambulia Iran ?
 
Kilichojitokeza ni hiki, Israel ilipoishambulia Iran, alijua fika kuwa Iran lipiza Kwa Ukali.
Kwahiyo Israel alichofanya ni kulinda Kwa Nguvu zote anga lake na kuweka Mfumo wa ulinzi standby.
Hata Sasa ulinzi umeimarishwa sana
Mkuu naomba kukuuliza, kutokana na shambulizi la Iran, Israel imelindwa au imejilinda!?
 
Siku si nyingi tutasikia "pray for Iran and children of Iran”
Kama wanahangaika na hezbollah kwa miaka zaidi ya 70 atamuweza iran??? Be serious my friend hujaona raisi wa israel kajishusha kasema walishambulia nyumba jirani na ubalozi wa iran na sio ubalozi wa iran, mambo siyo rahisi kama unavyoona kwenye movie
 

Attachments

  • Screenshot_20240414-183330_Instagram.jpg
    277.2 KB · Views: 2
  • Screenshot_20240415-122615_Facebook.jpg
    318.3 KB · Views: 1
Mkuu hebu tuekane sawa kwanza,hivi hayo yanayoitwa mafanikio ya Esrael kutokana na shambulizi la Iran yamepatikana baada ya kulindwa vyema na washirika wake au kujilinda yenyewe!? Maana naona sifa kubwa mno inapewa mifumo ya ulinzi wa Israel wakati kazi kubwa zaidi imefanywa na mifumo ya ulinzi wa anga ya mataifa mengine!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…