Aliyemshambulia mwenzie kisa Mwijaku akosa dhamana, atupwa mahabusu

Aliyemshambulia mwenzie kisa Mwijaku akosa dhamana, atupwa mahabusu

Sawa
Haisaidii, hao division one tuko nao huku tunasaga chaki,na huenda hata mishahara tunawazidi na wengine ni jobless.

Nadhani wewe ni mtu mzima usiyeendeshwa na mentality ya vyuo,eti chuo furani ni Bora kuliko chuo Y.


Waulize sasa hao division one ya udsm wako wapi?
Sawa bwana mdogo UDSM YA ZAMANI SIO KAMA YA SASA HIVI MTU KAPATA TWO IN EARLY 20s UDSM HAWAKUDAHILI KUSOMA PALE SASA HIVI WANADAHILI KILA GRADE UDSM YA ZAMANI SIO KAMA YA SASA
 
Wazazi wanajinyima na kuwalipia gharama za elimu wao wanakaenda kugombania wanaume shuleni.

Ona sasa. Huko akitoka hata kusoma hataweza kusoma vizuri. Ng'ombe kabisa.
 
Sawa

Sawa bwana mdogo UDSM YA ZAMANI SIO KAMA YA SASA HIVI MTU KAPATA TWO IN EARLY 20s UDSM HAWAKUDAHILI KUSOMA PALE SASA HIVI WANADAHILI KILA GRADE UDSM YA ZAMANI SIO KAMA YA SASA
Basi UDSM ya zamani ni hovyo sana kama watu kama wewe waliosomea UDSM ya zamani walikuwa wanaandika paragraph nzima kwa herufi kubwa.
 
Kumbe ni manka, nimekuelewa.
Kina manka huwa hawakurupuki.
Atavumilia mpaka siku litimie ndio anafanya majambo
Huwa wanafundishwa kuwa ngunguri palipo na neema. Pale hela za fala mwijaku zinaliwa vizuri tu na anawekeza kwao huko😁 siku ndugu yenu nguvu za kupiga kelele zikiisha mtaskia mlio.
 
Mwijaku naye alikuwa mtuhumiwa mwanzoni, naona baada ya kubanwa pumbu na polisi walimuachia...
Polisi hawawezi kumbana pumbu, hana kosa na pia hao watoto sio under 18 years. Wangekuwa minors ndio ingekuwa kasheshe japo kwa kutumia mgongo wa uchawa wa mama angejikuta yuko free kwa simu moja tu kutoka mitaa ya Ferry.
 
Wanafunzi wa "Vyuo vikuu"! 😁
Sio ajabu siku hizi ajira hamna aisee!
 
Mmoja kati ya wanafunzi watatu kutoka vyuo vikuu tofauti tofauti jijini Dar es Salaam, waliodaiwa kumshambulia mwenzao wakimgombania msanii na mtangazaji wa vipindi vya redio, Burton Mwemba maarufu kama Mwijaku, ameswekwa mahabusu baada ya kukosa dhamana katika kesi ya jinai inayomkabili na wenzake hao.

Mwanafunzi huyo Mary Gervas Matogolo (22), mwanafunzi wa
Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) na wenzake wawili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu, leo Mei 30, 2025.

Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Gwantwa Mwankuga, wanakabiliwa na jumla ya mashtaka manane ya kusababisha madhara kim-wili, kutishia kuua, kutoa taarifa za uongo mitandaoni na uharibifu wa mali.

Mbali na Mary wanafunzi wengine waliopandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa tuhuma hizo ni Ryner Ponci Mkwawili wa

Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam na Asha Suleiman Juma, wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu, Dar es Salaam (TIA) wanakabiliwa na mashitaka manane.

Hakimu Gwantwa, alitaja masharti ya dhamana, kuwa kila mshitakiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili, wenye barua za utambulisho, vitambulisho vya Taifa, watakaotia watakaosaini Bondi ya dhamana ya Sh5 milioni kila mdhamini.

Washtakiwa Ryner na Asha wametimiza masharti hayo na kuachiliwa huru kwa dhamana lakini Mary ameshindwa kutimiza
masharti hayo ya dhamana.

Hivyo Hakimu Mwankuga ameamuru apelekewe mahabusu gerezani mpaka Juni 13, 2025, kesi hiyo itakapotajwa tena


View attachment 3351673
Yaone kwanza kazi kusumbua wazazi tu.........hata ndoa hayana lakini yameperekana mpaka mahakamani kwa ajili ya U......b.......o........o....... kweli mchuma janga hula na wa kwao
 
Back
Top Bottom