Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Mbowe sio mjinga alishatambua hilo,hasa pale vikaragosi tokea chama kingine walikuwa wanataka eti Mbowe angatuke kisa hanunuliki.
Kumbuka Chadema sio lelemama.
Ndugu una macho lakini huoni, tatizo la CHADEMA ni Mbowe ila kwa kuwa mnajifanya vipofu basi endeleeni na upofu wenu.
 
mwana wa Tanzania,
Kwahiyo ile Kesi yake iliyokuwa ikimkabili Yeye na Viongozi (Wabunge) wa CHADEMA atakuwa ameshanusurika nayo au atakuwa akiendelea Kuihudhuria huku akiwa amevalia Sare ya Chama chake Kipya?
Si unaona hata yule chapombe wa kule banabana alikuwepo kwenye msafara wa viongozi wa Chadema ambao wako kwenye kesi hii lakini yeye hakushtakiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hii trend ya wanaume na ndevu zao kulamba matapishi yao hadharani na wanapohojiwa wanakua wengi wa visingizio kuwa ndo siasa ilivo inakupa picha moja tu kuwa kwa Tanzania wanawake wako strong na wanasimamia wanachokiamini kuliko wanaume
 
Wenye chama chao wanaamini ndiyo kinaimarika zaidi sasa hivi. 😁!

#MwambaTuvushe! #5Tena!

Mashinji aliwahi kuimarisha chama mpaka useme chama ndio kinapoteza uimara kwa yeye kuhamia ccm? Huyo domo zege ndio alichangia cdm kuwa waoga.
 
Bro naomba tujitolee kutafuta njia za kujenga upya ushupavu wa vijana kusimamia wanachokiamini. Yaani Nyerere ameondoka na dhamira yake.

Inaumiza sana watu wametumia pesa kusomesha watu ambao hata wao wenyewe wanashindwa kujisimamia.Inaumiza sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM uchaguzi huu kutakuwa na kugombania madaraka kama wakulima na wafugaji.
 
Utanisamehe lakini nadhani mnahitaji kufanya kazi ya ziada kubadilisha chama chenu kipo kwenye hali mbaya. Mnachofanya sasa ni kama Magu anavyojifanya uchumi wa nchi unaendelea vizuri.
CHADEMA haiwezi kuzuia watu kununuliwa ama kujiuza , hii si kazi yetu , bali unachotakiwa kufahamu ni kwamba kabla KANU ya Kenya haijafa na kuzikwa , ilifanya kama inavyofanya CCM, ilinunua kila imtakaye akiwemo Raila Odinga aliyepewa Ukatibu Mkuu.
 
Mashinji aliwahi kuimarisha chama mpaka useme chama ndio kinapoteza uimara kwa yeye kuhamia ccm? Huyo domo zege ndio alichangia cdm kuwa waoga.
Kama hamkuona mchango wa Slaa baada ya kuhama itakuwa Mashinji?

Hakuna jipya!
 
Asalaleee tumembakiza Mboye tu. Nayeye ataunga mkono juhudi.
 
mwana wa Tanzania,
Mungu tupe ujasiri tuweze kutumia elimu zetu kujiingizia kipato. Pamoja na elimu yako anajiunga CCM ili apewe kazi ya kuajiriwa kupitia teuzi badala ya kufungua hospitali yake na kutoa ajira kwa madaktari walioko mitaani.

Chonde chonde CCM mrudisheni huyo kwenye fani yake ya utabibu badala ya kumpa vyeo vya kisiasa.
 
Hii usaliti wa Mbowe utakitafuna CHADEMA miaka mingi ujayo.!

Mbowe hakustahili kuendelea kuwa mwenyekiti wa CHADEMA, yeye ndio msimamizi na muongozaji wa hawa viongozi wasaka madaraka ndani ya CHADEMA. Tulipiga kelele sana kuwa hakupaswa kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm ili hili kosa lake lipatiwe ufumbuzi na sura tofauti.

Ni nani alikuwa hajui kuwa Mashinji hakuwa kiongozi sahihi wa CHADEMA hasa kwa cheo cha ukatibu Mkuu? Kama katibu mkuu ambaye alikuwa mtendaji mkuu anaondoka chamani na kusema kuwa amegundua cdm haina mpango wa kuletea wananchi maendeleo, hapo mwenyekiti anaendelea kukaa ili iweje?
 
Back
Top Bottom