Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Na mimi sina chama lakini kuanzia leo ninajiunga na CCM rasmi. Bwana Polepole kadi ya mwanachama kiasi gani na niipatie wapi?. Kama ni kulipa kwa mtandao nilipe halafu mniambie nikachukulie wapi.
 
Big up CHADEMA

Vichwa vya habari vya magazeti mwezi huu wa February vingekuwa:
1 Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Pwani ahamia CCM (Sumaye)
2. Mwenyekiti wa CHADEMA ahamia CCM (Cecil Mwambe)
3.Katibu mkuu wa CHADEMA ahamia CCM (Mashinji)

Kweli mko makini
 
Huyu jamaa nilimstukiaga siku ya kwanza kujiunga, sijui kwanini wale wote roho yangu iliyowastukia wote wamerudi walipokua.

Ivi yupo kwenye kesi ya Aqulina?
 
CCM inatumia akili ndogo sana kupumbaza CHADEMA. Na daima siku zote Chadema itakuwa kwapani kwa CCM hadi siku chama hicho kikifa.
 
Huyu Dr mashinji Duh! By the way ndiyo maana Mbowe hakumpendekeza kuwa katibu mkuu alishamuona kuwa na dalili ya Kuunga mkono juhudi
Huyu intelijensia ya CHADEMA ilishammulika kitambo tu ila ilisubiriwa wakati muafaka wa kumpiga chini bila kelele wala mikwaruzo.

Imagine Sumaye au Mwambe mmoja wao angechaguliwa kuwa mweyekiti Taifa na Maahinji angeendelea kuwa KM, leo hii kungekuwa na CHADEMA? Ndiyo maana wapiga debe wakuu wa Sumaye na Mwambe walikuwa wanaCCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa siasa zilizo serious - Mbowe na Lisu walitakiwa wajiuzuru kwa ujinga walioufanya 2015
Wenye akili wengi tulijua consequence za utapeli ule.
 
Kama hamkuona mchango wa Slaa baada ya kuhama itakuwa Mashinji?

Hakuna jipya!

Kwa taarifa yako, uimara na kukubalika kwa CHADEMA ilikuwa ni uwezo binafsi wa Slaa kujenga hoja. Mbowe alikuwa anatembelea nyota Slaa na ndio maana Slaa kaondoka Mbowe kaishia kuchemsha na kuomba maridhiano yasiyo na kichwa wala miguu. Huyo Mashinji alikuwa takataka kama takataka nyingine.
 
dah ni pigo kubwa sana la CHADEMA ikiwa ni siku chache tu baada ya MWAMBE na SUMAYE kuhamia CCM haiya kazi ndo kwa kwanza imeanza ikiwa ni dakika ya tatu ya mchezo mpaka tukafike 45 sijui itakuaje
Tumia akili hata hiyo kiduchu uliyo nayo, pigo gani wakati alishapigwa chini? Ingekuwa bado ni KM sawa, hivi unajua kwa nini alitupiwa virago?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom