Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Next ni Bulaya na wenzake.
Kuhama chama ni haki ya msingi ya kila mtu kikatiba, ndiyo maana Tundu Lissu alihama kutoka NCCR Mageuzi na kwenda Chadema, Zitto alihama kutoka Chadema na kwenda ACT, Sumaye na Lowasa walihama kutoka CCM na kwenda Chadema na baadaye wamerudi tena CCM, Nyarandu alihama CCM na kwenda Chadema, Maalimu Seif alihama CCM na kwenda CUF na baadaye ACT.

Huo ndio ukomavu wa demokrasia, unaamua uwe chama gani kwa ridhaa yako. Mtu anapohama chama hutakiwi kumkejeri na kumtukana ni haki yake kikatiba na hiyo ndiyo demokrsia tunayoitaka kila siku na kuihubiri.
 
kazi ya kuhama hama inakuja kukamilika mwezi wa 7 baada ya kukatwa na kukatika, hawa ni watovu wa nidhamu wanaaribu vyama
 
Yaani “wanamuomba Mwenyekiti kujiunga” na wanapokelewa hapohapo. CCM bana na hizi abradacadabra!

Mashinji kapiga hesabu za mbali akaona isiwe taabu. At 47 yesrs huku watoto wakiwa bado wadiho and jobless, ameamua kurudisha mpura kwa kipa. Bila shaka kaahidiwa donge nono mno
 
Huyu mashinji mimi nilimuona kitambo hakuwa na msaada kwa chadema kama vile akitumika indirect
sasa ni wakati upinzani wajenge chama cha upinzani makini, hawa wapita njia ndio iwe mwisho

Viongozi makini chadema wanajulikana kwa asilimia

Tundu Lissu 100%
Mbowe 100%
Msigwa 100%
Mnyika 70%
Halima Mdee 100%
Bulaya 60%
Heche 70%

Waliobakia kwa chadema ni 50-50 hawafai kabisa kupewa nafasi za uongozi wowote wa juu ni hatari tupu, wananunulika kwa bei poa kabisa.

Kule zanzibar Jembe ni Maalim Seif 100% na Mazrui 100% waliobaki ni mashaka mashaka matupu.
 
Huyo anaiweka ile kesi yao ya kuchonga ktk mazingira magumu kwani yeye tayari amesharidhia lile takwa lililofanya waundiwe hiyo kesi.

Hii serikali haina cha kuwashawishia watu wajiunge nayo tofauti na kutoa ahadi za vyeo kwa walengwa au kukubaliana nao bei kabisa halafu eti bado wanahimiza watu walipe kodi.

It defeats common sense to urge and rally people to pay taxes while using the fraction of the taxes so paid to lure the opposition politicians to join your corrupt government, this reflects nothing but the epic of ineptitude and lunacy.
 
Doh kwa hiyo leo story ingekuwa Mwenyekiti wa CDM (Mwambe) na Katibu Mkuu CDM (Mashinji) wahamia ccm. Hongera CDM.
 
Halitasalia jiwe juu ya jiwe, asema bwnaa wa majeshi. Bado kusikia Erythrocyte na Salary Slip . Muda si mrefu Chadema mpya itachipuka chini ya Kamanda Mnyika.
Nasi wanachadema tulio uhamishoni, tutarejea nyumbani kwa furaha.
 
Back
Top Bottom