Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

CHADEMA wametoka watu wengi,viongozi na wasio viongozi,kutoka kwao hakukunitisha,ila walipotoka watu Hawa wawili nilijuta Sana,nilisikitika Sana,niliogopa Sana nikijua CHADEMA Sasa Basi,haipo tena na Wala haitasimama Tena.

Watu wawili hao walikua na nguvu Sana,waliifanya ikapendwa na maelfu ya Watanzania Mimi nikiwa mmoja wapo,wawili hao ni Slaa na Zitto.

Hata hivyo cha kushangaza pamoja na kutoka kwao CHADEMA bado ipo. Hawa wengine waliotoka wacha watimize Haki yao ya kidemokrasia.

Hata hivyo kuna baadhi wapo waliobaki wakitoka labda hofu yangu itatimia,ila Hawa wanaotoka SASA ni afadhari watoke tu,maana ni walikua mzigo.
 
Hakuna namna yoyote Mbowe anaweza kukwepa lawama kwa hili lililotokea leo hii, ilikuwaje wa/akampa nafasi nyeti ya Katibu Mkuu wa Chama?

Kwa kipindi chote alichohudumu kama Katibu Mkuu ambaye kimamlaka anahudhuria vikao vyote nyeti vya chama... mangapi yamevuja?

Hata kama wameshtuka mwishoni na kumpa Mnyika nafasi ya Ukatibu Mkuu wa Chama, its too late. Chama kimeyumba sana chini ya Mashinji kama Katibu Mkuu, tulipokuwa tukiuliza tunapewa majibu rahisi ya mtu wa ofisini! Kumbe alishakuwa recruited na Lumumba, aibu gani hii?
 
Hivi hawezi kubaki tu na taaluma yake kama siasa haiwezi?
 
Huwezi kuwa chadema kabisa wewe naapa! CHADEMA hakuna asili ya umbeya na ushambenga!
Mabadiliko ndani ya CHADEMA wanayaona. Huwezi kuwa na kundi la watu bila kuwa na mapungufu.

Naamini iko siku hili pungufu linalo tusumbua tutalijuwa. Kila mabadiliko yana chanzo na iko siku tutaweza kuanza kufanya mabadiliko.
 
Pompeo na Bi Nancy wapo wanajiuliza hii nchi inayoitwa Tanzania wana mfumo gani wa siasa!
 
Doh kwa hiyo leo story ingekuwa Mwenyekiti wa CDM (Mwambe) na Katibu Mkuu CDM (Mashinji) wahamia ccm. Hongera CDM.
Kuna kitu kinaitwa Propositional Logic: A if and only if B. Kama Mashinji angeendelea kuwa Katibu Mkuu na Mwambe akaukwaa Uenyekiti ambapo ruzuku, mizigo na mafungu yote yapo at their disposal.

wasingekwenda CCM. Hiki unachokiona ni katika jitihada za kumaintain their status-quo in life na kuhakikisha familia zao zinaendelea kula mema ya Nchi
 
CDM imepitia changamoto nyingi lakini bado inaendelea kusimama imara!
Slaa alikua na nguvu Sana Chamani,lakini alivyoondoka alindoka na mke wake tu,Zito alikua Ana NGUVU Sana Chamani kwa kweli alivyoondoka alindoka na vikundi vya watu, lakini cha kushangaza CHADEMA imeendelea kuwepo,ukimya huu wa CHADEMA ni ukimwa wa kuwekewa minyororo miguuni,wakitaka kujua Kama ukimya huu ni wa kifo, wafungue hiyo minyororo.
 
Huyu jamaa hakua na mvuto tokea kipindi hiko....hapa najiuliza tu kama angekua bado katibu mkuu angeondoka?au kaondoka kwakua amepigwa chini?
 
Back
Top Bottom