Kuhama chama ni haki ya msingi ya kila mtu kikatiba, ndiyo maana Tundu Lissu alihama kutoka NCCR Mageuzi na kwenda Chadema, Zitto alihama kutoka Chadema na kwenda ACT, Sumaye na Lowasa walihama kutoka CCM na kwenda Chadema na baadaye wamerudi tena CCM, Nyarandu alihama CCM na kwenda Chadema, Maalimu Seif alihama CCM na kwenda CUF na baadaye ACT.
Huo ndio ukomavu wa demokrasia, unaamua uwe chama gani kwa ridhaa yako. Mtu anapohama chama hutakiwi kumkejeri na kumtukana ni haki yake kikatiba na hiyo ndiyo demokrsia tunayoitaka kila siku na kuihubiri.