Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

CHADEMA WOTE HAMIENI CCM MPEWE VYEO HAPO NDIO MTAWEZA KUTWALA NCHI KWA MGONGO WA NYUMA CCM WAKISHTUKA IMOOO. SASA HIVI CCM WANASHANGILIA CHADEMA KUPEWA VYEO NDANI YA CHAMA CHAO. HUYU MASHINJI WALIKUWA WANAMUITA KILAZA ILA ATAPEWA BONGE LA CHEO WALE WA BUKU SABA WATABAKI WANASHANGAA. SIASA NI SAYANSI.
 
Hali hii itaendelea weeeee mpaka itafikia chuki kubwa miongoni mwa CCM na CHADEMA, ikifikia hapo sasa yeyote atakaetoka CHADEMA kwenda CCM ataonekana msaliti mkubwa atatengwa na Jamii hawatoshirikiana nae kwenye maziko ama kwenye furaha, hapo sasa tutashuhudia upinzani wa kweli na ukombozi utakuwa umekaribia.
 
2008 - 2010 Evin School of Management (Shahada ya Uzamili (Masters) ya Public Relations (CSR)
Kiukweli mtu aliyesomea MD halafu anakuja kufanya masters ya PR na alikuwa na PR mbovu vile, huyu mwacheni aende tuu, ana very impressive CV lakini delivery ni bure kabisa!.

Ila na yeye angalau amejitambua
P
 
Mbowe sio mjinga alishatambua hilo,hasa pale vikaragosi tokea chama kingine walikuwa wanataka eti Mbowe angatuke kisa hanunuliki.

Kumbuka CHADEMA sio lelemama.
 
feyzal,
Wabunge wengi mliokua nao leo ni kwa ajili ya Lowasa.

Labda kama hujui siasa ndio unaweza kusema hivyo. Lowassa alete wabunge wengi kwa kupanda jukwaani na kuongea dakika 2 kwa kusema "Elimu, elimu, elimu? Je, angeweza kuongea nusu saa si angekuwa rais wa Afrika mashariki kabisa. Kwa taarifa yako Lowassa aliikuta CHADEMA ikiwa bora kuliko maelezo, na hata kitambulisho cha kura kiliitwa kichinjio kwani watu walijua Lowassa atapitishwa na CCM.

Ni bahati tu watu walikuwa wanaikubali sana cdm kiasi kwamba hata Mbowe alipofanya upuuzi wa kubadili gia angani bado watu wengi waliopata kura CHADEMA. Usitoke kupotosha ukweli. Kama wabunge wengi waliletwa cdm na Lowassa akiwa na miezi miwili kabla ya uchaguzi, tuonyeshe alifungua matawi mangapi ya CHADEMA baada ya uchaguzi.
 
Kweli Tanzania waliosoma wana matatizo ya kuchanganua yanayowahusu. Daktari wa binadamu,bado anahangaika na kubadili vyama?.

Yaani ameshindwa kutumia elimu yake kusimama na kuwa kioo cha vijana kujitegemea?!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sasa akihudhuria kwenye kesi yake atakuwa nzi wa kijani katikati ya makamanda
 
Mbowe sio mjinga alishatambua hilo,hasa pale vikaragosi tokea chama kingine walikuwa wanataka eti Mbowe angatuke kisa hanunuliki.
Kumbuka Chadema sio lelemama.
FB_IMG_1570488518462.jpg
 
Kwa akili hizi na haya yanayoendelea, sidhani hata kuna haja ya kuwa na multiparty system nchi hii. Inavyoonekana ni kuwa upinzani nchi hii umejaa mamluki wengi toka CCM.

Ni upumbavu wa hali ya juu kudhani kuwa hawa wanasiasa tunaowaamini kuna siku watalivusha hili taifa, everyone is fighting really hard to feed himself.
Hayo tuliyazungumza kitambo tokea 2015
Tanzania bado haina Upinzani Kuna Mamluki tu
Lakini Vibendera kutwa kutukana
Wataelewa tu
 
Wenye akili wanaondoka CHADEMA kukimbia udhalilishaji wa kuongozwa kishikaji.
Wanaotaka viti maalum wanaondoka CHADEMA kwenda CCM kwenye takrima ya vyeo.

Huyu tulishamstukia siku nyingi sana alikuwa anawasiliana na watu wa kitengo na viongozi wa juu kabisa wa CCM. Kwa vile kumchinja kobe yataka timing basi wakati muafaka akachiliwa mbali kimtindo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wale wote waliomwagwa na CHADEMA wanahama kwa speed ya 5G..huko CCM kuna nini jamani na sisi tukuje wote
 
Back
Top Bottom