.
By Sangu J
.
Leo Februari 18, 2020 tumeshuhudia uamuzi wa msomi mwingine na Kigogo ndani ya CHADEMA Dkt. Vicent Mashinji, na kuamua kuingia kwenye na Sera za Chama cha Mapinduzi.
.
Dkt. Mashinji ameeleza. sababu mbalimbali za uamuzi wake lakini kubwa ile anayosema alitamani zaidi kuwa sehemu ya watu wanaoleta maendeleo katika nchi yake ya ahadi ya Tanzania.
.
Japo wanasema ni uamuzi wake kikatiba lakini mimi napenda nijadili kidogo athari zinazoweza kujitokeza kwa chama chake cha zamani hasa kuelekea kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi na baada ya uchaguzi, na moja ya athari kubwa wanayoweza ipata CHADEMA kuondoka kwa Mashinji ni kukosa mvuto kwa wasomi.
.
Unajua kwa siasa za Tanzania Chama Tawala kwa kawaida huwa anakua na mvuto kwa kundi la wasomi kutokana na kuwa nafasi mbalimbali ambazo zinaweza kuwafaa wasomi, lakini vyama vya upinzani nchini kitu pekee kinachoweza kuwavutia wasomi ni uwepo wa wasomi wenzao ndani ya chama, ndiyo maana miaka fulani uliikuta CHADEMA iliweza kupenya mpaka Vyuo Vikuu kwa kuwa na wasomi mbalimbali kama Prof. Safari, Baregu, Kitila Mkumbo, Esther Matiko na wasomi wengine kama Slaa, Dkt. Mashinji, na kuliifanya CHADEMA kuwa kivutio kwa baadhi ya wasomi kwa sababu wenzao walikuwepo huko.
.
Kuondoka kwa Prof. safari, Slaa, na Mashinji ni miongoni mwa mapigo ambayo yameikuta CHADEMA na yanaweza kuipoteza kuelekea uchaguzi wa 2020 na 2025 kwa sababu kuna baadhi ya Analysis za kisomi wanazikosa kama ilivyo kwa CCM.
.
Dkt. Slaa alishawahi kusema siasa ni mchezo wa hesabu za kupata watu, na mfumo bora zaidi ambao ulikuwa unatumiwa na vyama vya upinzani ni kukuza vijana kutoka Vyuoni ambao idadi kubwa huwa wanavutiwa zaidi na Prof. na Dkt.
.
Naiona CHADEMA itakayokuja kufanana na CUF miaka 10 baadaye kwa sababu ya kukosa wasomi, ambao chachu ya kufanya tafiti ndani ya chama.
.
#MaoniYangu #KijanaMzalendo
#IloveTZ
Sent using
Jamii Forums mobile app