Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Mkurugenzi wa Habari Chadema Mh. John Mrema azungumza baada ya Mashinji kuondoka

 
Unafikiri hana njaa huyo jamaa.

Kule alikuwa kwa special task anarudi kupeleka reports ndio wakome CHADEMA kuparamia watu wasiowajua.

Nakukumbusha ishu ya Dr Ulimboka, unaikumbuka? Ila ili tuliache tutaongelea baadae ila CHADEMA inaenda kuwa TLP soon.
Aisee unataka kusema alipenyezwa?
 
CCM BADO NI CHAMA KUBWA SANA. VYAMA VYA SIASA TANZANIA VINAMILIKIWA NA WATU BINAFSI WAACHENI WATU WAFANYE MAAMUZI KWANI HAKUNA DEMOKRASIA.

1. ACT WAZALENDO - ZITO KABWE
2. CHADEMA - FREEMAN MBOWE
3. CUF - IBRAHIM LIPUMBA.
4. ....

KWANI CCM INAMILIKIWA NA NANI?

WAACHENI WATU WENYE AKILI ZAO TIMAMU WAFANYE MAAMUZI NA WALIOFUNGWA AKILI KICHAWI WAENDELEE NA VYAMA VYA WATU BINAFSI.
 
Huyu alibaki chadema kwa sababu ya cheo tu, katibu Mkuu ambaye angeifaa chadema Ni albanie marcus
 
Dakika chache baada ya kuhamia CCM, Bwana Mashinji amebadili cover photo ya ukurasa wake wa Twitter na kuandika "Remember you have a family to feed, not a community to impress".View attachment 1361832
_
Nini maoni yako?
Bora amekuwa muwazi kuwa maslahi binafsi ndiyo yamempeleka huko tofauti na ile misukule mingine iliyokaririshwa kuwa inaenda kuunga juhudi. At least amejiweka huru hivyo tumuache akatafute mkate wake na familia yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hayati Mwalimu J. K. Nyerere alivyosema, " Ukitenda dhambi ya ubaguzi haishii hapo, itaendelea"
Kupinga ufisadi uliokuwa unafanywa na utawala wa CCM wa awamu za nyuma kuliifanya CHADEMA ipate umaarufu mkubwa.

Kumpokea Lowassa na kumpa nafasi ya kuwa mgombea wa Urais, CHEDEMA walitenda dhambi kwa sababu huyo ndiye walikuwa wanamtuhumu kama ni fisadi aliyekuwa katika kundi la aibu ( group of shame).

Baada ya kutenda dhambi hiyo na kubaki nayo, CCM kupitia Rais mteule wa awamu ya Tano alitubu dhambi ya ufisadi kwa niaba ya chama chake na kuwawajibisha mafisadi wote wa kipindi cha nyuma na wa kipindi chake.

CHADEMA imeshindwa kuwa na hoja ya kuwapatia umaarufu tena na badala yake wamebaki kama wanaharakati wa kudai uhuru bila kujali wao wakichukua madaraka watafanya nini.

Sisi tuliokuwa tunapenda upinzani imara ili uimarishe chama chetu cha CCM, Tumebaki na wasiwasi mkubwa kwa sababu siku tukipata Rais dhaifu Inchi itarudi tena kwenye Ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.
 
Kama mliyagundua hayo kwa hiyo mnayoiita intelijensia ya chama kwanini hamkumvua uwanachama na kumfukuza chamani huyo Mashinji? Yani mtu anasuka mipango yote hiyo halafu mnambakisha chamani wa nini? Tena akiwa Katibu Mkuu wa Chama kitaifa?
Haiingii akilini
 
Tumekusamehe mashinji ukweli umekuweka huru make njaa hainaga baunsa
 
I see, judgement za wanasiasa wetu bado zinaathiriwa na njaa, hakuna mahali tunaweza tukawa na wanasiasa wenye kauli thabiti, watu wenye kusimamia maslahi ya nchi kama hayo maslahi ya nchi hayana maslahi ya matumbo yao. Bado tuna safari ndefu
 
CHADEMA mmekwisha nyinyi ni chama cha mtu binafsi msitegemee watu wenye akili timamu kuendelea kuwaunga mkono. Endeleeni na SACOS ya Mbowe
 
Back
Top Bottom