Kama hayati Mwalimu J. K. Nyerere alivyosema, " Ukitenda dhambi ya ubaguzi haishii hapo, itaendelea"
Kupinga ufisadi uliokuwa unafanywa na utawala wa CCM wa awamu za nyuma kuliifanya CHADEMA ipate umaarufu mkubwa.
Kumpokea Lowassa na kumpa nafasi ya kuwa mgombea wa Urais, CHEDEMA walitenda dhambi kwa sababu huyo ndiye walikuwa wanamtuhumu kama ni fisadi aliyekuwa katika kundi la aibu ( group of shame).
Baada ya kutenda dhambi hiyo na kubaki nayo, CCM kupitia Rais mteule wa awamu ya Tano alitubu dhambi ya ufisadi kwa niaba ya chama chake na kuwawajibisha mafisadi wote wa kipindi cha nyuma na wa kipindi chake.
CHADEMA imeshindwa kuwa na hoja ya kuwapatia umaarufu tena na badala yake wamebaki kama wanaharakati wa kudai uhuru bila kujali wao wakichukua madaraka watafanya nini.
Sisi tuliokuwa tunapenda upinzani imara ili uimarishe chama chetu cha CCM, Tumebaki na wasiwasi mkubwa kwa sababu siku tukipata Rais dhaifu Inchi itarudi tena kwenye Ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.