Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Mimi bado nasema Mbowe ana stahili kuubeba huu mzigo wa lawama 2015 alitukosea sana Kumpa Lowassa....wale waliopigania chama kwa moyo mmoja walitengwa kwenye baadhi ya maamuzi mazito leo upinzani umelegea.


Atuombe radhi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nasema Mh Mbowe anastahili pongezi nzito, maana alikuwa amezungukwa na mamruki na waganga njaa ndani ya chama!, lakini amekipambania chama hadi leo kipo pamoja na msukosuko kinachopitia!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa ni STATE AGENT..

CHADEMA walifanya makosa makubwa kumfanya kuwa Katibu Mkuu

CHADEMA lazima wajiimarishe kwenye Intelligence yao, vinginevyo kila mara watakuwa wanarudi nyuma.

Wawapuge wasiohusika na chama chao
Namsikiliza hapa anajitetea .baada ya kutolewa nafasi ya Ukatibu Mkuu kaona tonge limedondoka kaamua kuhamia CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daktari mzima wa binadamu mwenye elimu kubwa kiasi hiki kujihusisha na siasa africa.....such a waste. Bora angetafuta kazi ya udaktari nje ya nchi
 
Naendelea kuwaonya vijana wa kitanzania, msikubali kuvunjwa miguu au kuumizwa kwa namna yoyote ile mkiwapambania wanasiasa wa taifa lenu. Kama umeamua kupambana, pambania kile unachoamini na sio mwanasiasa.

Wanasiasa wa Tanzania ni wachumia tumbo,hawajui itikadi na hawana itikadi. Wanatafuta ugali, ndio maana wataungana na kuwa wamoja pale ugali wao utakapojaribiwa.

Haya,bado wengine wengi wataendelea kuwavunja moyo kwakuwa mliwapambania.
 
Siasa za Kusini mwa Jangwa la Sahara....

Siasa za kimaslahi....
 
mwana wa Tanzania,
Screenshot_20200218-122437.png
 
Back
Top Bottom