Ally Dangote auawa jijini Arusha
Nipo serious mkuu,ukute alifananishwa au labda niyeye,ndomaana nikasema,ni vema angetiwa nguvuni,halafu afikishwe mbele ya vyombo vya sheria,haki itendeke.Hiyo mob justice,ingekua vema ikaelekezwa kwa wezi wa mali za umma,ambao wanajulikana na karibia kila mtanzania,ila sheria hazichukui mkondo wake,jamii ingeheshimika,kuliko kumuua mtu,tena yawezekana hakupewa hata nafasi ya kusikilizwa,lakini ndo hivyo.Kuna habari za watu wengi tu kuuawa,kwa kuitiwa mwizi,huku si kweli,na watu kuua bila kumhoji wala kumsikiliza,siyo fair kabisa.Anyway ndiyo umma wetu huu.
Nimeweka link hapo juu, alikamatwa na akakiri kabisa mwaka jana mwezi wa 5 lakini wananchi wanashangaa yupo bado mtaani.
 
Pole kwa familia,ndugu na jamaa,may his soul R.I.P.
Mob justice ni mbaya,wangempeleka mbele ya vyombo vya sheria,haki itendeke,ukute alisingiziwa au kafananishwa.
Nani angeenda kutoa ushahidi kuithibitishia mahakama kuwa aliua? Mahakama haiwezi kupata ushahidi wa uhalifu, jamii inayomzunguka ndiyo inayomjua. Hayajawahi kukukuta ndiyo maana unasema R.I.P kwa muuwaji aliyeuawa. Wakati mwingine tukubali tu kuna wahalifu tunaishi nao kwenye jamii zetu inatakiwa wasiishi wanasumbua kuanzia wazazi wao. Jamii za zamani wazazi walikuwa wana declare kwamba huyu katushinda wazee wanamaliza wenyewe. Huwezi kuishi mtaani mnashindwa hata kutuma mtoto dukani kwa sababu ya pimbi mmoja ambaye mnamjua
 
Ni kweli mob justice ni mbaya. Lakini ukiona katajwa hilo jina inaonekana ni mtu maarufu kwa shghuli hiyo na anafahamika kwa hilo.

Shida kubwa ni polisi huwa wanawaachia wakishahonga.
Screenshot_20231120-164028_WhatsApp.jpg

Kulikuwa na kampeni kubwa sana kumsaka, yapata mwezi mzima
 
Kwanini hakuna Mob Justice kwa mafisadi wa fedha za Umma na extra judicial killings chini ya baraka za serikali ? rejea watu kuokotwa kwenye viroba, Ben Saa 8, Azori & E.t.c ... Wezi wa kuku na viTVndio wanauwawa wa Matrillion wanasindikizwa na Escort hotelini
Mafisadi hayooo yanatanua tu! Washenzi wamekunja bilioni 345 kiulainii. Halafu wewe upo unakimbizana na TRA na kiduka chako cha mtaji wa milioni 5 ili watoto wako wale na kusoma. Hawa ndiyo wanakuja kujenga mahekalu ya kutisha na kucheka vijana kuwa siyo wabunifu na kwamba elimu yao haijawasaidia.

Kwenye hukumu hizi kuna ubaya gani kusema kuwa pesa zote zilizoibwa zirudishwe na kila walichonacho kinataifishwa?

Halafu yule mama masikini wakampiga mvua 22 kisa kakutwa na vipande 12 vya nyama ya swala eti nyara za taifa 😬😬😬😬

IMG-20231120-WA0020(1).jpg
 
Katika kipindi cha Mwezi mzima Kijana Ally Dangote amekuwa akitafutwa kwakutekeleza mauaji ya watu mbalimbali katika maeneo ya Longdong, Ungalimited na Sinoni

Kijana huyu alikuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi, majira ya Leo mchana wananchi wenye hasira kali wamemtia nguvuni na kumpokonya uhai.

Pia soma > Kibaka maarufu, Ally Dangote atiwa mbaroni Arusha

View attachment 2820024
Ally Dangote(Kulia)​
Alhamisi iliyopita nilipata taarifa kwa kijana wa Handeni kuwa Kuna mzee anakuja kumaliza kazi kwani nasikia dogo babu yake wa huko iringa alikuwa anamlinda kimazungara

Chezea Tanga wewe
 
Siku yake ilishafika na alikuwa anakitafuta kifo kwa kila namna ...

Kwa mujibu wa kituo cha Sunrise redio huyo Ally Dangote alikuwa anafanya mauaji na kisha kupotea na baada ya muda anarudi eneo lile lile alilofanya tukio ...

Jana inasemekana alikamatwa na kina mama na bahati ikawa upande wake akafanikiwa akaponyoka na baada ya muda akarudi tena eneo lile lile alilokoswa kukamatwa ..

Cha kushangaza Maeneo yale kuna kituo cha Polisi cha Unga Ltd lakini walishindwa kumdhibiti kwa wakati, hadi kufikia mahakama ya mtaa kutoa hukumu.

Apumzike anapostahili.
 
Back
Top Bottom