NAONESHA MSISITIZO [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
1.Ule ushahidi wa ugaidi wa Rwakatare uliosema unao na hata mbinguni uko tayari kuutoa ilikuwaje usiutoe hadi kufanya gaidi aendelee kutamba mitaani?
2.Tundu Lissu alishambuliwa wakati wa uongozi wako, lakini hadi unaondoka madarakani hakuna chochote cha maana kilichofanyika zaidi ya danadana za maneno toka kwako na Polisi uliokuwa unawaongoza?
3.Polisi wako wa Dodoma chini ya uongozi wako walisema wana video za tukio zima kupitia CCTV, lakini alivyoingia LUGOLA akasema eneo hilo la makazi ya viongozi hakukuwahi kuwapo na CCTV, nani mkweli kati yenu.
4.Wakati wa uongozi wako kuliasisiwa dhana ya "Wasiojulikana" ambao walitesa Watanzania wengi na wengine kuuawa na kuokotwa fukweni na mitoni wakiwa kwenye viroba, ulipoulizwa ukasema ni wageni lakini ulipobanwa ukakaa kimya, Leo unatwambia nini kuhusu maiti hizi na dhana ya wasiojulikana ambayo ni wazi kwako walijulikana na wanajulikana?
4.Ben Saanane na Azory Gwanda walipotea/walipotezwa wakati wa uongozi wako, na ulihusishwa na upoteaji wao, hebu Leo umejitokeza baada ya kupotea JF kwa muda, ni kwa vipi usihusishwe na upoteaji wao?
5.Uzalendo ni kuipenda nchi, na huwezi kuipenda nchi bila kuwapenda wananchi. Ni vipi uzalendo upimwe kwa kuvaa Scarf yenye rangi za bendera ya Taifa, huku ukifurahia kupotea kwa maisha ya wananchi?
6.Katiba yetu inasema nchi yetu inafuata Demokrasia ya vyama vingi, Je, katazo la mikutano ya kisiasa ulilolisimamia kwa nguvu zako zote linapata uhalali kupitia sheria ipi?