Anayejua Rais Samia anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

😞
 
Uvunjifu wa amani unaufanyaje ukiwa sebleni kwako au kwenye banda la mpira ukiwa unacheki game? Je, waliouliwa kwenye mazingira haya unawaelezeaje?
Hizo ni stray bullets, ni ajali kazini, lawama wapewe waliosababisha ambazo ni wahalifu!
Walikuwa wanatafuta Haki! Umemnyanganya shati lake, anakwambia nirudishie shati langu, unasema usivuruge Amani! Atatafita njia yoyote kupata haki yake.

Byeyombo...kelele
Kudai haki kuna njia zake, sio kufanya uhalifu
 
Sheria inasema hukumu yao kifo bila kufikishwa mahakamani?
Sijui akili zako uliacha wapi wakati unaaandika hayo.
Walipewa onyo hawalusikia, sheria pia haisemi ufanye uhalifu na ugaidi
 
Walipewa onyo hawalusikia, sheria pia haisemi ufanye uhalifu na ugaidi
Onyo haliwapi wauwaji uhalali wa kuuwa bila mtuhumiwa au mkosaji kufikishwa mahakamani na hukumu ya kifo kutolewa na mahakama.
 
AMRI ILITOLEWA NA ABDULI, SAMIA ANAMSIKILIZA ABDULI KWA CHOCHOTE ASEMACHO.
 
Serikali ipi wakati hakukuwa na Rais madarakani , unapindua mgombea wa urais?
 
Wewe unalpwa nini kutetea wauaji na mashetani hawa?
Shetani hata mimi na wewe tunaweza kugeuka tukawa wanyama.

Ule uhuni ungeachwa uendelee kwa siku moja tu nchi ingeingia kwenye machafuko makubwa sana.

Gharama za mapinduzi siku zote huja na mashujaa pamoja na wahanga.
 
Shetani hata mimi na wewe tunaweza kugeuka tukawa wanyama.

Ule uhuni ungeachwa uendelee kwa siku moja tu nchi ingeingia kwenye machafuko makubwa sana.

Gharama za mapinduzi siku zote huja na mashujaa pamoja na wahanga.
Wewe mnyarwanda usitete ujinga sisi ndugu zetu wameuwawa wakiwa majumbani wala hawakufika kwenye maeneo ya maandamano ninapoona mpuuzi kama wewe unatoa comment ya kijinga kama hii yako nakuweka kundi moja na wauji na kwa nyie wanyarwanda kuuana ni jadi yenu. Nina uhakika ungekuwa na ndugu ambaye ameuwawa na askari akiwa nyumbani kwake usingeandika huu upuuzi wako. Hivi shule ulienda kusomea upuuzi?
 
Wapo vijana walipigwa shaba mitaa ya Wazo Hill kosa lao walivunja na kuiba ile supermarket ya Shoppers iliyopo kushoto kwa Bagamoyo Road halafu wakakimbia ndani kwao kujificha, waliuliwa hapo hapo nyumbani kwao.

Yale yalikuwa machafuko sio vitu vya kuombea vitokee, yale ni maisha ya kawaida huko DRC huku kwetu tulijaribu kitu tusichokifahamu.
 
Hapa Mwanza maeneo ya Mjimwema watu walitolewa kwenye kibanda umiza wakiangalia mpira wakaamriwa kulala chini wakapigwa risasi za vichwa watu 12 wengine wakiwa vijana under 15yrs na matukio ya hivyo ni mengi mbona huzungumzii scenario kama hizi unazungumzia tu watu waliouwawa kwenye vurugu? Au hukumbuki hata bibi wa miaka 75 aliyepigwa risasi kule Magomeni akiwa sebuleni kwake ambaye stori yake ilipelekea Tume ya Chande kuzuia watu wasitoe maelezo mbele ya vyombo vya habari. Unapotetea mauaji haya jaribu kuwa na ubinadamu na kuacha kutawaliwa na uchawa kwa muuaji Samia.
 
Pointi ya msingi ni ukweli kwamba walioanzisha zile vurugu hawakujua madhara yake yatakuwa vipi.

Ukisema watu waliuwawa bila hatia, unakuja ukweli kwamba tarehe 9 na 25 Desemba hakuandamana mtu hata mmoja na hakupigwa risasi mtu yoyote yule.

Ile siku ilikuwa mbaya sana imetia doa historia ya Tanzania. Yale mateso waliyopata wasio na hatia yoyote ndio maisha ya kawaida huko DRC na Somalia.

Kukinukisha balaa lake linawatesa wasio na hatia. Huwezi kuitoa dola madarakani kwa kutumia siasa za vurugu.
 
Kinachoniumiza ni kimoja tu'

Ni kwanini baadhi yao walifutwa nyumbani? Kama inavyosemwa?

Hii inaumiza sana'

Ila hakuna nafsi itakayo kwepa udongo siku moja 🌍🥲
Hii kauli tumeikataa wote wenye akili! Mbona wewe hukufuatwa uvunguni ulipojificha
 
Kimsingi machafuko hayakuwepo ila uchu wa madaraka ndio ulipelekea mass killings.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…