Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

🙄🙄🙄🙄 mkate tu ndio akili itamkaa sawa labda
 
KUna dalili kwamba watu wametiwa kibano na maisha. Wako hoi kiasi kwamba sasa wana matumaini na kila jambo, hata kama ni la ujinga tu! Mtu gani anayekubaliana na rais kila jambo? hawa wote wanaomsifia Samia ni bure tu! Hawajui hata nini kizuri au kibaya anachofanya. Wao wapo wapo tu!
 
Hujui uongealo. Urais ni muendelezo, kuboresha dosari na kusonga mbele, iko hivyo leo na itakua hivyo kila wakati. Na kwa wenzetu wana kitu kinaitwa National Policy ambayo hufuatwa na Rais yeyote anayeingia madarakani. Ndiyo maana alivyoingia Obama alimtafuta Osama kama ilivyokua kwa watangulizi wake. Lakini kama sera au jambo ni bovu, ni sahihi kufuta na kutupilia mbali. Kwa mfano kama kuna uonevu katika kuwapa watu kesi zisizotekelezeka au za kubambikia watu, ni haki kwa Rais makini kuwaambia wasaidizi wake wajiridhishe na kama zilionea watu, kufuta kabisa.
Mama yuko sahihi kwa 100%.
 
Uzaifu MUNGINE hakai kabisa makao makuu ya nchi akikaa Sana siku tatu anarudi baharini kupunga kaupepo wakati mwendazake alikuwa anakaa mwenzi mzima anaotea jua juu ya mawe huyu amezoea UPEPO kuangalia mijusi ikikimbizana juu ya mawe hataki
Wewe hamnazo jiwe ni jiwe na mama ni mama kwahyo unataka Samia naye akalale kwenye yale mawe ya dodoma na lile jua Kali hivo
 
Dah Yani unaumia mtu kusifiwa, hamnaga Rais anayetoa vitu vya burebure mfuko, Raisi huweka mazingira wezeshi na Rahisi kwa Raia. So msiumie kusifiwa akikosea tu ataambiwa
 
Mama yetu ye ni kuomba tu, jamani naomba, ndugu zangu niwaombeni....
... ombi la mkuu wa nchi ni agizo; don't misinterpret! Mjinga ndiye ataona ameombwa kumbe ameelekezwa. Na asiyeweza kutofautisha "ombi la Rais" na maombi mengine hastahili kukalia ofisi ya umma. Yesu Kristo alipowatawadha miguu wale 12 unadhani alionekana dhalili? Alitisha! Wenye akili walitafutana mle!

Kiongozi bora huongoza kwa mifano na lugha rahisi kueleweka na isiyokera. Kupigapiga makelele kutisha unaowaongoza ni dalili za kiongozi mjinga.
 
Mm naona kila ishara ya maendeleo ktk uchemi wetu ...cha muhimu ni kudhibiti tu mijitu inayo kula rushwa
 
Kama vipi mfuate unayemkubali huko aliko. Unafanya nini hapa wakati unayemkubali na aliyewadekeza kwa ujinga hayupo. Mfuate mwendazake huko aliko. Hivi kwanini mlikuwa mnafurahia kupigwa risasi kwa binadamu wenzenu? Wewe ni mtu gani unafurahia binadamu mwenzako anasokomezwa kwenye viroba akiwa marehemu? kwanini hamna huruma nyie wafuasi wa mwendazake? Hivi hamjifunzi tu kwa kifo chake kama cha paka mwizi tu?
 
Mama yetu ye ni kuomba tu, jamani naomba, ndugu zangu niwaombeni....
Huko kunaitwa ni kuongoza watu,na siyo kutawala,to remind and ask us how we came from bad to worse under Magufuli regime is to ignore from which way we came,,instead we should focus on celebrating mama samia's styles,we should celebrate it's tenacity,we should celebrate her will of healing the wounds and making this mama Tanzania great again...
 

Kwa mantiki ya hoja yako, hii mada haina maana. Kama tunatakiwa kujiamini sisi wenyewe basi hakuna haja ya kupoteza muda kujadili udhaifu wa Samia au kumlinganisha na Magufuli. Wote hawana maana kwetu.
 
Mama yupo powa ila haya makongamano tunarudi zile enzi..
Ilitosha siku 100 bila makongamano haya kila mkoa
 
Robinson hakuna udhaifu wowote ,kumbuka Hayati JPM alimuamini mama hata akampendekeza yeye kuwa mgombea mwenza mara mbili,wacha mama yetu apige kazi!!!
 
Tunajua
Unajua Mwendazake alituachia roho ya kuchukiana, ubabe, na chuki.. Ndio maana mama akijaribu kurekebisha kasoro.. Wafiwa wa Chato wanapagawa
Tunajua mnataka ahalibikiwe ili 025 muanze kumdhalilisha na kutukana chama.
 
Mkuu upo? Habar za siku mingi, bado uko Korosho Region na au Gas City?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…