Kwanza, Rais amekuwa ni mtu anayehariri maamuzi ya mtangulizi wake badala ya kuanzisha mema yake. Katika hali hiyo anashangiliwa kwa kuamini kwamba anapambana na maamuzi ya JPM aliyoyafanya. Ni siku 100 hatujasikia muelekeo wake wa uchumi mbali na kukamilisha waliyoanzisha na JPM na yeye kufufua yaliyokataliwa; Bagamoyo.
Pili ni tabia ya kutaka kumfurahisha kila anayekutana naye. Anakutana na akina mama, anatoa ahadi na kukubaliana nao kila kitu. Anakutana na vijana anatoa ahadi na kukubaliana nao kila kitu. Anakutana na wafanyabiashara, anatoa ahadi na kukubaliana nao kila kitu. anakutana na mwekezaji wa kulima kutoka Malaysia anatoa ahadi.
Unawezaje kukubaliana na kila ombi la wafanyabiashara, utadhani ndo wanaounda serikali? Yaani kwamba serikali haina maoni yake juu ya hayo wanayoyaita ni matatizo ya kibiashara? Rais anataka atunge sheria za kodi kwa kushirikiana na wafanyabiashara kweli?
Nchi inahitaji uongozi. Wanawake waongozwe, vijana waongozwe, wafanyabiashara waongozwe. Wengi hawajielewi zaidi ya familia zao na miradi yao.