Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Ndugu naomba ujue kuwa !JPM KISHA KUFA HATORUDI!KUBALIANA NA UKWELI UPONE ROHO NA NAFSI!!MUUNGE MKONO MAMA MBONA JPM NA UKATILI WAKE WOOTE ULIMUUNGA MKONO IWEJE MAMA MPOLE UNASHINDWA?????!!!!WEWE VP WEWE?UNA MATATIZO GANI WEWE???!!!!NTAKUKATA KIBAO WEWE!!!ACHA WENGE!!!!
🙄🙄🙄🙄 mkate tu ndio akili itamkaa sawa labda
 
Taaluma yangu ni ualimu. Tumefundishwa saikolojia na tunaitumia kufundisha. Nawaona mukiwa watu muliofeli maisha kabla ya JPM. kila kiongozi munampa matumaini yenu, mukiamini mambo yatakuwa mazuri. Nawaona kichwani mukiamini Samia iko siku ataachia pesa ziingie mifukoni mwenu. Nawaona ni watu ambao kila jambo ni kwa sababu ya mwingine na ni mwingine atakayewapa maisha mazuri.

Mawazo hayo na tabia hizo hata Wamarekani walikuwa nazo wakati wanamchagua Trump. Waliamini atawasaidia kuwa matajili. Eleweni hivi, binadamu huwa ana tabia ya kujiamini yeye na siyo kumuamini mwingine. Kama ninyi ni watu wazima na imani yenu kwa 100% iko kwa Samia, basi kuna shida vichwani.

Nawaomba musichukie ukweli huu. kila mmoja wenu atafakali kimya kimya kwa nini yuko hivyo?
KUna dalili kwamba watu wametiwa kibano na maisha. Wako hoi kiasi kwamba sasa wana matumaini na kila jambo, hata kama ni la ujinga tu! Mtu gani anayekubaliana na rais kila jambo? hawa wote wanaomsifia Samia ni bure tu! Hawajui hata nini kizuri au kibaya anachofanya. Wao wapo wapo tu!
 
Kwanza, Rais amekuwa ni mtu anayehariri maamuzi ya mtangulizi wake badala ya kuanzisha mema yake. Katika hali hiyo anashangiliwa kwa kuamini kwamba anapambana na maamuzi ya JPM aliyoyafanya. Ni siku 100 hatujasikia muelekeo wake wa uchumi mbali na kukamilisha waliyoanzisha na JPM na yeye kufufua yaliyokataliwa; Bagamoyo.

Pili ni tabia ya kutaka kumfurahisha kila anayekutana naye. Anakutana na akina mama, anatoa ahadi na kukubaliana nao kila kitu. Anakutana na vijana anatoa ahadi na kukubaliana nao kila kitu. Anakutana na wafanyabiashara, anatoa ahadi na kukubaliana nao kila kitu. anakutana na mwekezaji wa kulima kutoka Malaysia anatoa ahadi.

Unawezaje kukubaliana na kila ombi la wafanyabiashara, utadhani ndo wanaounda serikali? Yaani kwamba serikali haina maoni yake juu ya hayo wanayoyaita ni matatizo ya kibiashara? Rais anataka atunge sheria za kodi kwa kushirikiana na wafanyabiashara kweli?

Nchi inahitaji uongozi. Wanawake waongozwe, vijana waongozwe, wafanyabiashara waongozwe. Wengi hawajielewi zaidi ya familia zao na miradi yao.
Hujui uongealo. Urais ni muendelezo, kuboresha dosari na kusonga mbele, iko hivyo leo na itakua hivyo kila wakati. Na kwa wenzetu wana kitu kinaitwa National Policy ambayo hufuatwa na Rais yeyote anayeingia madarakani. Ndiyo maana alivyoingia Obama alimtafuta Osama kama ilivyokua kwa watangulizi wake. Lakini kama sera au jambo ni bovu, ni sahihi kufuta na kutupilia mbali. Kwa mfano kama kuna uonevu katika kuwapa watu kesi zisizotekelezeka au za kubambikia watu, ni haki kwa Rais makini kuwaambia wasaidizi wake wajiridhishe na kama zilionea watu, kufuta kabisa.
Mama yuko sahihi kwa 100%.
 
Uzaifu MUNGINE hakai kabisa makao makuu ya nchi akikaa Sana siku tatu anarudi baharini kupunga kaupepo wakati mwendazake alikuwa anakaa mwenzi mzima anaotea jua juu ya mawe huyu amezoea UPEPO kuangalia mijusi ikikimbizana juu ya mawe hataki
Wewe hamnazo jiwe ni jiwe na mama ni mama kwahyo unataka Samia naye akalale kwenye yale mawe ya dodoma na lile jua Kali hivo
 
KUna dalili kwamba watu wametiwa kibano na maisha. Wako hoi kiasi kwamba sasa wana matumaini na kila jambo, hata kama ni la ujinga tu! Mtu gani anayekubaliana na rais kila jambo? hawa wote wanaomsifia Samia ni bure tu! Hawajui hata nini kizuri au kibaya anachofanya. Wao wapo wapo tu!
Dah Yani unaumia mtu kusifiwa, hamnaga Rais anayetoa vitu vya burebure mfuko, Raisi huweka mazingira wezeshi na Rahisi kwa Raia. So msiumie kusifiwa akikosea tu ataambiwa
 
Mama yetu ye ni kuomba tu, jamani naomba, ndugu zangu niwaombeni....
... ombi la mkuu wa nchi ni agizo; don't misinterpret! Mjinga ndiye ataona ameombwa kumbe ameelekezwa. Na asiyeweza kutofautisha "ombi la Rais" na maombi mengine hastahili kukalia ofisi ya umma. Yesu Kristo alipowatawadha miguu wale 12 unadhani alionekana dhalili? Alitisha! Wenye akili walitafutana mle!

Kiongozi bora huongoza kwa mifano na lugha rahisi kueleweka na isiyokera. Kupigapiga makelele kutisha unaowaongoza ni dalili za kiongozi mjinga.
 
Mm naona kila ishara ya maendeleo ktk uchemi wetu ...cha muhimu ni kudhibiti tu mijitu inayo kula rushwa
 
Kwanza, Rais amekuwa ni mtu anayehariri maamuzi ya mtangulizi wake badala ya kuanzisha mema yake. Katika hali hiyo anashangiliwa kwa kuamini kwamba anapambana na maamuzi ya JPM aliyoyafanya. Ni siku 100 hatujasikia muelekeo wake wa uchumi mbali na kukamilisha waliyoanzisha na JPM na yeye kufufua yaliyokataliwa; Bagamoyo.

Pili ni tabia ya kutaka kumfurahisha kila anayekutana naye. Anakutana na akina mama, anatoa ahadi na kukubaliana nao kila kitu. Anakutana na vijana anatoa ahadi na kukubaliana nao kila kitu. Anakutana na wafanyabiashara, anatoa ahadi na kukubaliana nao kila kitu. anakutana na mwekezaji wa kulima kutoka Malaysia anatoa ahadi.

Unawezaje kukubaliana na kila ombi la wafanyabiashara, utadhani ndo wanaounda serikali? Yaani kwamba serikali haina maoni yake juu ya hayo wanayoyaita ni matatizo ya kibiashara? Rais anataka atunge sheria za kodi kwa kushirikiana na wafanyabiashara kweli?

Nchi inahitaji uongozi. Wanawake waongozwe, vijana waongozwe, wafanyabiashara waongozwe. Wengi hawajielewi zaidi ya familia zao na miradi yao.
Kama vipi mfuate unayemkubali huko aliko. Unafanya nini hapa wakati unayemkubali na aliyewadekeza kwa ujinga hayupo. Mfuate mwendazake huko aliko. Hivi kwanini mlikuwa mnafurahia kupigwa risasi kwa binadamu wenzenu? Wewe ni mtu gani unafurahia binadamu mwenzako anasokomezwa kwenye viroba akiwa marehemu? kwanini hamna huruma nyie wafuasi wa mwendazake? Hivi hamjifunzi tu kwa kifo chake kama cha paka mwizi tu?
 
Mama yetu ye ni kuomba tu, jamani naomba, ndugu zangu niwaombeni....
Huko kunaitwa ni kuongoza watu,na siyo kutawala,to remind and ask us how we came from bad to worse under Magufuli regime is to ignore from which way we came,,instead we should focus on celebrating mama samia's styles,we should celebrate it's tenacity,we should celebrate her will of healing the wounds and making this mama Tanzania great again...
 
Taaluma yangu ni ualimu. Tumefundishwa saikolojia na tunaitumia kufundisha. Nawaona mukiwa watu muliofeli maisha kabla ya JPM. kila kiongozi munampa matumaini yenu, mukiamini mambo yatakuwa mazuri. Nawaona kichwani mukiamini Samia iko siku ataachia pesa ziingie mifukoni mwenu. Nawaona ni watu ambao kila jambo ni kwa sababu ya mwingine na ni mwingine atakayewapa maisha mazuri.

Mawazo hayo na tabia hizo hata Wamarekani walikuwa nazo wakati wanamchagua Trump. Waliamini atawasaidia kuwa matajili. Eleweni hivi, binadamu huwa ana tabia ya kujiamini yeye na siyo kumuamini mwingine. Kama ninyi ni watu wazima na imani yenu kwa 100% iko kwa Samia, basi kuna shida vichwani.

Nawaomba musichukie ukweli huu. kila mmoja wenu atafakali kimya kimya kwa nini yuko hivyo?

Kwa mantiki ya hoja yako, hii mada haina maana. Kama tunatakiwa kujiamini sisi wenyewe basi hakuna haja ya kupoteza muda kujadili udhaifu wa Samia au kumlinganisha na Magufuli. Wote hawana maana kwetu.
 
Mama yupo powa ila haya makongamano tunarudi zile enzi..
Ilitosha siku 100 bila makongamano haya kila mkoa
 
Robinson hakuna udhaifu wowote ,kumbuka Hayati JPM alimuamini mama hata akampendekeza yeye kuwa mgombea mwenza mara mbili,wacha mama yetu apige kazi!!!
 
Tunajua
Unajua Mwendazake alituachia roho ya kuchukiana, ubabe, na chuki.. Ndio maana mama akijaribu kurekebisha kasoro.. Wafiwa wa Chato wanapagawa
Tunajua mnataka ahalibikiwe ili 025 muanze kumdhalilisha na kutukana chama.
 
Huko kunaitwa ni kuongoza watu,na siyo kutawala,to remind and ask us how we came from bad to worse under Magufuli regime is to ignore from which way we came,,instead we should focus on celebrating mama samia's styles,we should celebrate it's tenacity,we should celebrate her will of healing the wounds and making this mama Tanzania great again...
Mkuu upo? Habar za siku mingi, bado uko Korosho Region na au Gas City?
 
Back
Top Bottom