Ameingizwa kingi sana. It's either uwezo wake wa kufikiri ni mdogo sana au kuna watu anaowaamini sana lakini wanamharibia makusudi. Kwa jinsi alivyoungwa mkono siku chache za mwanzo alitakiwa ashikilie hapohapo. Aliungwa mkono na wasomi wote, viongozi wote wa dini, wananchi wa kawaida, wafanyabiashara, wawekezaji, nchi wahisani, vyama vyote vya siasa bila kujali itikadi zao, vyombo vya habari, wanaharakati etc.
Alitakiwa ashikilie hapohapo ili aendelee kuungwa mkono zaidi and im sure 2025 kazi yake ingekua rahisi sana. Lakini "wajuba" wakamsoma halafu wakamuingiza kingi, nae bila kutafakari akaingia kichwakichwa. Sasa kajiharibia kote. Hakuna anayemuelewa kwa sasa. Sio viongozi wa dini, sio wanahabari, sio wafanyaniashara, sio wananchi wa kawaida wanaolipa tozo, sio wawekezaji. Kila mmoja anamuona hopeless tu.
Hata akiongea kitu saivi hakipewi uzito tena. Wanampuuza ndani na nje ya chama chake. Bora aongee Manara habari yake itapewa kipaumbele sio ya Jumong. Umaarufu wake umeshuka sana. Zile siku chache za mwanzo ukisikia sauti yake tu unaacha kila kitu kumsikiliza, lakini kwa sasa hakuna mwenye muda wa kumsikiliza. Jana mzee mmoja kamuona kwenye TV akasema "Badilisha chanel,weka hata ya Somalia" 🤣🤣
Mbaya zaidi hata waliomuingiza kingi nao wamemgeuka. Angalia huko ndani ya chama chake, kila siku wanatoa matamko ya kuwatishia wanachama wenzao wanaomkosoa Jumong. Kwa kifupi haeleweki ndani ya chama chake, wala nje ya chama. Amevurugwa akavurugika. Poor her. Sijui kama 2025 atatoboa. Ama kweli mafanikio yana baba wengi, lakini matatizo ni mtoto yatima.!
Credit: Malisa
Nami naungana na wasomi. Nimemsikiliza akihojiwa BBC anajibu maswali juu juu sana. Kama mwenyekiti wa chama wanachama wamemzidi ujanja. Gwajima anatomasa kiti, Polepole anapapasa mgongo wa kiti.