Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.
MATAGA wafa kifo cha MENDE
 
Huna akil ww
 
Kwahivyo mnataka ajenge maviwanja na mahospitali ya rufaa ya chato nk? Hata reli kwenda mwanza ililazimishwa na mwenda silazima tunaeza amua iishie dom kwanza! Daraja la busisi nalo tupime haikuwa kipaumbele cha taifa bali cha mwenda na wakweze! Mbona mwenda alikataa kujenga bandari bagamoyo toka kwa Jakaya! Mbona alikataa katiba kitu muhimu na kilichokwisha tafuna kodizetu!!
Mama abidue mamiahadi na mamipango ya hovyo yamaujenzi isiyo na maana aliyoamua mwenda haiwezekani nchi inajengwa Dodoma na Chato na Mwanza tuu huku watu wanateseka makodi,mishahara finyu,hakuna madaraja wala increments,ajira hakuna,account zao kuvamiwa kisa maujenzi ujenzi tuu!!
Upuuzi huo msahau ninyi mlokuwa mnafaidika na mwenda tena msahau jumla maana hatutawapa tena nchi mlotuonesha waziwazi yametosha!!!
 
Yaani ulitegemea Samia awe Magufuli? Hata Jinsia tu ni tofauti, lakini hata wangekuwa Jinsia moja kama Kigwangala mambo yanhebadilika. Kiufupi hakuna anayeweza kuwa exactly kama mwingine. Hata wewe na yule hamfanani. Kikubwa zaidi ni kwamba kama Samia anataka kufaulu LAZIMA AWE RAIS. Kulazimisha awe Magufuli ni kujidanganya na atafeli vibaya. Tatizo lenu Wafaidika wa SERA ZA KIKATILI za Magufuli mlitegemea eti SAMIA atafanya kila kitu kama Magufuli, awe katili kama Magufuli, aruhusu mauaji kama Magufuli, atukane watu hadharani kama Magufuli, adhalilishe watu kwenye majukwaa kama Magufuli, aite Wewekezaji wezi kama Magufuli. Huyu ni Samia, na binadamu mwenye busara akipewa nafasi ya mwingine lazima aangalie madhaifu ya mtangulizi na kuyarekebisha au kuyatupilia mbali kabisa ili jamii imuelewe. Mliokuwa mnaregemea kumuona Magufuli exactly ndani ya Samia jifungieni ndani maana hamtamuona tena.
 
Aliekwambia uchumi unajengwa kwa watu kuajiriwa? Nitajie nchi ambayo wananchi wake wote wana ajira unasema ameua sector binafsi leta mifano si kusema tu .Nitajie sector binafsi ambayo inafanya shuguli zake Tanzania imekimbia waliokimbia ni wakwepa kodi na makampuni ya kitapeli lakini kama ulikuwa unafanya shuguli zako vzr huwezi kuondoka kwani sheria ni zile zile

Mbona hatukuona makampuni ya madini yakikimbia tena yenyewe ndo yalikuwa yanatuibia kwelikweli .Mbona hatujaona sigara,makampuni ya simu ,makampuni ya vinywaji yakikimbia acheni mambo yenu bhana rudini mmeambiwa rudini milango ipo wazi njoeni mwenye shamba hayupo .
Acha nikushauri tu kama upo Dar ( ingawa Kwa akili zako najua hata Dar utakuwa hujawai kufika) basi nikushauri nenda Dar alafu panda gari ya Gongo la mboto kutokea Posta.

Then tembelea Shopping Malls za Mkuki Tower, Quality Centre na Quality Plaza uone biashara ngapi zimefungwa kwenye hizo shopping malls 3 tu??? Pia jaribu kuulizia tu ni watanzania wangapi walikuwa wameajiriwa kwenye hizo shopping malls tu??? Then Njoo humu uongee huo utumbo wako!!!

Kama una akili pia ulizia hali kiwanda cha dangote ikoje??? Kiwanda cha Rhino cement kiliishia wapi???

Kama ajira sio uchumi basi uchumi ni nini??? Huko kukopa hela kuliko maraisi wote kwa miaka 5 tu na kwenda kutumia hizo hela kujenga chato alikofanya huyo mpuuzi wenu magufuli ndo uchumi???? Huna akili wewe!!
 
Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.
Wewe ni msukuma?

Tuanzie hapo kwanza
 
Anatupeleka kwenye :-
1. UHURU NA HAKI
2.Uwekezaji-utakaoleta ajira na kodi.
3. Weledi
4. Umoja na mshikamano wa kitaifa.
 
Wabongo tuna shida sana, ndio maana Mkapa alikuwa anasema we are too lazy.

Mimi nilitegemea analysis ya maneno na matendo yake ya wiki hizi mbili badala yake hizi porojo. Tuambie kupitia kitendo A, B na C au kauli 1, 2 na 3 naamini tunapotea. Kauli zake zote ni ukweli mtupu. Na kama ukweli ukisemwa unaenda kutupoteza, basi tuna matatizo makubwa sana.
 
Ndio tunachotaka atekeleze miradi tutampa kura tofauti na hapo tutamfurusha yeye na CCM yake
Toka lini kura yako na mjomba wako ikawa na nguvu? Acha kujidanganya, pia mwache mama afanye usafi, Nchi ilichafuka sana, kama kubambikia kodi na kuingilia akaunti za wafanyabiashara we unaona poa, sisi hatukubaliani na unyang'anyi huo, bora mapato yapungue kuliko dhuluma kwenye kodi!
 
Mmeanza [emoji15] hivi inamaana hayati ndo alikua correct? Yaan nyie [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Watanzania tuwe wazarendo, wasio wazarendo vyombo vya dolla mpo, TCRA ipo washughulikieni! mkuu wa Mkoa upo, Mkuu wa Wilaya upo. Wawekeni watu rock up!

Nimeshagiza midege mikubwa 2 zitaingia mwezi ujao

Wapinzani wameungana na mabeberu wametuibia sana, sasa ni zamu ya wanyonge

Nimejisakrifaisi kwa ajili ya wanyonge! Mtanikumbuka!

Mkurugenzi nimekuteua mimi, mshahala nakulipa mimi, sasa ole wako umpitishe mpinzani

Kuhusu zao la korosho, ole wako uandamane, nitawapiga na shangazi zenu.
 
Cha msingi ni kujua destination, lakini suala la njia sio muhimu sana. Ukipanda ndege ndio utaelewa zaidi.
 
Back
Top Bottom