Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.
CCM mnahaha sana. Naona mlizoea vya kunyonga kwa miaka mitano sasa vya kuchinja vinawasumbua[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Ultimately, time will tell!

Ukweli ni kwamba kiongozi anayeweza kusimamia maono yake haogopi kufanya (na kusimamia) unpopular decisions. Kiongozi ukitaka kumfurahisha kila mtu, acha kazi ya uongozi na badala yake kauze ice cream!

Ingawa bado ni mapema kusema chochote, sijaona dalili za toughness inayohitajika kutekeleza ile miradi mikubwa ya kimkakati aliyoirithi. Rai yangu ni kwamba tumuungeni mkono ili kama ni kushindwa ashindwe sio kwa sababu sisi ndiyo tumemfanya ashindwe.
 
[emoji1666][emoji106][emoji120][emoji3578]
FB_IMG_16172183787161027.jpeg
 
We mtu mbona umemsakama mama una ugomvi nae?
 
Siku mbili hizi ushaanza kuona kuwa unapotea! au umekula nauli?

Nani alikudanganya kuwa awamu ya jiwe ilikuwa inatekeleza yale yaliyokuwa kwenye kurasa 300? Wapi ilani ilisema Rais akifika sehemu atoe maburungutu ya pesa hapo hapo?

Mwacheni Rais Samia afanye kazi enyi wachumia tumbo, matumbo yenu hayajai tu?
 
Mnataka mpotee mara ngapi? Hata hivyo, hana cha kupoteza kwani mliyempa kura keshajiondokea. Muombe Mungu ifike 2025.
 
Mama kaanza vizuri sana, usipomkubali kwa hizi hatua alizoanza nazo utakuwa na tatizo bila shaka.Alichonikosha zaidi ni namna alivyowaelekeza viongozi kutumia akili zaidi katika kuongoza wananchi badala ya ubabe,ni jambo jema.Kikubwa sisi kama wananchi tumsupport na tusisite kutoa maoni ya kujenga na siyo kutukana na kejeli, nina imani Tanzania itapiga hatua kubwa kimaendeleo.
 
Siku mama yenu akiwaambia ata kwa goli la mkono atashinda ndiyo hamtaamini[emoji124][emoji124]
 
Wale tuliokua tunawaita nyumbu naona sasa ndo wako na mama. Maneno yao ya kejeli na ushabiki tu. Kinachonisikitisha hakuna chama cha upinzani serious ila kama kitakuja kuwepo ntakupigia kura za hasiraaaa
Hahahaaha Mataga umechanganyikiwa na kupaniki,kweli mpira pasi aiseee.
 
Ndio tunachotaka atekeleze miradi tutampa kura tofauti na hapo tutamfurusha yeye na CCM yake
Naona wewe unavurugwa akili na jambo moja tu: "MIRADI".

Hivi uongozi ni kutekeleza miradi peke yake?

Mimi pia, kama wewe vile, nimeanza kuingiwa na mashaka juu yake, lakini wasiwasi wangu sio juu ya utekelezaji wa hiyo miradi pekee.

Kuna mambo ambayo amejaribu kuyazungumzia kwa juujuu yanayonitia wasiwasi mkubwa ju yake.

Lakini nitavuta subira nine mwelekeo wake hasa unaenda vipi.

Akiamua moja kwa moja kurudi kule kwa Kikwete, atanishangaza sana.
 
ANATUPELEKA MASIKINI KUBAK NA UPUUZI WAO WA AWAMU YA 5, NA SISI WENYE UWEZO KURUDI KUISHI KAMA MALAIKA...
 
Kipindi cha Yesu Masihi wa Bwana
Wayahudi walimpinga sana wakisema Kristo hatoki katika uko wa Daudi

Labda nikutoe wasiwasi SSH aliyekuwepo ndani ya CCM ni mpango wa Mungu hata kama wanadamu wamehusika na mbinu chafu kutimiza azma zao

Mungu halali wala hasinzii kwa ajili ya Taifa lake mkuu.pia yeye ndio mwenye maamuzi yote
 
Back
Top Bottom