Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

we kila siku thread mpya kumnanga rais kwan una shida gani?
 
Tena mafisadi wamejipanga kweli kweli. Asipojitoa maisha yake kama sadaka kwa watanzania ataishia kuwapigia magoti kama JK alivyowahi tudanganya eti mafisadi ukiwagusa nchi inaweza ikayumba hahahahah, ila mwamba Dkt Magufuli aliwashughulikia na nchi ilikuwa shwariiii
 
Kwani ufisadi Tz hii ulishawahi kuisha?alichokuwa anakifanya jiwe, ni kuuziba tu ili usijulikane kwa wananchi, lakini mama samia akiamua kufukua makabuli kwa kipindi cha miaka 5 nyuma ifanyike special audit!!watu tutazimia!!ki fupi CCM, na ufisadi ni samako na maji.
 
Basi huyu nae auzibe ili twende bila kuuona
 
Basi huyu nae auzibe ili twende bila kuuona
Haina haja ya kuuziba, na ndio maana unaonekana kuwa ni mkubwa, na hana uwezo wa kuuzuia, kwani hata awaondoe wote wanaomzunguka kwa sasa, hata timu yake iliyoko nje ni wale wale tu!!sasa wale wafuasi wa mwendazake ndio wanapiga kelele ohooo ufisadi, ufisadi, utadhania ulikuwa haupo!!
 
unazinguliwa na nani nchi iliishapotea hatua tuendako bali tunajua tulikotoka tu.hakuna kinachogusika ,mafuta juu,nyama juu,mahindi juu,samaki juu kila kitu kiko juu.matozo kibao na wapigaji wamerudishwa tena serikalini ni shida tupu.
 
A
AKiwaondoa wote ataweka nani kama yeye mwenyewe anaweka wale ambao walishahalibu na kuachwa ndo anawaona super?

Watu wanaomfulahia ni wale waliokuwa wanaiba na kuzibiwa njia na ndo anawarudisha kwenye usaidizi sasa analalamika nini?

Kwani tanzania ni hao tu mdo wasomi na hakuna wapya ambao wanaweza kumsaidia?

Kuna watu walimchukia maguful na bado wakawa kwenye nafasi kama watendaji ingawa tabia zilibadilika kwa kubanwa
na wakawa wanamtukama magufuli kupitia miatandao na majina feki sasa ndo wanamshangilia mama huku wanamuibia na kujifanya wanamshambulia hayati magufuli.

Ni wajibu wake kuaondoa hao wanafiki na sio kulia lia maana anaowapenda ndo wanawaza jinsi ya kumchotea mali za nchi.
 
Hii ni taarifa au michambo ama mengineyo..? Hapo bado sijagusia lugha..(masakitiko!!)🤣
 
Keyboard warriors kama wewe unakuta hata kuongoza tu familia yako imekushinda
 
Rais Samia ameshindwa kuendeleza miradi ya kimkakakati kama ujenzi wa reli,bwawa la mwalimu Nyerere.Siku hizi nidhamu makazini zimeshuka watu hawafanyi kazi vizuri kama enzi za Rais Magufuli,Siku hizi umeme unakatika ovyo na ufisadi umerudi tena wanawekana kwenye nyazifa ambazo ni muhimu.Pia ninaongea na watu wengi wa kawaida hawana Imani na Rais huyu.Mimi Kwa maoni yangu huyu Rais hafai kuongoza hii nchi mwisho wake uwe 2025.Kwa maslahi Mazima ya nchi hii tutafute Rais mwingine mwaka 2025 ambaye anauwezo wa kusimamia miradi ya maendeleo Kwa ustadi mkubwa na kudumisha utawala Bora na demokrasia.huyu Rais ameshaonesha kuwa ni dhaifu, kuwavutia wawekezaji haitoshi iwapo umeshindwa kuwawekea mazingira mazuri Kwa mfano upatikanaji wa nishati ya uhakika,uendelezaji wa reli kama njia muhimu ya usafirishaji wa bidhaa.
 
Ngoja tuone amalize mwaka hadi julqi atakapokamilisha budget yake..Lakini kwa kweli ameshindwa kujigawanya mfano kupqmbanq na upqnadaji bei wa vitu ovyovyo,,magufuti alikataa hili..
 
Ukigombea tu utatosha au hata kugombea hautoshi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…