Baadhi ya kauli ambazo tumezisikia kutoka kwa Mama Samia na viongozi wengine fulani waliohudumu chini ya JPM zinaonesha kwamba hao viongozi walikuwa wanahubiri na kusimamia wasichokiamini. Kitendo hicho cha kuhubiri na kusimamia wasichokiamini kilikuwa unafiki na utovu mkubwa wa nidhamu kwa wapigakura wa nchi hii. Hili limenikumbusha hata ule utovu wa nidhamu ambao VP na PM waliuonesha wiki nne zilizopita kwa kuwapa wapigakura salaam hewa kutoka kwa Hayati JPM ilhali wakijua JPM alikuwa mahututi ndani ya ICU.
Katika utumishi, sio kitu cha ajabu kuwa na tofauti za kimtazamo juu ya jambo fulani. Hata hivyo, inapotokea kwamba VP au waziri anaamini tofauti za kimtazamo zilizopo kati yake na Rais, juu ya jambo hilo, ni kubwa sana na hazivumiliki endapo Rais atakataa ushauri wake, basi ni bora akajitenga na msimamo wa Rais kwa kujiuzulu.
VP au Waziri akishindwa kujitenga na kitu ambacho anaamini kinaumiza maslahi ya taifa, VP au waziri huyo anakuwa ameonesha udhaifu mkubwa sana wa kiuongozi. Kiongozi lazima awe na ujasiri wa kusimama upande wa haki hata kama kufanya hivyo maana yake ni kupoteza kazi. Vinginevyo, huyo hafai kabisa kushika dhamana kubwa kama hiyo.
Needless to say, VP au Waziri anayehubiri na kusimamia asichokiamini hawezi hata kuweka kiasi sahihi cha juhudi inayohitajika kufikia malengo yaliyotarajiwa. Kwa maneno mengine, yeye anageuka kuwa VP au waziri mzigo.
Mama Samia ameonesha udhaifu wa kiwango cha PhD na amekuwa mfano mbaya kabisa kwa mawaziri wake. Bila shaka, Rais anawaambia mawaziri na taifa zima kwamba unafiki katika Serikali unakubalika. Yumukini mfano wa unafiki aliouonesha ni silaha ambayo wateule wake hawatasita kuitumia dhidi yake. Inasikitisha, to say the least!