Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Mfikishieni taarifa huyo mama yenu kuwa tozo ndo inaenda kuwa anguko lake la milele hakuna atakayekubali kumpa kura yake au kumuunga mkono labda huyo mtu awe kichaa au ukiute hayapo tayari


Sikuwahi kuwaza yupo hivi, ni Rais asiyesikia anayeongozwa ongozwa tu ambaye haeleweki

Anajuwa kabisa kuwa asilimia 98 ya watanzania hawataki tozo ukiachana na hiyo asilimia 2% ya machawa wake na vikundi vya mapambio vinavyolipwa kutetea tozo

Lakini bado hajali, huyu mama ana kiburi sana, anafahamu fika kuwa hizi tozo zinawaumiza watanganyika sana sana, lakini hajali maana waumiao sio wenziwe.

Ule wembe tulomnyolea mtangulizi wake tutaendelea kumnyoa akiendelea na hii kiburi yake, ni kichaa tu anayeweza kuunga mkono tozo, itampasa Mwanaume kuwa kama "chachi" ndo aunge mkono tozo maana ni jambo ambalo haliungiki mkono

Ndipo nagunduwa ana kiburi sana huyu mama ukimuona nje na muonekano wake wa rohoni ni tofauti kabisa, hana sifa za kuwa kiongozi, huyu bibi hatufai kabisa.

Lakini nakwambieni huyo mama yenu asifikiri tutamchekea, tutaendelea kumkomalia hadi hii jeuri,ngendembwe, tambo na kiburi chake kimkwishe.
 

MKuu labda tu kama umeamua kutema nyongo. Samia hatatoka madarakani kwa maneno matupu.
 

Aliyekwamba anahitaji kura zenu ili awe Rais ni nani.Tunategemea goal la mkono.
 
Kilio cha samaki.
Tume ni yao
Polisi ni wao
Chama dola ni wao
Ninyi hata maandamano mkiitwa mnajifungia ndani nani akujali?
 
Muacheni mama aupige mwingi. Nchi hujengwa na wananchi.
 
Amen.
 
Ila baadhi ya Watz wana matatizo sana, sitoshangaa Samia akishinda uchaguzi mkuu kwa kishindo
 
Niliapa sitojihusisha na siasa na kupiga kura, nitaendelea hivyo hivyo mana hayo mambo sio muhimu kwenye maisha yangu.
 
Ila baadhi ya Watz wana matatizo sana, sitoshangaa Samia akishinda uchaguzi mkuu kwa kishindo
Swala si baadhi watanzania kutokua na akili nzuri,
Swala n hata wakiwa nazo na wasipompigia kura samia, Samia atashinda tu..( hii ndio jeuri ya CCM)

Yani anaachaje kushinda wkt ana
1).TUME inayochaguliwa na mgombea urais wa CCM( Samia mwnyw).
2). JESHI LA POLISI la linalofanya kazi kwa maslahi ya CCM.
 
Vyakula vinapanda bei kiasi cha wananchi wa kawaida kuhangaika kupata ulaji chakula unaostahili. Kwa mfano mchele sasa ni sh 3500 kutoka 1200 .

Mitaani hali ni ngumu. Mzunguko wa pesa ni kidogo kabisa na hata wafanya biashara wanalia na kusaga meno.

Wananchi wanakamuliwa tozo kiasi cha kuwafanya wakose kipato cha ziada na hii kuwanyika haki ya kupata mahitaji muhimu.

Watanzania wanaumia kila siku.
 
Mada Kama hii muhimu kwa maisha ya kila siku unakuta inakosa wachangiaji. Mambo mengine yaliyokuwa na mashiko ndiyo unakuta komenti kibao.
 
Utashangaa kesho Mgwasi ana-tweet "Tunaomba wananchi wawe watulivu, tutatolea ufafanuzi suala la kupanda bei za vyakula"

 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ingekuwa bora ukatuordheshea kama Kuna vitu kaboronga sio kusema hafai tuu
 
Ingekuwa bora ukatuordheshea kama Kuna vitu kaboronga sio kusema hafai tuu
Kwa kumsaidia:
Kuna suala la panya road na matukio mengi ya mauaji ya raia, hadi leo hajasema chochote. Ni kama hakuna kiongozi wa nchi. viongozi wa mikoa na wilaya wanatamka tu wanavyoona inafaa.

Kuna suala la kupanda holela kwa gharama za bidhaa kwa kisingizio cha vita, badala ya kudhibiti yeye anasema bidhaa zitapanda zaidi.

Kuna suala la mkanganyiko wa taarifa kati ya viongozi, mfano suala la vice na naibu waziri kuhusu uhifadhi wa samaki, mama hajasema chochote!

Suala la tozo amemuachia mwigulu.
Suala la nyongeza ya mshahara 2.3% badala ya 23% akamuachia Kasimu afafanue!
Viongozi wa kisiasa wanadharau jeshi la polisi, na anaunga mkono! Yuko kimya!
Hayo na mengine mengi yanaonesha hatuna rais.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…