Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Wewe ni mnufaika wa hayati, kwa taarifa yako hawezi kufufuka. Tafuta fursa ya kiuchumi ujipange nayo. Wapumbavu mlizoeshwa Ripoti FAKE ya CAG wakati wa Magufuli sasa Rais Samia anapokea Ripoti ya ukweli inayoonyesha gaps kwenye Serikali yake.

Badala kwanza ya kupongeza hilo la kupokea ripoti mnasema eti ajiuzulu?

Kwani yeye kuwa Rais ndiyo maana yake kuwa ndiyo kasababisha huo ufisadi?

Acheni mfumo ufanye kazi kisheria
Mbona povu?

Kwani kasema uongo?
 
Mbona povu?

Kwani kasema uongo?
Ni uwongo. Nchi ina mfumo, wanaopaswa kuchukua hatua dhidi ya waliotuhumiwa ni accounting officers wa Taasisi husika. Siyo jukumu la Rais kusema huyu aondoke kama ambavyo Magufuli alikuwa anawafukuza akina Wilson Kabwe pale daraja la Kigamboni.

Nchi ina mifumo ya utawala wa sheria, tuifuatae.
 
Ni uwongo. Nchi ina mfumo, wanaopaswa kuchukua hatua dhidi ya waliotuhumiwa ni accounting officers wa Taasisi husika. Siyo jukumu la Rais kusema huyu aondoke kama ambavyo Magufuli alikuwa anawafukuza akina Wilson Kabwe pale daraja la Kigamboni.

Nchi ina mifumo ya utawala wa sheria, tuifuatae.
Hao so called accounting officer wanamkagua boss wao aliyetajwa na waziri wa fedha kule bungeni kama ni mhusika wa upigaji?
 
Riport ya CAG is just assessment ha justify chochote mpaka pale itakojadiliwa na Bunge na TAKUKURU kufanya uchunguzi kisha wahutumiwa kufikishwa Mahakamani.

So,is just an assessment report,ambayo haiwezi mfanya MTU ajihudhuru.
 
Wengine sijui mmezaliwa kwa kupita tundu gn?,hivi kutoa maoni ya samia ajiuzuri wewe ni sukuma gang?
Impersonation of nonsense... sasa mambo ya siasa yanahusiana vip na mimi kuzaliwa mkuu?

Unaweza nitajia rais mmoja wa Africa aliewahi kujiuzulu toka kuumbwa kwa Dunia ukiacha SA.

Au ni hate motives behind the agenda.
 
Kenya na ukame wao kwa sasa hawana migao ya ueme kipindi hiki cha Masika, lakini cha ajabu Tanzania tuna migao hadi leo hii na hakuna anaye jali kabisa wala kuona ni tatizo, yaani migao ya umeme sio ishu kabisa.

Hakuna nchi kwa Bara la Africa kwa sasa yenye mgao wa umeme zaidi ya Tanzania, South Africa walikuwa na mgao mkari ila baada ya mvua kunyesha hali ilitulia, sasa sisi mvua zinanyesha usiku na mchana na still tuna migao ya umeme hii maana yake nini?

Ni vitu vya kushangaza sana na haitangazwi kama mabwawa bado hayana maji au wahuni wamefungulia maji ili migao iendelee wapige pesa na sana watakuja kuwambiwa wao ni stupidy.

Tukisema Mama ni very weka kuna wajinga wana amka kumtetea, huwezi ukatengeneza migao kipindi hiki ambacho mvua zinanyesha na mabwawa yana maji,
 
Ni wazi Samia huko alipo haamini kinachoendelea kwa namna anavyopondwa kila kona!

Samia alishajiaminisha eti anapendwa na hakutarajia kibao kumbadirikia kwa ghafla asivyotarajia hali inayompa wakati mgumu mno ki uongozi na ki siasa

Chaguo pekee alilobakisha ni yeye kutumia vyombo vya dola kuwathibiti wakosoaji wake hata ambao hakuwatarajia

NAJAWA HOFU HUENDA SAMIA AKAWA DIKTETA KULIKO...
 
Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani...
Moderator mbona unaunganisha Uzi huu.?? Hovyo Sana jf kwasasa
 
Ni ajabu kuendelea kuona bunge na taasisi mbalimbali za serikali zikiendelea na shughuli za kila siku ilhali taifa limekubwa na sintofahamu kubwa iliyoletelezwa na mkataba tata wa bandari yetu ya Tanganyika.

Vilevile ni ajabu kuendelea kumshuhudia rais samia akiendelea kuziba masikio pamoja na lawama lukuki anazoshtumiwa kwazo kwa yeye kuruhusu makubaliano ya mkataba ule tata yaendelee.

Ukweli ni kwamba taifa linashuhudia mtanzuko wa ajabu kuanzia kijijini hadi mijini kulihusu jambo lile.

Samia jitokeze ulisemee hilo na ikiwezekana sitisha jambo hilo kwa maslahi mapana ya nchi.

Tofauti na hapo jambo hilo halitokuacha salama ki siasa.
 
Back
Top Bottom