Shalom,
Toka ameingia madarakani kwa bahati ya umauti wa Magufuli kuna vitu hayuko sawa kuongoza na kusimamia watendaji.
Yafuatayo ayatibu
1. Anafanya usanii kuhusu haki za wafanyakazi mishshara hajaboresha, kuhusu malimbikizo ni usanii hajalipa.
2. Wafanyakazi wanaonewa sana na mabosi wao hasa kutopewa haki zao mfano kuna taasisi nyingi mabosi hawatekelezi viwango vipya vya posho za usafiri na vikao.
3. Halindi wakulima hasa bei ya pembejeo na pembejeo nyingi ni fake.
4. Masomo ya mazao ya wakulima hakuna jitahada.
5. Kero za Halmashauri kwa wakulima zimerudi.
6. Kero za maji, umeme, mfumuko wa bei.
7. Uhaba wa Dollar, kupanda kwa nauli Tena bila huruma na hakuna unsfuu wa maisha,
8. Analea kauli zenye dharau hana machungu (Mwigulu na Nape, January), anaongea kiulaini sana na yupo kinyumbani zaidi kauli zake na sio kama Rais wa nchi.
9. Toka ameingia ikulu hajawahi kutoa kauli thabiti za kukemea.
10. Wanaomsifia wanamdanganya wanaonufaika ni wafanyabiashara wanaokula na TRA, viongozi wenye mafungu ya kuiba na safari nyingi.
11. Kuna rushwa kithiri za pesa na ngono kwenye kupata kazi.
12. Bodi ya mikopo elimu ya juu inawatesa sana wanafunzi wa vyuo imefika wakati wanafunzi wanatoa rushwa za ngono na pesa ili mambo yao ya mikopo ifa ikiwe. Hii ni kero kubwa hadi aibu.
13. Watu wanakwepa kutoa receipts za EFD hapa ni kilio kikubwa TRA wamekaa ofisni inatia hasira sana.
14. Uanzishwaji wa biashara lessen na vibali ni jini la umaskini TRA ni nyoka mwenye sumu biashara zinakufa viwango vikubwa vya makadirio ya Kodi, wivu, ukiritimba.
15. Kodi ya mapato kwa wanaopangisha nyumba haikusanywi TRA wamekaa ofisni kimya, wenye nyumba wanaokula bata hawalipi Kodi ya mapato.
16. Anasafiri sana kuliko kutenga muda wa kushughulikia kero za wananchi, Hana muda wa kuhamasisha kufanya kazi kwa bidii na kulipa Kodi.
17. Hajui kama raia wanamchukia, wanahasira nae kwa kukosa ukali kwa watendaji wake.
18. CCM wanamchora tu ila yeye hajui wanampaka mafuta kwa gongo la chupa.
19. Mzunguko wa pesa ni aibu maisha magumu, mtu kupata chenji ya elfu10 na elfu5 ni kero kero kubwa.
20. Watumishi wengi wamekata tamaa wanafuraha nyumbani kuliko kazini, extra duty na overtime sifuri.
Rais shtuka kidogo kula na kipofu. Maisha ni ubinadamu ongeza furaha kwa wananchi na watumishi.
Ni hayo tu
Wadiz