Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Msomi unatakiwa ku behave kama msomi, kujitofautisha na akina Zembwela, Kitenge na Mpoto
Duh...!, naona unazidi kuniogesha!, yaani mimi ni kama Zembwela au huyo Kanga...?!. Mpoto ni kichwa!. Hao chawa wako wawili wanaweza kuleta hoja kama HII ?.
P
 
Mkuu Manyanza , hizi ni hisia tuu, uthibitisho ni 2025, utashangaa!.
P
Ila wewe naye wakati mwingine unashangaza sana, yaani kwa umri wako wote ulionao hujui nini hutokea wakati wa chaguzi zote nchi hii. Kwamba kinachotangazwa na tume kinaakisi uhalisia wa matokeo ya kura? yaani unakuta jumla ya kura inayotangazwa kwenye kituo X inazidi idadi ya waliojiandikisha kwenye hicho kituo.
 
Mkuu Snowflake, hili neno, elimu, elimu, elimu, ni hoja kuntu, sio tuu 95% Hawaelewi ni nini maana ya Maendeleo, wala hawajui wanachagua nini!.

Watanzania wanahitaji elimu, elimu, elimu!. Mimi kwa upande wangu kwasababu ni mwanahabari, mwanasheria, nimejotolea nitajitahidi kusaidia kuelimisha umma kuhusu katiba, sheria na haki.
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=Nk5MFIyFVsRr8TxT

Vipindi hivi vitaendelea mpaka 2025 wakati wa uchaguzi vitawaelimisha wananchi tuanze kuchagua kwa kufanya an informed decision na sio kuchagua kwa mazoea.
P

Umeamua kupoteza muda wako ni hicho kipindi chako, kama uwanja wa kampeni na uchaguzi hautakuwa sawa itakuwa umeamua kufukuzana na upepo tu. Mara ngapi hata kura za ubunge tu watu wanaamua kupitia sanduku la kura, then msimamizi wa uchaguzi anamtangaza wanayemtaka wao.
 
Duh...!, naona unazidi kuniogesha!, yaani mimi ni kama Zembwela au huyo Kanga...?!. Mpoto ni kichwa!. Hao chawa wako wawili wanaweza kuleta hoja kama HII ?.
P
Yuko sahihi kabisa, ingawa wewe unafanya makusudi kulinganisha na akina Zembwela. Uwezo, elimu, na uzoefu wako ni mkubwa sana na hupaswi kubehave hivyo unavyobehave
 
Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani.

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari.

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena.

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.
Nilidhani kila mtu anajua anapokwenda
 
Kwa sasa tuko uelekeo wa nyakanazi tunatafuta njia hatuioni...
 
Shalom,

Toka ameingia madarakani kwa bahati ya umauti wa Magufuli kuna vitu hayuko sawa kuongoza na kusimamia watendaji.

Yafuatayo ayatibu

1. Anafanya usanii kuhusu haki za wafanyakazi mishahara hajaboresha, kuhusu malimbikizo ni usanii hajalipa.
2. Wafanyakazi wanaonewa sana na mabosi wao hasa kutopewa haki zao mfano kuna taasisi nyingi mabosi hawatekelezi viwango vipya vya posho za usafiri na vikao.
3. Halindi wakulima hasa bei ya pembejeo na pembejeo nyingi ni fake.
4. Masomo ya mazao ya wakulima hakuna jitahada.
5. Kero za Halmashauri kwa wakulima zimerudi.
6. Kero za maji, umeme, mfumuko wa bei.
7. Uhaba wa Dollar, kupanda kwa nauli Tena bila huruma na hakuna unsfuu wa maisha,
8. Analea kauli zenye dharau hana machungu (Mwigulu na Nape, January), anaongea kiulaini sana na yupo kinyumbani zaidi kauli zake na sio kama Rais wa nchi.
9. Toka ameingia ikulu hajawahi kutoa kauli thabiti za kukemea.
10. Wanaomsifia wanamdanganya wanaonufaika ni wafanyabiashara wanaokula na TRA, viongozi wenye mafungu ya kuiba na safari nyingi.
11. Kuna rushwa kithiri za pesa na ngono kwenye kupata kazi.
12. Bodi ya mikopo elimu ya juu inawatesa sana wanafunzi wa vyuo imefika wakati wanafunzi wanatoa rushwa za ngono na pesa ili mambo yao ya mikopo ifa ikiwe. Hii ni kero kubwa hadi aibu.
13. Watu wanakwepa kutoa receipts za EFD hapa ni kilio kikubwa TRA wamekaa ofisni inatia hasira sana.
14. Uanzishwaji wa biashara lessen na vibali ni jini la umaskini TRA ni nyoka mwenye sumu biashara zinakufa viwango vikubwa vya makadirio ya Kodi, wivu, ukiritimba.
15. Kodi ya mapato kwa wanaopangisha nyumba haikusanywi TRA wamekaa ofisni kimya, wenye nyumba wanaokula bata hawalipi Kodi ya mapato.
16. Anasafiri sana kuliko kutenga muda wa kushughulikia kero za wananchi, Hana muda wa kuhamasisha kufanya kazi kwa bidii na kulipa Kodi.
17. Hajui kama raia wanamchukia, wanahasira nae kwa kukosa ukali kwa watendaji wake.
18. CCM wanamchora tu ila yeye hajui wanampaka mafuta kwa gongo la chupa.
19. Mzunguko wa pesa ni aibu maisha magumu, mtu kupata chenji ya elfu10 na elfu5 ni kero kero kubwa.
20. Watumishi wengi wamekata tamaa wanafuraha nyumbani kuliko kazini, extra duty na overtime sifuri.

Rais shtuka kidogo kula na kipofu. Maisha ni ubinadamu ongeza furaha kwa wananchi na watumishi.

Ni hayo tu

Wadiz
 
Shalom,

Toka ameingia madarakani kwa bahati ya umauti wa Magufuli kuna vitu hayuko sawa kuongoza na kusimamia watendaji.

Yafuatayo ayatibu

1. Anafanya usanii kuhusu haki za wafanyakazi mishshara hajaboresha, kuhusu malimbikizo ni usanii hajalipa.
2. Wafanyakazi wanaonewa sana na mabosi wao hasa kutopewa haki zao mfano kuna taasisi nyingi mabosi hawatekelezi viwango vipya vya posho za usafiri na vikao.
3. Halindi wakulima hasa bei ya pembejeo na pembejeo nyingi ni fake.
4. Masomo ya mazao ya wakulima hakuna jitahada.
5. Kero za Halmashauri kwa wakulima zimerudi.
6. Kero za maji, umeme, mfumuko wa bei.
7. Uhaba wa Dollar, kupanda kwa nauli Tena bila huruma na hakuna unsfuu wa maisha,
8. Analea kauli zenye dharau hana machungu (Mwigulu na Nape, January), anaongea kiulaini sana na yupo kinyumbani zaidi kauli zake na sio kama Rais wa nchi.
9. Toka ameingia ikulu hajawahi kutoa kauli thabiti za kukemea.
10. Wanaomsifia wanamdanganya wanaonufaika ni wafanyabiashara wanaokula na TRA, viongozi wenye mafungu ya kuiba na safari nyingi.
11. Kuna rushwa kithiri za pesa na ngono kwenye kupata kazi.
12. Bodi ya mikopo elimu ya juu inawatesa sana wanafunzi wa vyuo imefika wakati wanafunzi wanatoa rushwa za ngono na pesa ili mambo yao ya mikopo ifa ikiwe. Hii ni kero kubwa hadi aibu.
13. Watu wanakwepa kutoa receipts za EFD hapa ni kilio kikubwa TRA wamekaa ofisni inatia hasira sana.
14. Uanzishwaji wa biashara lessen na vibali ni jini la umaskini TRA ni nyoka mwenye sumu biashara zinakufa viwango vikubwa vya makadirio ya Kodi, wivu, ukiritimba.
15. Kodi ya mapato kwa wanaopangisha nyumba haikusanywi TRA wamekaa ofisni kimya, wenye nyumba wanaokula bata hawalipi Kodi ya mapato.
16. Anasafiri sana kuliko kutenga muda wa kushughulikia kero za wananchi, Hana muda wa kuhamasisha kufanya kazi kwa bidii na kulipa Kodi.
17. Hajui kama raia wanamchukia, wanahasira nae kwa kukosa ukali kwa watendaji wake.
18. CCM wanamchora tu ila yeye hajui wanampaka mafuta kwa gongo la chupa.
19. Mzunguko wa pesa ni aibu maisha magumu, mtu kupata chenji ya elfu10 na elfu5 ni kero kero kubwa.
20. Watumishi wengi wamekata tamaa wanafuraha nyumbani kuliko kazini, extra duty na overtime sifuri.

Rais shtuka kidogo kula na kipofu. Maisha ni ubinadamu ongeza furaha kwa wananchi na watumishi.

Ni hayo tu

Wadiz
Mkuu kwanza nikuombe hiyo notion ya kutumia neno USANII katika kunasibisha tabia ama mwenendo wenye longolongo ndani yake ni kutudhalilisha wasanii ambao tunafanya kazi kubwa kwenye jamii. Tunaelimisha, Tunaburudisha, Tunatibu kupitia sanaa zetu.

Tukirejea kwenye hoja.
Pale juu pameshakosa umakini, ndo maana KR yupo karibu isivyo kawaida ya status yake kujaribu kuokoa baadhi ya yanayookoleka.

Pili. Mimi simuoni kama SSH anakosea, bali tunasahau shina na mzizi wa fitina ni CCM. Tudeal nayo badala ya kuchambua watu wa kushughulika nao ndani humo
 
Ukweli uwekwe wazi.
Samia sio kiongozi mzuri bado anahitaji kuongozwa.
Ccm kwa ajili ya kupenda rushwa, dhuruma na ufisadi wameshindwa kabisa kumuongoza Rais. Wanaona hiki ndio kipindi chao cha mavuno.
Hali si shwari ktk nyanja nyingi.
 
Back
Top Bottom