Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Baadhi ya kauli ambazo tumezisikia kutoka kwa Mama Samia na viongozi wengine fulani waliohudumu chini ya JPM zinaonesha kwamba hao viongozi
Na je kwa kiongozi jambazi kama JPM aliyedumu chini ya fisadi WBM na msanii JMK kwa miaka zaidi ya ishirini, unasemaje?
Katika utumishi, sio kitu cha ajabu kuwa na tofauti za kimtazamo juu ya jambo fulani. Hata hivyo, inapotokea kwamba VP au waziri anaamini tofauti za kimtazamo zilizopo kati yake na Rais, juu ya jambo hilo, ni kubwa sana na hazivumiliki endapo Rais atakataa ushauri wake, basi ni bora akajitenga na msimamo wa Rais kwa kujiuzulu.
Je jambazi JPM alijitenga na wakubwa zake kwa miaka zaidi ya ishirini?
VP au waziri akishindwa kujitenga na kitu ambacho anaamini kinaumiza maslahi ya taifa, VP au waziri huyo anakuwa ameonesha udhaifu mkubwa sana wa kiuongozi. Kiongozi lazima awe na ujasiri wa kusimama upande wa haki hata kama kufanya hivyo maana yake ni kupoteza kazi. Vinginevyo, huyo hafai kabisa kushika dhamana kubwa kama hiyo.
Kwa miaka zaidi ya ishirini kwa nini Magufuli aliwatumikia hao anaodai walipindisha taifa hadi adai anainyosha?
Needless to say, VP au waziri anayehubiri na kusimamia asichokiamini hawezi hata kuweka kiasi sahihi cha juhudi inayohitajika kufikia malengo yaliyotarajiwa. Kwa maneno mengine, yeye anageuka kuwa VP au waziri mzigo.
Huyo jambazi na muuaji mkubwa kwa maiaka zaidi ya ishirini hakuwa mzigo?
Mama Samia ameonesha udhaifu wa kiwango cha PhD na amekuwa mfano mbaya kabisa kwa mawaziri wake. Bila shaka, Rais anawaambia mawaziri na taifa zima kwamba unafiki katika Serikali unakubalika. Yumukini mfano wa unafiki aliouonesha ni silaha ambayo wateule wake hawatasita kuitumia dhidi yake. Inasikitisha, to say the least!
Ficha upumbavu wako wewe shetani mkubwa, bila shaka hivi sasa unaamini huyo muovu yuko mbinguni akitoa amri kwa malaika, thubutu!
 
Wewe mtoa mada ndiyo mnafiki mkubwa sana wakati hayati anamkosoa JK hadharani nina maana JK hajafanya chochote kwenye awamu yake achane unafiki nyie vijana
 
Hivi wapingaji bado wako mpaka kipindi hiki,mi nilijua akiingia mwingine mtakaa kimya...
 
Ni kitu cha kusikitisha sana. Huyu mama alitakiwa aachie ngazi mapema kwa hiari yake akiwa makamu wa JPM, akatabanaisha anachokiamini. Kwa staili hii ya kugeuza mwelekeo analea tabia ya unafiki itakayolimaliza taifa kiutendaji na kimatokeo iwe kwa siasa za ndani au nje ya nchi. Mama akae akijua kuwa muda wote JPM alikuwa sahihi sana ukijaribu kuitafuta Tanzania iliyo huru kisiasa na kiuchumi.
Aache woga wa kupambana na wabaya wetu kama wao wasivyo waoga wa kutuhadaa na kuchezea rasilimali zetu kwa kutumia wanazoziita taasisi za kimataifa zenye kuwanyooshea njia za ukoloni mambo leo. Mama Pambana na mabeberu kwa usalama na usitawi wa watanzania. Usiwaogope.
 
Hakuna uhai baada ya umauti. Aliyekufa kafa. Mwacheni mama apige kazi akiwa na maono yake mapya. JPM angelikuwa hana maono mapya angelifanya aliyoyafanya?
Ni mpuuzi tu ambaye anaweza kuogopa kusawazisha makosa ya marehemu.

uko sahihi hakuna anayepinga au kumtakia mama ashindwe au aogope kufanya marekenisho ila ndo safari yake imeanza akiwa dereva na arekebishe kwa vitendo mapungufu ya aliepita maana walikuwa timu moja anyajua vyema na kwa kupima kila ushauri maana watu wanao msifu leo watamgeuka au umeasau Magufuli alivyoanza? maoni si chuki bali i kila mtu ana namna tofauti ya kuwasilisha maoni yake kibaya siku hizi watu hatukubaliani kutokubaliana bali mwenye maoni tofauti na wewe ni adui mwisho wa siku wote tunapotea na kupoteza uwezo wakujenga hoja kuazia nyumbani mtaani hadi mtandaoni
 
Ninachokumhuka na kuishi nacho kuhusu Wanasiasa ni ile kauli ya mwalimu wangu alipokuwa anawazungumzia watu hawa,alisema "Usimuamini Mwanasiasa,sababu watu hawa ni WAONGO" .

Yaani ni Waongo wa kauli na waongo wa vitendo.
 
Mkuu watu ni wajinga sana..hawajui wananchi wanahitaji nini na mama nae kafuata huo huo mkumbo..sio kwa zile hotuba zake yaan hata kuziskiliza ni kero..anataka turudi enzi za kina jk.kuchekeana chekeana.. hatutaki uswahili kwenye masuala ya kulipa kodi kwenye masuala ya rasilimali za nchi..
Time will tell..JPM will never be forgoten.
Hahahaaa mpigaji naona mnahaha km nn maana tulivo kua tunawaambia hali mbaya mnasema sisi ni wapiga dili sasa kimegeuka kwenu hapa hakuna kuonea tutalipa kodi inayostahili sio kwa kuoneana ...na nyinyi zamu yenu tulieni dawa iwaingie ,[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom