Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Naunga mkono.

Kuna masuala mengine uwezi kuyatolea maamuzi ya hapo hapo ili kumfurahisha mwenyeji wako lazima ulinde maslahi MAPANA ya wananchi wako.
 
Kuna watanzania hawana huruma.... kwahiyo wakulima walio lala na magunia ya mahindi pale mipakani unadhani wao hawakusajiliwa kusaidiwa kwa hili? Hata kama amefanikiwa kwa hili tuu ni neema kubwa sana maana haya tumeyakosa muda mrefu
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ yaani Rais wetu aalikwe na rais wa Kenya ili waongee mambo kadhaa ya kuboresha maisha ya wananchi wa nchi zote mbili (Uhuru anaangalia upande wake, Samia anaangalia upande wetu na kunakuwa na vuta'nikuvute kama ilivyo kawaida ya majadiliano ya kibiashara) na mwishowe nia ni kila mmoja apeleke maboresho kwa wanachi wake, ila tunachopokea ni 'mahindi' πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€.

Hatujasikia COVID, hatujasikia tutafute njia ya kushirikiana kunufaika na utalii nchi zote mbili, hatujasikia ujenzi wa barabara kuunganisha nchi hizi mbili, hatujasikia gesi wala kwamba watanzania waalikwe kufanya biashara bila vibali, nk. Tumesikia tu 'mahindi' πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Kwa hiyo leo tunatakiwa kujifunza kuwa Samia amealikwa Kenya na kuongea na wafanyabiashara na wabunge wa pande zote mbili kuongelea mahindi au alichofanikiwa ni kufungulia mahindi pekee? daaah.
 
Misukule ya Jiwe Yazidi Kutapatapa!!!
Yaani inahangahika hatari.... binafsi Mama Samia hajanigaiwia pesa wala kuleta unga kwangu ila nina amani, furaha na najihisi huru....mengine ya ziada.....akikosea tutamkosoa kwa nia njema lakini si kwa minyororo tuliyokuwa tumefungwa enzi hizo
 
Nimeamini kweli hii nchi mambumbumbu ni wengi sana kama mleta mada. Unasema tumewaachia gesi yetu hivi unajuwa hata kilichofanyika kuhusu gesi huko Kenya? Jamani tuwe tunafuatilia hivi vitu kikichofanyika ni MoU na mjadala unaendelea lengo ni kufikia mkataba utakaonufaisha pande zote mbili kwa sawa. Sasa inakuja mbuzi hapa inasema mama kaacha gesi Kenya aisee bado tuna safari kama nchi.
 
Magufuli was super bana, vitu vidogo kama hivi avifate kenya? Angepiga simu moja tu wasipotaka waache.watanunua wengine au sisi tutakula wenyewe kwani sh ngapi basii??

Ila jpm alikuwa chuma aisee
Nyie wengi wenu mlivutiwa na zile kelele zake na kuongea kwa vitisho na kujifanya mwamba kumbe werevu wanamchora tuu kikowapi sasa mbona imemuondoa? Au hujuwi kilichomuua mungu wenu?
 
Wakulima tumefaidika sasa tutajua mahindi kutoka Elfu 3 hadi Elfu 20 kwa debe
Viazi toka Elfu 30 hadi 180 kwa kilo 60
Nyanya toka Elfu 25 hadi Elfu 60 kwa Tenga
 
..Magu aliwahi kwenda Afrika Kusini akapeleka kamusi za kiswahili.🀣🀣

..ndio fursa aliyokwenda kutafuta South Africa.
Kufika Mwezi la 9 wafuasi wa Magu watakuwa hii bin taabani🀣🀣πŸ₯°πŸ₯°
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…