Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Unafiki wake nini, mbona hayati nae alikuwa hivo hivo wakati anamuambia JK asafir tu ili alete mahela, alivoingia unakumbuka akasemaje na akatendaje?

Mtateseka sana, nchi imechukuliwa na CDM kiulaini bila hata push up yani.
 
sijasoma yote nkamaliza, lakini nahisi hapa kuna harufu kali ya mataga wa lumumba wakiwa hoi kwa matamko machache tu ya bi mkubwa.
hizi sio zama za matambio, angalieni mwenzenu comrade kigwanga la ameshasoma upepo na anaenda na biti la uviko 21
 
Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.
Ni dhahiri huyu mama anautu na ubinaadamu ndiyo maana ya uongozi, Jua anaongoza watu sio mifugo, kama ataiga style ya JK na akaboresha alipokosea JK sioni kama kunashida yoyote.

Mwenye akili nzuri hawezi kuiga mengi ya aliyafanya huyu baba
 
Naona MATAGA mmefungua ID nyingi ili mumpinge mama.

Rais wenu Jiwe alishakufa

Hivi nani aliyekuwa na Ubavu wa kuzungumza au kumpinga jiwe? Yeye mwenyewe alishasema hapingiwi kwa hiyo unategemea wangefanyaje? zaidi ya kwenda na muziki wa jiwe huku wakiumia roho.
 
Mama Samia ndio mwokozi, Watanzania walikuwa wanamsubiria... Praise team mtahama nchi..

Mnafiki ni yule aliyekuwa anajifanya mtetezi wa wanyonge kumbe hana lolote...
Eti tunajenga kwa fedha zetu za ndani, kumbe ni fedha za mikopo...

Akwende zake huko akaongoze malaika...

Kama kuna kitu hakikuwa sawa, lakini alishindwa kujitenga nacho, hana namna sahihi ya kukikana isipokuwa unafiki! Where’s collective responsibility?
 
Tukisema huyu Mama hajielewi wala haelewi hii nchi inataka nini kwa sasa,kuna watu wanakuja na hadithi za Sukuma Gang Mara MATAGA!!
Mkuu watu ni wajinga sana..hawajui wananchi wanahitaji nini na mama nae kafuata huo huo mkumbo..sio kwa zile hotuba zake yaan hata kuziskiliza ni kero..anataka turudi enzi za kina jk.kuchekeana chekeana.. hatutaki uswahili kwenye masuala ya kulipa kodi kwenye masuala ya rasilimali za nchi..
Time will tell..JPM will never be forgoten.
 
Back
Top Bottom