Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Mkuu watu ni wajinga sana..hawajui wananchi wanahitaji nini na mama nae kafuata huo huo mkumbo..sio kwa zile hotuba zake yaan hata kuziskiliza ni kero..anataka turudi enzi za kina jk.kuchekeana chekeana.. hatutaki uswahili kwenye masuala ya kulipa kodi kwenye masuala ya rasilimali za nchi..
Time will tell..JPM will never be forgoten.
For his cruel heart n actions, he will never be forgotten
 
Ashasahaulika.

Ila ambao hawatamsahau ni wale aliowaumiza na maamuzi na ubabe wake, wale wa vyeti feki, tumbuatumbua, wa Kimara.....nk...hawatamsahau Kaa mabaya yake....haya huwa hayasahauliki.....ila mazuri husahaulika mapema sana.
Ni mmoja wa vyeti feki au? Hao waache wafie mbali bhana! Vyeti feki! NO! Hata kama tumempata rais mwenye vyeti vya aina hiyo, NO!
 
Tukisema huyu Mama hajielewi wala haelewi hii nchi inataka nini kwa sasa,kuna watu wanakuja na hadithi za Sukuma Gang Mara MATAGA!!
Jitambulishe basi upande wako! Wewe ni nani basi? Mtanzania na mpenda mabadiliko ya kweli kama mimi?

Tuungane pamoja basi kuipigania Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi! Badala ya kumlaumu mama wa watu, kisa tu ameamua kuondoa/ kupunguza baadhi ya madudu ya awamu ya tano.
 
Sukuma GANG/ Wajane, mna roho mbaya sana. roho zinawauma mama kukataa kuendeleza Dhambi za kuua na kutesa wasio na hatia.
Mmejipanga kumpoteza mama.
Ila hamtafanikiwa.
Tunaoipenda hii nchi tutamshauri tu afuate katiba basi.
 
Mkuu, hivi unajua madhara ya kupingana ama kwenda kinyume na kiongozi wa kiimla? Hivi unakumbuka CAG Assad kilimtokea nini pale alipoamua kusimamia ukweli na weledi ktk majukumu yake? Hivi unatambua nini kilichowatokea wapinzani hasa CDM pale walipojaribu kuonyesha mapungufu na udhaifu wa serikali ya awamu ya 5?

Ukiona wimbi la wasaidizi wa Rais aliyetangulia wakijitokeza hadharani na kupingana na mitazamo yake, basi utambue kuwa kuna sehemu mambo hayakuwa sawa. Isipokuwa walilazimika kufanya hivyo ili kulinda ajira zao na hatima zao za baadaye za kisiasa.
Huwa siwapendi viongozi wa nchi kwa mtindo wanavyopatikana. Hata huyu namuona ni feki tu, lakini ukiniambia CDM, natapika. Kwa nini CDM imeshindwa kuwa na viongozi wa maana? Wote vyeti feki na ufahamu feki! Sasa wooote wanamsifu Samia ili awaone wanafaa. Ni ajira tu inawasumbua.
 
Mama yupo vizuri Sana, tatizo nyinyi wanafiki, mnaopenda viongozi wanaowagawa wa Tanzania. Pia Wewe mnafiki namba moja. Dai katiba Mpya inayopunguza madaraka ya Rais.Rais akipewa madaraka anapewa kila kitu. Hata wasaidizi wasiporizika anachofanya Mkuu wao hawana jinsi.
 
Tukisema huyu Mama hajielewi wala haelewi hii nchi inataka nini kwa sasa,kuna watu wanakuja na hadithi za Sukuma Gang Mara MATAGA!!
😀😀😀 Sisi wengine tumekaa pembeni kuchungulia kwa chati...sijui Yale makontena yasiyolipia Kodi yatanza kupita Tena lini barabara...Sisi tunawahitaji zaidi wafanyabiashara kuliko wanavyotuhitaji Sasa....nickel ianze kuchimbwa haraka jamani...
 
Hivi MATAGA bado mnaamini Jiwe alikuwa right kwenye maamuzi yake mengi?Kulikuwa na mtu aliyekuwa na uwezo wa kumsahihisha Jiwe?Mama ameamua ''KUJISAHIHISHA'' kama kitabu cha Mwalimu J.K Nyerere kinavyoolekeza!
 
Ni mmoja wa vyeti feki au? Hao waache wafie mbali bhana! Vyeti feki! NO! Hata kama tumempata rais mwenye vyeti vya aina hiyo, NO!
marehem pia alikua na vyeti feki na alipo ulizwa akampoteza Ben. pole saambaya
 
Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.
Mbona Hayati hamkuuliza anatupeleka Wapi Acheni Unafiki wenu
 
Wafuasi wa Jiwe hamuamini macho yenu. Jiwe halinyanyuki tena . Muosha huoshwa . Wakati Jiwe linasema nchi inaibiwa kupitia mikataba mibovu. Kwani hakuemo kwenye baraza la Mkapa (rip) na baraza la Kikwete ?!. So kilichosababisha Maghufuli kukaa kimya kwa waliomtangulia ndicho kilichosababisha Rais Samia kukaa kimya kwa Maghufuli.

Odhis *
 
Back
Top Bottom