CCM Siyo ya kuiamini tena, laiti ningekuwa mmojawao baada tu ya matamshi hayo ningejiuzulu maana UNAFIKI ndio umethibitika rasmi hata kama kwa sasa wanajidai kutaka kujisafisha wameshaharibu taswira ni bora chama cha ADC kishike dola. Yuko wapi mama Sendiga?
Watu walikuwa wanawashambulia wanaharakati fulani kuwa ni wasaliti kumbe hao hao waliokuwa wakipiga kelele hizo ndio wasaliti na wanafiki namba moja.
1. Viongozi wa chama anachotoka hayati sio waungwana, wanafiki na inawezekana walidhamiria kumkatilia mbali kwa sababu wanazozijua bila kutafakari athari za muda mrefu ambazo kwa vyovyote vile haiwezekani kuzitibu na huenda kanda atokapo hayati ikaamua kukisurubu na kukifutilia mbali chama hicho huko na kwamba ni bora kurejea kwenye vyama mbadala. Hao watu ni wakimya, wapole, wanajulikana kama washamba na waliochelewa lakini wafuatilie ni kitu gani walifanya kwa Wajerumani, Waarabu wakaishia Kayenze, Nyerere alifanyiwa nini uwanja wa Nyamagana, Tabora, Shinyanga na Mara.
2. Wasaidizi wa Rais kuhusu usalama
3. Daktari maalum wa Rais
4. Wasaidizi na washauri wakuu wa Rais
Kwanza kitendo cha viongozi wa ngazi za juu kufanya ziara mikoani ndani ya muda ambao tetesi za hayati kuugua zikiwa zimeshika kasi ni uthibitisho kwamba ni sharti wawajibike kwa kuwahadaa waTanzania. Huwezi kumdanya Mtanzania eti Rais anawasalimia na anahimiza kuchapa kazi huku ukijua ukweli ni kinyume chake. Maana kila ukifanya ziara popote ndani ya eneo la utawala unatakiwa kuwa unampa taarifa mkuu wako wa kazi sasa ilikuwaje mmoja yuko huko Kaskazini kwa ziara ya siku sita na mwingine ziara huko Kusini huku kauli zikipishana? Wakato mmoja akiwaambia wananchi Rais anawasalimi lakini alipopewa kero za wananchi akadai atamtuma waziri husika kuja kufuatilia kero hizo kitu ambacho kwa miaka zaidi ya sita alikuwa hatoi kauli kama hiyo zaidi ya kusema atawakilisha kwenye mamlaka husika?
Taarifa tatu zinazokinzana zinatakiwa zitolewe ufafanuzi na uthibitisho ikielezea sababu za kitalaamu za kifo kwamba
1. Hayati aliugua ugonjwa wa moyo ghafla aina ya 'Atrial Fibrillation'
2. Hayati alishambuliwa na vimelea vya UVIKO (COVID-19) kama inavyodaiwa na mkosoaji wa hayati aliyeko huko Ubelgji
3. Hayati alifariki kati ya tarehe 6/3 na 9/3/2021 lakini ikafanywa siri hadi vuguvugu la mapinduzi lilipotaka kutumia nafasi hiyo kutwaa madaraka ndipo makamu wa Rais akaamuriwa sijui na nani kutangaza kifo akiwa ziarani huko mkoani Tanga wakato awali aliwaaminisha wananchi Rais ni mzima akiendelea na majukumu yake na kwamba aliwataka kuchapa kazi!!!
Wafuatao kwa namna yoyote wanawajibika kutoa wingu kwamba hawakujua kilichokuwa kinaendelea kuhusu ugonjwa, kupelekwa nje ya nchi na kurejeshwa kisirisiri pindi taarifa zilipovuja.
1. Makamu mwenyekiti wa chama tawala
2. Katibu mkuu wa chama tawala (kama yupo)
3. Katibu Itakadi na uenezi wa chama tawala
4. Makamu wa Rais (maana inasemekana wakati tetesi zimeanza mwanzo kabisa alifuatwa kutoka Zanzibar na akaongezewa ulinzi kisha yeye akaanza ziara mkoani Tanga wakati sintofahamu ikiiendelea)
5. Waziri mkuu ambaye mara kwa mara alikuwa akifanya ziara nyanda za juu Kusini na kukatishakatisha ziara hizo bila kuweka sawa kilichokuwa kikitolewa taarifa kutoka kwa Watanzania walioko nje ya nchi;
6. Mkurugenzi usalama
*Masuala yaliyopo hapo juu ni ya mhimu kuteguliwa sasa ili hali ya hewa iendane sawia na mabadiliko yanayoendelea hivi sasa kwa utawala ulipo madarakani ijapokuwa sio mpya (Chama kile kile chenye mjumuiko wa makundi yanayosigana kupambania madaraka chini kwa chini)
*The north exists in the presence of south whilst the west and east conveniently interacts with the former and latter steadhold polarized pillars.