Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani

Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari

Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi

Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena

Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.
Mama bwana anawaacha sana watendaji wake hewani.Unapompa mtendaji jukumu ni lazima kuwe na specifics and time line.Unapaswa pia kusema kama hakutimiza consequences ni nini kufuatana na sheria.Maneno "kaangalieni kama inawezekana," ni too vague.She is in short too general and soft,kitu ambacho hakifai kwa mtendaji mkuu.
 
Baadhi ya kauli ambazo tumezisikia kutoka kwa Mama Samia na viongozi wengine fulani waliohudumu chini ya JPM zinaonesha kwamba hao viongozi walikuwa wanahubiri na kusimamia wasichokiamini. Kitendo hicho cha kuhubiri na kusimamia wasichokiamini kilikuwa unafiki na utovu mkubwa wa nidhamu kwa wapigakura wa nchi hii. Hili limenikumbusha hata ule utovu wa nidhamu ambao VP na PM waliuonesha wiki nne zilizopita kwa kuwapa wapigakura salaam hewa kutoka kwa Hayati JPM ilhali wakijua JPM alikuwa mahututi ndani ya ICU.

Katika utumishi, sio kitu cha ajabu kuwa na tofauti za kimtazamo juu ya jambo fulani. Hata hivyo, inapotokea kwamba VP au waziri anaamini tofauti za kimtazamo zilizopo kati yake na Rais, juu ya jambo hilo, ni kubwa sana na hazivumiliki endapo Rais atakataa ushauri wake, basi ni bora akajitenga na msimamo wa Rais kwa kujiuzulu.

VP au waziri akishindwa kujitenga na kitu ambacho anaamini kinaumiza maslahi ya taifa, VP au waziri huyo anakuwa ameonesha udhaifu mkubwa sana wa kiuongozi. Kiongozi lazima awe na ujasiri wa kusimama upande wa haki hata kama kufanya hivyo maana yake ni kupoteza kazi. Vinginevyo, huyo hafai kabisa kushika dhamana kubwa kama hiyo.

Needless to say, VP au waziri anayehubiri na kusimamia asichokiamini hawezi hata kuweka kiasi sahihi cha juhudi inayohitajika kufikia malengo yaliyotarajiwa. Kwa maneno mengine, yeye anageuka kuwa VP au waziri mzigo.

Mama Samia ameonesha udhaifu wa kiwango cha PhD na amekuwa mfano mbaya kabisa kwa mawaziri wake. Bila shaka, Rais anawaambia mawaziri na taifa zima kwamba unafiki katika Serikali unakubalika. Yumukini mfano wa unafiki aliouonesha ni silaha ambayo wateule wake hawatasita kuitumia dhidi yake. Inasikitisha, to say the least!
Mama Samia ndiye Rais. Yaliyopita yamepita. Tugange yajayo.
Mwenyezi Mungu mtukufu ndiye yeye aliye mkuu. Mapenzi yake yatimizwe siku zote
 
Nadhani Mada yako ni ishara ya chuki binafsi dhiti ya mama yetu.... Na tambua maneno yako ni matunda ya Uhuru uliopewa na Mama yetu rais Samia
 
ALIKUWA MATAGA NO. 1 KWA JPM; alifanya kila kitu chini ya JPM....hata vile ambavyo hakukubaliana navyo!!! akaamua kuwa mnafiki ili apate mkate wake maisha yaendelee

JPM wa sasa wamebadilika ni wananchi wa TANZANIA aambao anawatumikia

JE ANAWATUMIKIA KWA UNAFIKI ULE ULE WA ALIVYOFANYA KWA JPM? au anatoa moyoni anachofanya?

kama usanii wake ulikuwa wa kiwango kile, hawezi kuaminika kwa sasa hivi pia

kaharibu
 
Naona MATAGA mmefungua ID nyingi ili mumpinge mama.

Rais wenu Jiwe alishakufa

Hivi nani aliyekuwa na Ubavu wa kuzungumza au kumpinga jiwe? Yeye mwenyewe alishasema hapingiwi kwa hiyo unategemea wangefanyaje? zaidi ya kwenda na muziki wa jiwe huku wakiumia roho.

mataga wa zamani sio?

wewe, lema, lissu ndio mataga wapya? au?
 
kunasehemu nilisoma kuwa kuna ukanda haustahili kupewa urais...naomba huu mwiko uanze kufuatwa tutakuja pata shida huko mbeleni.....

sahizi watu wanaona kama hii nchi ya kwao, full ukabila.... mwingine anaanzisha uzi eti wao ndio wanakura turufu tena, anatishia eti mbona south africa wazulu wanamfalme wao......

ikiwezekana tutaacha hata kupeleka maendeleo huko mmepata ya kutosha tayari.
 
ALIKUWA MNAFIKI NA MATAGA NO. 1
You are now pressed between a rock and hard surface.
Ulimtetea jpm kinafiki
Sasa unaogopa kumtetea Samia sababu yuko against sera za jpm though sera za jpm hukuzipenda kutoka moyoni
Wewe ulikuwa unapambana na cdm kwa kuendorse madudu ya jpm
You know we know mama ni wa ile imani yako but unajua we are watching...
You are caught up
 
Kuna baadhi ya kauli zake, niliwaona mawaziri kama wamepigwa shock hawaamini masikio yao. Siasa most of the time si hasa.
 
Tz taasisi zetu zinazidi kuwa dhaifu kwa ajili hakuta utaratibu wa kuwajibishana...

Ndo maana hata waziri, ama kiongozi hawez kujiwajibisha kama hakuna wa kumuwajibisha....

Kwa hiyo ktk mazingira kama haya hata mkitofautiana mtazamo na senior wako... unakausha tu adi umalize muda wako coz mazingira nje na hapo ni magumu sana.
 
Pole sana Mkuu vumilia ni kawaida ya Penicillin injection ilivyo inauma balaa. Mama ameonesha njia sasa tutakwenda kwa speed ya kutosha huku tukitabasamu.
 
Ni swala la muda tu. Hapa hatuna Rais
Mtapata tabu Sana[emoji1][emoji116]
JamiiForums-399706182.jpg
 
sijasoma yote nkamaliza, lakini nahisi hapa kuna harufu kali ya mataga wa lumumba wakiwa hoi kwa matamko machache tu ya bi mkubwa.
hizi sio zama za matambio, angalieni mwenzenu comrade kigwanga la ameshasoma upepo na anaenda na biti la uviko 21
Hii Inaitwa ROBA YA MBAO, kila ulichokimeza utakitema[emoji1][emoji116]

IMG_20210329_112523.jpg
 
Askofu Chidi na genge lako naona mnafika mbali sasa,kama hamukubali uongozi wa Rais Samia basi hameni nchi. Wewe uliacha uchungaji kuja kwenye siasa ili utimize ile ndoto yako ya kuwa na Taifa la Wasukuma,polisi walikukamata kisha wakakuachia kumbe mlikuwa na malengo ya muda mrefu kuivuruga nchi.
Huyu Chidi ndio yule niliyemsikia mjengoni akitowa sifa kebekebe akisema Samia ni konki fire akim-quote mtanzania Pierre au ni mwingine?
Kama ni huyo basi ni kinyonga aisee. Nilijua yupo upande wa Samia
 
Back
Top Bottom