Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Leo kama kawaida yangu, nikaamua kutembea mtaani kusikiliza wananchi wanasemaje kuhusu tozo hizi ulizowawekea wananchi.

Wananchi wanasema miezi yako mitatu ya kwanza uliwapa matumaini makubwa sana kwa hatua zako za kuonyesha hupendi uonevu, ukafungulia watu waliobambikiziwa kesi, ukafungua akaunti za wafanyabiashara kwenye haya mambo wananchi waliyapenda sana.

Ila sasa wanasema kuwa kwa hizi tozo ulizowawekea kwenye maisha yao hausomeki kabisa!

Wanahoji, wanasema mbona Mawaziri wako, makatibu wakuu, wanaburuza migari ya bei kubwa huku wakiwa na allowance ya mafuta kila wiki au mwez halafu unatoka hapo unawapandishia wananchi kodi kwenye mafuta yao, Wanauliza au kwa sababu hivi vitu kwenu ni bure kwa hiyo hamna uchungu, yaani hamjali?

Mama Wananchi huku mtaani wanahoji inakuwaje unapunguxa kodi kwenye pombe lakini unaiongeza kwenye mafuta, wanahoji huu ni uchumi wa wapi?, Wananchi wanasema ina maana unawapa unafuu walevi kuliko wasafiri wanaohitaji kumove around ili kufanya biashara?

Mheshimiwa rais, wananchi wanasema unazurura sana angani, yaani hutulii sehemu moja kufanya kazi, wanasema kila safari yako ni gharama kwao na eti ndiyo maana unawatoza makato makubwa ili kufinance safari zako za kutwa kucha uko angani.

Ndugu rais, wananchi huku kitaa wanasema hausomeki, wanasema hoja zenu za kujenga shule na barabara huko vijijini hazina mashiko wanasema kwa miaka yote 69 mliyokaa madarakani kwa nini hamjajenga hizo shule, kwa nini hamjajenga hizo barabara?

Mheshimiwa rais huku mtaani wananchi wanahoji sera yenu ya Elimu bure iko wapi wakati hata kujenga shule bado mnaenda kukamua pesa za watu walewale mnaosema eti mbataka kuwapa elimu bure? —Mheshiniwa rais, wababchi wanasema kuwa huu ni utani, dharau na kichekesho chenye kutia hasira. Wanasema eti unawakamua pesa bila aibu ili eti uwape elimu bure, elimu bure gani hii?

Ndugu rais, nataka nikwambie kuwa unapoteza sapoti ya wananchinkwa kasi ya kutisha sana kwa sababu ya sera zako hizi za uchumi. Rudi kwenye drawing board au ng'ang'ania muenendo huu wananchi wakose imani na wewe!

Do something, time bado iko upande wako, lakini it is running very fast against you!
Acha aendelee kuupiga mwingi,ndio muda wake
 
Mama apunguze kurembua awe serious kidogo hili la tozo sijamwelewa kabisa anatu force tumkumbe jiwe sasa
Mwenyewe alishasema yeye na Jiwe ni kitu kimoja ninyi ndio mnalazimisha kumtofautisha.
 
Hizi tozo lazima zilipwe sisi watu wa vijijini ndo tunao jua jinsi barabara zilivyo mbovu,hii hela inayotozwa itasaidia kukarabati barabara za vijijini kwa kiwango cha changarawe labda mama atusaidie aondoe kabisa makato ya loan board maana watu wa loan board wapo kimya Pia aondoe riba za Bank ili uchumi uchangamke
 
Tatizo kubwa ni hao wananchi...

Hivi wakati Bungeni wanatengeneza haya maajabu hao wananchi walidhani wanaongelea Tozo zipi ? Za kwenye Game ya Monopoly?

Hao wananchi ingebidi waanze na kina Mwigulu huko huko jimboni kwake bila kusahau kuwazomea kina Ndugai... (Bunge ndio mzizi wa Fitina)
 
Hawa wametofautiana jiwe licha ya mapungufu yake hakutokomoa na mikodi ya uonevu ka hii ya miamala, sikutiana tu umaskini, jiwe Ali control inflation's Sasa huyu kupandisha mafuta ndio kila kitu kitakuwa juu maradufu.
 
Mimi hata silipi narudi kutumia bank,hata watu wengi minao wajua wanatumia means nyingine, acha wazalendo watoe Hela mie kapuku sina Hela za kuchezea kabisa.
 
Hawa wametofautiana jiwe licha ya mapungufu yake hakutokomoa na mikodi ya uonevu ka hii ya miamala, sikutiana tu umaskini, jiwe Ali control inflation's Sasa huyu kupandisha mafuta ndio kila kitu kitakuwa juu maradufu.
Jiwe mwenyewe alikuwa anaelekea huko huko, maana alikuwa anaendesha nchi kwa mikopo na dhulma.
 
Ndo madhara ya kuua uchumi na siasa mbaya zilizokimbiza wawekezaji nchini maana wafanyabiashara na wawekezaji kukimbia maelfu ya watu walikosa ajira. Ccm wawekege na akili ya kuteua watu wenye vision ya kututoa kwenye umaskini na sio jinsi siku zinavoenda Hali ndo inazidi kuwa mbaya. Too much mikodi huua uchumi, na wawekezaji kula corner
 
Leo kama kawaida yangu, nikaamua kutembea mtaani kusikiliza wananchi wanasemaje kuhusu tozo hizi ulizowawekea wananchi.

Wananchi wanasema miezi yako mitatu ya kwanza uliwapa matumaini makubwa sana kwa hatua zako za kuonyesha hupendi uonevu, ukafungulia watu waliobambikiziwa kesi, ukafungua akaunti za wafanyabiashara kwenye haya mambo wananchi waliyapenda sana.

Ila sasa wanasema kuwa kwa hizi tozo ulizowawekea kwenye maisha yao hausomeki kabisa!

Wanahoji, wanasema mbona Mawaziri wako, makatibu wakuu, wanaburuza migari ya bei kubwa huku wakiwa na allowance ya mafuta kila wiki au mwez halafu unatoka hapo unawapandishia wananchi kodi kwenye mafuta yao, Wanauliza au kwa sababu hivi vitu kwenu ni bure kwa hiyo hamna uchungu, yaani hamjali?

Mama Wananchi huku mtaani wanahoji inakuwaje unapunguxa kodi kwenye pombe lakini unaiongeza kwenye mafuta, wanahoji huu ni uchumi wa wapi?, Wananchi wanasema ina maana unawapa unafuu walevi kuliko wasafiri wanaohitaji kumove around ili kufanya biashara?

Mheshimiwa rais, wananchi wanasema unazurura sana angani, yaani hutulii sehemu moja kufanya kazi, wanasema kila safari yako ni gharama kwao na eti ndiyo maana unawatoza makato makubwa ili kufinance safari zako za kutwa kucha uko angani.

Ndugu rais, wananchi huku kitaa wanasema hausomeki, wanasema hoja zenu za kujenga shule na barabara huko vijijini hazina mashiko wanasema kwa miaka yote 69 mliyokaa madarakani kwa nini hamjajenga hizo shule, kwa nini hamjajenga hizo barabara?

Mheshimiwa rais huku mtaani wananchi wanahoji sera yenu ya Elimu bure iko wapi wakati hata kujenga shule bado mnaenda kukamua pesa za watu walewale mnaosema eti mbataka kuwapa elimu bure? —Mheshiniwa rais, wababchi wanasema kuwa huu ni utani, dharau na kichekesho chenye kutia hasira. Wanasema eti unawakamua pesa bila aibu ili eti uwape elimu bure, elimu bure gani hii?

Ndugu rais, nataka nikwambie kuwa unapoteza sapoti ya wananchinkwa kasi ya kutisha sana kwa sababu ya sera zako hizi za uchumi. Rudi kwenye drawing board au ng'ang'ania muenendo huu wananchi wakose imani na wewe!

Do something, time bado iko upande wako, lakini it is running very fast against you!
Akiendelea kuongoza nchi kipopoma popoma ipo siku raia watampopoa mawe huku mitaani
 
Tatizo kubwa ni hao wananchi...

Hivi wakati Bungeni wanatengeneza haya maajabu hao wananchi walidhani wanaongelea Tozo zipi ? Za kwenye Game ya Monopoly?

Hao wananchi ingebidi waanze na kina Mwigulu huko huko jimboni kwake bila kusahau kuwazomea kina Ndugai... (Bunge ndio mzizi wa Fitina)
Hapa ndipo tunapoona umuhimu wa kuwa na upper Chamber ya parliament (senate) ambayo itakua inafanyia vetting bills za lower chamber.

Tusipofanya hivi hawa wabunge wanaochaguliwa Kwa amsha amsha huko majimboni watatuumiza sana.
 
So wanataka mwendazake arudi kwenye nafasi yake? Kisa tu jambo moja la kutuma na kutoa pesa tigopesa? Mara hii hili jambo moja limefuta mazuri yote aliyofanya? Ni bora mother awe dikteta tu kama JPM, Hawa watz hawana shukrani na ni mabingwa wa kusahau
 
Huyu New Dictator with Magufulism without Magufuli, amri za mauaji ,utekaji, ubambikizi wa kesi and the like atrocities bado ziko pale pale, hajawahi kuzitengua na bado zinafanya kazi.
1. Angalia anavyowalinda akina Mdee na uasi wao wa Katiba chini ya Ndugai.
2. Kongàmano la Katiba Mwànza limezuiliwa kwa amri yake
3. Mikutano ya kisiasa marufuku

4. Etc etc etc and much more to come

You need a new approach!
 
Kwa sasa hivi ni kama vile tupo kwenye hali ya hatari,

Na lawama zote ni kwako hivi nini kinaemdelea huko ndani, je, nchi imefilisika? hata kama ni kodi ya uzalendolakini sio kwa kiwango hicho aisee, tozo imekua kubwa mno kwenye miamala, bado kwenye mafuta tena,

Ni bora utuambie ukweli sisi kama Raia wako tuelewe, kama mtangulizi wako aliiacha nchi haina hela tujue tu tutaridhia kwa hiyari hata kuichangia nchi, tukiambiwa ukweli tuko tayari hata muweke control namba tuichangie nchi kwa hiyari

Lakini kwa haya mambo ya kuongeza tozo kinyemera hapana kwakweli mnamkandamiza mwananchi na sasa mnaenda kuiua kabisa huduma ya kifedha kwa mitandao ya simu,

Bora ulihutubie taifa kuwaeleze ukweli Raia kama nchi imefilisika tujue.

Over
 
So wanataka mwendazake arudi kwenye nafasi yake? Kisa tu jambo moja la kutuma na kutoa pesa tigopesa? Mara hii hili jambo moja limefuta mazuri yote aliyofanya? Ni bora mother awe dikteta tu kama JPM, Hawa watz hawana shukrani na ni mabingwa wa kusahau
Wacha wawekezaji waenjoy kuwekeza Tanzania hata kama hawalipi kodi.
 
Back
Top Bottom