Mama Samia achana na cheap popularity haitakusaidia lolote unatakiwa usiwe muongeaji sana maana naona unaanza kutoboa matundu ya hela wakati huo ukiwa umewekwa kwenye mtego mgumu na mzito sana wa ilani yenye kurasa 300 ya kutekeleza miradi yote iliyoko kwenye ilani.
Yaani kumbuka sasa hivi hauko kwenye meli mpya uko kwenye meli ileile sema tu imepata mawimbi katikati ya safari.
Mama nimekushangaa sana unaposema kuna miradi mingine iko kwenye makaratasi wakati wewe na Hayati Magufuli ndio mliotembea nchi nzima kuinadi kwa hiyo tunataka ahadi zilizoko kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Tofauti na hapo hatutakuelewa tutanyima kura 2025 kama ukitaka kuomba ridhaa ya kugombea tena.
Jitahidi sana kwenye suala la kodi usiwalaumu tu TRA waonye hata wafanyabiashara pia maana ni wakorofi.
A leader must have a vision of where she wants her country to be in the the future? Does Samia have a vision for Tanzania? Kuwaambia Wananchi kuwa bei zitaendelea kupanda kiholela [ price gauging] ni kuwahimiza wafanya biashara kuwaumiza wananchi!! Samia anatakiwa awe upande wa wananchi kwa serikali yake kusimamia na kuwaadhibu wafanyabisahara wanaofanya price gauging!
Mfano mzuri ni hawa wauza vifaa vya ujemzi kama nondo na cement; Kuna viwanda vingi vinavyotengeneza nondo nchini hivyo haiwezekani wakauza wote nondo ya 16mm sh. 45,000 isipokuwa tu kama wana CARTEL ! Hivyo serikali haina budi kuingilia kati kulinda wananchi. Kuhusu cement , Twiga cement kiwanda chake kinatumia gesi kutoka kusini katika kuzalisha cement yake hivyo tunategemea kuwa TWIGA cement bidhaa yake iwe na Bei chini zaidi kuliko viwanda vingine vya cement visivyotumia gesi kuzalisha na sio vinginevyo!!
Waziri wa viwanda anatakiwa ndio awe mstali wa mele kuhakikisha kua huu mfumuko wa bei nchini hauchangizwi na wafanya biashara wanaoongeza bei ilikuwaumiza wananchi na sio kwa sababu cost of production yao imepanda!!