Kama ilivyo hapo juu, Ukweli sisi Watanzaia mlisha tuona mazezeta wa kutosha kiwango cha juu kabisa, sijui nisemeje! Viongozi wenzako tulisikia wakitupa matumaini ya kwamba bei ya mafuta ingelishuka kwa kiasi fulani kwa mwezi huu wa july, lakini ni kinyume chake kabisa! wengi tulisubiri ili angalau tusubiri kapunguzo ka bei hiyo eti pengine kwa sababu ya hiyo ruzuku.
Hivyo ni kweli unayodhamira nzuri kwetu Watanzania wa bara? Maisha yamekuwa magumu sana tena sana, hii hali ni tofauti kubwa sana na kule visiwani, sasa twajiuliza hii inachangiwa na nini?
Nina imani pengine lipo kundi linalokuingiza chaka na hawa wafanyabiashara wakubwa ndiyo wanaofaidika sisi tulio wengi tunaisoma namba!
Hivyo usikii kelele za kulaumiwa Waziri wako J.Makamba, haya bibie lakini kipo utakachovuna kwa siku zijazo, nakutakia safari njema huko ulipo.