Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Tangu ameingia madarakani nimeona ziara nyingi anazifanyia nje ya nchi na katika ziara hizo tulichokipata ni mikopo mbalimbali kwa ajiri ya miradi mbalimbali ! Kuhusu kukaa nchini na kufanya ziara katika mikoa mbalimbali kujuwa kero za wananchi hili naona hili halifanyi kabisa kwa asilimia kubwa, hata akikaa nchini mara nyingi ana kaa ikulu na kusubilia taarifa za viongizi wake wa chini na akikaa zaidi ya miezi miwili basi ujue kuna mtu atapata teuzi hayo ndiyo nayoyaona anayoyafanya.

ziara kubwa nchini ya kwanza kumbukumbu ya mwalimu nyerere iliyofanyika mkoa wa mara na akaambiwa kero za mkoa huo

Ziara ya pili mkoa wa mwanza sikukuu ya wafanyakazi

Ziara ya tatu mkoani pwani

Ziara ya nne daresalaam kukagua soko la kariakoo

Ziara ya tano mkoa wa tabora kuzindua barabara.

Ziara ya sita mkoa wa kagera wilaya ya chato kuzindua shule mgeni alikuwa MSEVENI.
Kwa hiyo hii ni mikopo sio? 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220618-081225.png
    Screenshot_20220618-081225.png
    145.1 KB · Views: 13
  • Screenshot_20220618-081021.png
    Screenshot_20220618-081021.png
    161.1 KB · Views: 14
  • Screenshot_20220616-205756.png
    Screenshot_20220616-205756.png
    149.9 KB · Views: 13
  • Screenshot_20220614-122928.png
    Screenshot_20220614-122928.png
    149.7 KB · Views: 11
  • Screenshot_20220614-121554.png
    Screenshot_20220614-121554.png
    199.8 KB · Views: 10
Kama ilivyo hapo juu, Ukweli sisi Watanzaia mlisha tuona mazezeta wa kutosha kiwango cha juu kabisa, sijui nisemeje! Viongozi wenzako tulisikia wakitupa matumaini ya kwamba bei ya mafuta ingelishuka kwa kiasi fulani kwa mwezi huu wa july, lakini ni kinyume chake kabisa! wengi tulisubiri ili angalau tusubiri kapunguzo ka bei hiyo eti pengine kwa sababu ya hiyo ruzuku.
Hivyo ni kweli unayodhamira nzuri kwetu Watanzania wa bara? Maisha yamekuwa magumu sana tena sana, hii hali ni tofauti kubwa sana na kule visiwani, sasa twajiuliza hii inachangiwa na nini?
Nina imani pengine lipo kundi linalokuingiza chaka na hawa wafanyabiashara wakubwa ndiyo wanaofaidika sisi tulio wengi tunaisoma namba!
Hivyo usikii kelele za kulaumiwa Waziri wako J.Makamba, haya bibie lakini kipo utakachovuna kwa siku zijazo, nakutakia safari njema huko ulipo.
 
Zanzibar wana Rais
Katiba mpya ni muhimu kuliko. Haiwezekani kabisa rais mzanzibar kule Zanzibar na wakati huo huo bara ni mzanzibari tena.
Kwa mamlaka makubwa ya rais wanaweza kufanya watakavyo sababu katiba inaruhusu.
 
Umetoa fedha kuruzuku mafuta lakini watu wameipiga yote. Ona bei ya mafuta imepaa
 
Inawezekana andiko lako likawa na mashiko makubwa lakini limepoteza maana kwa hoja zako nyepesi.......

Kwa kifupi umeileta mada kiumbea na kizandiki......hakuna tuzo wala mashindano ya kuanzisha mada......kama huna taarifa za kutosha juu ya jambo husika basi Baki nalo tu mwenyewe.......
 
Tukumbushane,

Wakati mijadala mingine ikiendelea,

AGENDA kuu Kwa sasa nchini ni KATIBA mpya.

RASIMU alosimamia Judge WARIOBA irudi mezani mjadala uanzie hapo.

Amen
 
Soko la dunia mafuta hayapandi?..Kama hayapandi duniani tangu kuanza ruzuku Basi u sahihi kuamini anadanganywa
 
Mama kunahaja ya yeye kuangalia washauri wake ni kama haoni mambo yanavyoenda malalamiko ya wananchi ni makubwa yeye ameziba masikio kule Bima huku mfumuko wa bei kila kitu kipo hoi watendaji wake wanakula kuku kwa mlija huku wananchi wakisoma namba kwa kukosa huduma mbalimbali za kijamii kwa kweli nchi yetu kuongoza ni rahisi sana. hii awamu ni ngumu na hatari kuwahi kutokea tangu tupate uhuru.

Mama hali ni ngumu mno tena ni ngumu mno hao vijana wako ni matapeli wanakupotosha huku mtaani mambo ni magumu mno watu wamechoka chakali! wanakuita majinamengimengi mwisho wa siku watatoka hapo yatakuwa kama ya srilanka.
 
Mawaziri wawili vijana wa nishati na fedha wanaichafua taswira ya taasisi ya urais makusudi.

Wenye chama Chao chukueni hatua.
 
Mama kunahaja ya yeye kuangalia washauri wake ni kama haoni mambo yanavyoenda malalamiko ya wananchi ni makubwa yeye ameziba masikio kule Bima huku mfumuko wa bei kila kitu kipo hoi watendaji wake wanakula kuku kwa mlija huku wananchi wakisoma namba kwa kukosa huduma mbalimbali za kijamii kwa kweli nchi yetu kuongoza ni rahisi sana. hii awamu ni ngumu na hatari kuwahi kutokea tangu tupate uhuru.

Mama hali ni ngumu mno tena ni ngumu mno hao vijana wako ni matapeli wanakupotosha huku mtaani mambo ni magumu mno watu wamechoka chakali! wanakuita majinamengimengi mwisho wa siku watatoka hapo yatakuwa kama ya srilanka.
Una ushahidi?
 
Kama Mwendazake aliweza hakuna atakayeshindwa..
 
Back
Top Bottom