Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

SINTOFAHAMU kubwa iliyoletelezwa na MKATABA TATA WA BANDARI YETU YA TANGANYIKA!
Siyo bandari moja, ni bandari ZOTE za Tanganyika. Na kuna waungaji mkono!
1686648020019.png


1686647940225.png
 
Keyboard worriors
Unao uhuru kusema hivyo ila je toka uwe na akili timamu ni jambo lipi liliwahi kuwaleta Watanzania kulihoji bila kujali itikadi za vyama vyao kama hilo la BANDARI?!

Hilo ni zaidi ya uwazavyo na ndiyo maana limedumu kwa takribani wiki nzima bila kuchuja, jiulize?
 
Unao uhuru kusema hivyo ila je toka uwe na akili timamu ni jambo lipi liliwahi kuwaleta Watanzania kulihoji bila kujali itikadi za vyama vyao kama hilo la BANDARI?!
Kuhoji Kuna faida gn kama hujibiwi na mkataba ushapita hivyo. Unakuwa kama lofa vile unahoji lakini wanakuona pungazeze tuu mbwa wakubweka.
 
ripoti ya CAG ft kuuzwa kwa BANDARI lazima mnyooke

Watu wanataka wakasomeshe watoto wao uingereza huko wanaforce pesa ili watoto wao wasome waje kuwa wabunge, mawaziri Na maraisi waendelee kutuburuza
 
Ni ajabu kuendelea kuona bunge na taasisi mbalimbali za serikali zikiendelea na shughuli za kila siku ilhali taifa limekubwa na sintofahamu kubwa iliyoletelezwa na mkataba tata wa bandari yetu ya Tanganyika.

Vilevile ni ajabu kuendelea kumshuhudia rais samia akiendelea kuziba masikio pamoja na lawama lukuki anazoshtumiwa kwazo kwa yeye kuruhusu makubaliano ya mkataba ule tata yaendelee.

Ukweli ni kwamba taifa linashuhudia mtanzuko wa ajabu kuanzia kijijini hadi mijini kulihusu jambo lile.

Samia jitokeze ulisemee hilo na ikiwezekana sitisha jambo hilo kwa maslahi mapana ya nchi.

Tofauti na hapo jambo hilo halitokuacha salama ki siasa.
Ajabu ya watanzania ni kuombea na kusubiri majizi yapate ajali za kisiasa ilhali rasilimali zimeshapigwa mnada, najiuliza hiyo ajali ya kisiasa itarejesha rasilimali zilizofisadiwa na kunonesha mifuko ya watawala!? Ajabu ya Karne!!
 
Sina maneno mengi ndugu zangu hebu kula chuma iyo [emoji116][emoji116][emoji116]
 

Attachments

  • b550ee98759bd0ff8ae0a6f4263ab181.mp4
    905.2 KB
Huyo ndiye Rais wa nchi hiyo cheap popularity inaingiaje?

Mkitaka msitake yeye ndiyo kiongozi mkuu wa nchi na ndiye aliyeachiwa hatamu ya uongozi, mbona aliyepita kuna miradi aliiwacha hivyo hivyo?

Tuwe na subira, kwani yeye hajatoka upinzani ni kiongozi wa CCM ileile na ilani ileile kinachotofautiana ni utendaji tu. Ukizingua unazinguliwa.
Tunaomba mrejesho
 
Tunaelekea Dubai sasa,uko mtaoga na mtavaa nguo Mpya,mtakula na kushiba,au mnataka tuwauze tena Marekani??
 
Mbona kama naona nchi inaelekea pabaya? Hata hii mikataba uchwara wanayo taka kusaini hamuioni? Au hamna meno ya kuuma?
 
Back
Top Bottom