Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Kwa siku nyingine tena tupo gizani baada ya umeme kukatwa. Hakuna ratiba yoyote ya siku ya wiki wala saa. Umeme unakatwa na kurudishwa na Wahusika wakiamua au tuseme kama wapendavyo na bila taarifa. Hakuna tamko lolote kuhusu hali hii kutoka kwa kiongozu wa nchi, na imeishia wateuøe wake kila kuchao wanakuja na matamko mbalimbali kinzani ya lini adha hii itafikia tamati. Kee hii nchi Rais kweli yupo na anafahamu uhalisia wa maisha haya ya mateso matupu kwa Raia wake? Huyu Rais kama kweli yupo kwanini anajificha na haonyeshi kuguswa wala kujali?

Mtamkumbuka Ngosha.
 
Mlisema tatizo ni. JYM , amekuja Biteko ambae haijulikani kama ni m Tanzania ; ndio ameshika hilo eneo

Now thus far amesha prove failure

Leo amesema wazi, hajui ni lini ishu ya umeme itaishi

Miaka 60 ya uhuru, si mchezo
 
Yule mwamba JPM aliweza sana

Hadi Leo najiuliza yule msukuma aliwezaje?

Hakukua na shida ya dolaa

Hakukua na shida umeme

Petrol by that time was 1780/L

Ujenzi wa miundombinu ilikuwa inaenda kwa kasi
Hakukuwa na tozo

Dah

Huyu mwamba aliwezaje jamani

Tangu mwamba asepe : tumerudi enzi ya 2014/5
 
CCM mnatuachia sana shida kwa wajukuu zetu, walau hawa wazee waliosoma kipindi cha mkoloni na Tanu wameweza kudhibiti zile akili za mapinduzi.

Huko mbele na hawa watoto wenu mnaowaandaa kuja kushika dola mtaleta hekaheka sana maana mapinduzi yatakuwa kila baada ya wiki.
 
Mkuu tunamlaumu bure yule mama, hakutegemea kuvaa viatu alivyonavyosasa, urais unahitaji watu waliojipanga, wakasukwa wakaiva.

Sasa kwa mama umekuja kwa bahati, pia nchi kwasasa mahaba mengi, hana maamuzi maana hajui afanye nn
Kama Hana uwezo si ajiuzuru akakae na familia yake, na siyo kama Hana uwezo, ni Hana uwezo kabisa
 
1. Sukari imeadimika hakuna kauli ya Rais
2. Umeme ni mgawo wa kikatili hakuna kauli ya Rais.
3. Dola imeadimika hakuna kauli ya Rais.
4. Maji ni mgawo katika miji mikubwa hakuna kauli ya Rais
5. RUSHWA na ufisadi uliokithiri hakuna kauli ya Rais
6. Miradi mingi ya kimkakati na Ile yenye tija inasuasua hakuna kauli ya Rais
7. Wananchi wanaambiwa watumie hii fursa ya kuadimika kwa sukari kulinda afya zao kwasababu sukari ni hatar kiafya hakuna kauli ya Rais.
8. Kudorora kwa huduma za umma hakuna kauli ya Rais
9. Wananchi kunyanyaswa na watumishi wa umma kwa kejeli na majigambo hakuna kauli ya Rais
10. Nchi haileweki Ina vision Gani wala mwelekeo Gani hakuna kauli ya Rais.
Je huyu Rais anamuongoza nani?
Je ni Rais wa matajiri tu?ana lengo Gani na nchi yetu?
Kwanini asikae pembeni waje wengine wenye Nia ya dhati na wachapa kazi. Wananchi wamekosa matumaini kabisa kwake.
Mimi sitakuchagua hata nishikiwe bastola hufai na ondoka kabisa
 
View attachment 2912089

Kwa hiyo huyu ndiye tunamsubiri atutatulie changamoto za umeme?

Huyu ndiye tunamtegemea amalize changamoto zetu za kupanda bei ya sukari?

Huyu ndiye tunayemtegemea atumalizie changamoto zetu za hali duni ya maisha, umasikini, huduma mbovu za afya, maji na miundombinu? Na mateso ya umasikini tunayopitia?

Huyu ndiye tunayemtegemea atutoe kwenye orodha ya nchi masikini tunayoishi chini ya dola 1 walau tufikie kupata milo mitatu kwa siku?

Ok. Basi Sawa.

NB: Mods naomba msichanganye uzi wangu na ule mwingine. Maudhui ni tofauti.
 
1. Sukari imeadimika hakuna kauli ya Rais
2. Umeme ni mgawo wa kikatili hakuna kauli ya Rais.
3. Dola imeadimika hakuna kauli ya Rais.
4. Maji ni mgawo katika miji mikubwa hakuna kauli ya Rais
5. RUSHWA na ufisadi uliokithiri hakuna kauli ya Rais
6. Miradi mingi ya kimkakati na Ile yenye tija inasuasua hakuna kauli ya Rais
7. Wananchi wanaambiwa watumie hii fursa ya kuadimika kwa sukari kulinda afya zao kwasababu sukari ni hatar kiafya hakuna kauli ya Rais.
8. Kudorora kwa huduma za umma hakuna kauli ya Rais
9. Wananchi kunyanyaswa na watumishi wa umma kwa kejeli na majigambo hakuna kauli ya Rais
10. Nchi haileweki Ina vision Gani wala malengo Gani hakuna kauli ya Rais.yupo mafichoni tu.
Je, huyu Rais anamuongoza nani?
Je, ni Rais wa matajiri tu?ana lengo Gani na nchi yetu?

Kwanini asikae pembeni waje wengine wenye Nia ya dhati na wachapa kazi. Wananchi wamekosa matumaini kabisa kwake.

Mimi sitakuchagua hata nishikiwe bastola hufai na ondoka kabisa
 
Dah! Hali ya maisha imekuwa ni ngumu kweli kweli. Kama sisi wenye wategemezi, ndiyo tuna wakati mgumu kweli kweli. Halafu kuna watu eti wanampigia chapuo aendelee mpaka 2030!!

Si tutatafika tukiwa tumechoka sana, kama hali yenyewe ndiyo hii. Yaani nchi kwa sasa inamilikiwa na wapiga dili!! Hali imekuwa si hali tena. Hata Magu alikuwa na madhaifu yake mengi, ila Bi Mkubwa nadhani amezidi. Maana yupo kama figure head tu. Hana kabisa maamuzi.
 
Kama wewe ni jobless maana yake huna kazi unaelewa, gharama za maisha zilipanda kila pembe ya nchi.

Tozo, kupanda kwa nauli, kupanda bei ya vyakula, nk.

Haya yanatosha kuwa na Rais mwingine awe wa CCM au upinzani.
 
Tatzo mnatak viti vya kuzunguka na Ofisi zenye Ac ,vijana mjiajiri kazi zipo nyingi
 
Back
Top Bottom