Megalodon
JF-Expert Member
- Apr 9, 2021
- 3,534
- 7,866
Kwa siku nyingine tena tupo gizani baada ya umeme kukatwa. Hakuna ratiba yoyote ya siku ya wiki wala saa. Umeme unakatwa na kurudishwa na Wahusika wakiamua au tuseme kama wapendavyo na bila taarifa. Hakuna tamko lolote kuhusu hali hii kutoka kwa kiongozu wa nchi, na imeishia wateuøe wake kila kuchao wanakuja na matamko mbalimbali kinzani ya lini adha hii itafikia tamati. Kee hii nchi Rais kweli yupo na anafahamu uhalisia wa maisha haya ya mateso matupu kwa Raia wake? Huyu Rais kama kweli yupo kwanini anajificha na haonyeshi kuguswa wala kujali?
Mtamkumbuka Ngosha.